Tuesday, 8 September 2015

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] NANI ANAWAFADHILI CCM, UKAWA?

PESA YA ESCROW NDO ZINATUMIKA MAKE BIL203 SI MCHEZO
--------------------------------------------
On Tue, 8/9/15, Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] NANI ANAWAFADHILI CCM, UKAWA?
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: Wanazuoni@yahoogroups.com, wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, 8 September, 2015, 15:09

Dan

wewe afadhali bado unafikiri.  waandishi wengi wenziyo
wamezolewa na mafuriko
On Sep 8, 2015 2:29
PM, "Daniel Mbega" <mbega.daniel@gmail.com>
wrote:
NANI ANAWAFADHILI CCM,
UKAWA?


Na Daniel Mbega
KILIO cha muda mrefu cha Watanzania ni kudumaa kwa maendeleo
na kukua kwa tabaka la maskini kunakochangiwa na mfumo usio
rasmi wa ufisadi uliotamalaki kiasi cha kuua maadili ya
utumishi wa umma.
Misingi imara iliyowekwa na waasisi wa taifa hili imevunjwa
kwa makusudi na wale waliopewa dhamana ya uongozi, jambo
ambalo limefanya pengo kati ya walionacho na wasionacho liwe
kubwa zaidi.
Japokuwa ufisadi umekuwepo kwa miaka mingi nchini, lakini
kashfa zimewekwa hadharani katika kipindi hiki cha awamu ya
nne ya uongozi wa Jakaya Kikwete, ambaye pamoja na kushindwa
kutoa maamuzi magumu katika baadhi ya mambo, lakini
amethubutu kuweka uwazi na kuacha sheria ichukue mkondo wake
kwa baadhi ya watu waliotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu kuna
maswali mengi ya kuwauliza wanasiasa, hususan wa CCM na wale
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba fedha
wanazofanyia kampeni wamezitoa wapi.
Pamoja na ukweli kwamba ipo Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya
mwaka 2010 na Sheria Namba 1
ya Uchaguzi ya mwaka 1985,
lakini kwa hali inavyoonekana sheria hizi hazifuatwi kwani
dhahiri gharama zinazotumiwa na vyama hivyo ni kubwa kuliko
sheria inavyoelekeza.Sheria ya Gharama za Uchaguzi
inaagiza, gharama za kampeni kwa Mbunge zinapaswa kuwa Shs.
30 milioni na zisizidi Shs. 80 milioni kulingana na ukubwa
wa jimbo husika, na kwa upande wa kampeni za urais,
zinapaswa zisizidi Shs. 6 bilioni.Sheria ya Gharama za Uchaguzi
madhumuni yake ni kujenga mazingira yatakayowezesha kuwapo
kwa uwazi zaidi katika matumizi ya fedha zitakazotengwa kwa
ajili ya kampeni, pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa
ndani ya vyama vya siasa katika uteuzi wa mgombea na
uchaguzi wenyewe kwa ujumla.Sheria hiyo inaelezea masharti
kuhusu fedha zitakazotumika kwa ajili ya uchaguzi, maana ya
gharama za uchaguzi, uchaguzi ndani ya Vyama vya Siasa,
gharama ambazo vyama vya siasa vinapaswa kutumia wakati wa
uchaguzi, masharti kwa Vyama vya Siasa na wagombea kutoa
taarifa kuhusu gharama zitakazotumika wakati wa
uchaguzi.Aidha, sheria hiyo
inazungumzia kuhusu michango au misaada inayotolewa na
kupokewa na vyama vya siasa, kuzuia fedha kutoka nje ya nchi
kwa ajili ya kampeni za uchaguzi, matumizi ya gharama kwa
vyama na taasisi za kiserikali wakati wa kutoa elimu ya
Kampeni na chaguzi za kisiasa.Tumeshuhudia jinsi chaguzi za
ndani za kura za maoni kwa CCM na Chadema zilivyogubikwa kwa
rushwa na kuna baadhi ya wagombea ambao walidakwa na Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wengine
wakaenguliwa na vyama vyao kwa matukio
hayo.Sehemu ya tano ya sheria hii
inahusu masharti yanayokataza baadhi ya matumizi ya fedha
kama gharama za kampeni na uchaguzi. Matumizi hayo ni yale
yanayohusu gharama kwa vitendo vinavyozuiwa au kuwa haramu
wakati wa kampeni na uchaguzi.Sheria inasema kila chama cha
siasa kitagharamia kampeni za uchaguzi kwa kutumia gharama
za uchaguzi zinazotokana na vyanzo vyake, kwa mujibu wa
kifungu cha 8(1) cha sheria hii. Na kifungu cha 8(2)
kimezingatia kuwa mgombea anaweza kutumia gharama zake
mwenyewe wakati wa kampeni pale inapobidi kulingana na
mahitaji ya kampeni zake.Sheria hii inaweka sharti la
uwazi katika mapato na matumizi ya vyama na wagombea kwa
ajili ya uchaguzi kabla, wakati wa uchaguzi na baada ya
uchaguzi na katika kifungu cha 9(1), inasema: "Mgombea
atatakiwa kutoa taarifa ya fedha alizonazo na anazotarajia
kupata na anakusudia kuzitumia kama gharama za uchaguzi
ndani ya siku saba (7) baada ya siku ya uteuzi. Taarifa hizo
zitawasiliskwa kwa Katibu Mkuu wa chama kwa mgombea wa
nafasi ya Urais na kwa mgombea wa nafasi ya Ubunge na
Udiwani taarifa zake ataziwasilisha kwa Katibu wa Chama
wilaya."Kila chama cha siasa
kinachoshiriki katika uchaguzi ni lazima ndani ya siku
thelathini (30) baada ya siku ya uteuzi wa wagombea kufanywa
na Tume ya Uchaguzi kitoe taarifa kwa Msajili juu ya fedha
zote ambazo kinakusudia kutumia kama gharama za uchaguzi; na
kutumia kwa kuwadhamini wagombea wa chama hicho zikiwa ni
kama gharama za uchaguzi.Pamoja na maelekezo hayo ya
Sheria, lakini bado hakuna atakayekuwa na uhakika zilikotoka
fedha hizo, zina masharti gani na ni kiasi gani hasa, kwa
sababu naamini hakuna anayeweza kueleza kiwango halisi cha
bajeti yake – si kwa...http://www.brotherdanny.com/2015/09/nani-anawafadhili-ccm-ukawa.html



--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER &
PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
               www.brotherdanny5.blogspot.com

"Kama
hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?"
~ Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es
Salaam, 1995




--

Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la
'Mabadiliko'.

Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

 

 

For more options, visit this group at:

http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Mabadiliko Forum" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.

To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.

Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.

To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAE93EM_8LrDcb79-%3Dv627TC9-FPmpr%2BOzBLHPXWqCmMD9a9AfQ%40mail.gmail.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment