Thursday, 10 September 2015

Re: [wanabidii] Kwa nini Rose Kamili si kamili

Bakari nakushukuru umetoa hoja yangu. Ubarikiwe sana.
Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 9/10/15, 'salhabakari' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Kwa nini Rose Kamili si kamili
To: "'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, September 10, 2015, 5:58 AM

Elisa, Kama una uwezo,
beba mimba, zaa, tunza watoto kwa style hiyo, kisha utajua
nini la kufanya.Mwache Rose Kamili afanye anayoyaona
yanamfaa kama mama.Wewe ni mwanamme, huwezi kuvaa uanamke
hata siku moja!
SB
On Sep 9, 2015 11:12 PM,
'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kwa nini Rose Kamili si kamili


MALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya
mke wake wa
zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod
Slaa, Rose
Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa
mume wake
huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.




Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk.
Slaa
anatangaza kung'atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila
mihogo na
familia yake, jambo ambalo si la kweli.



Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya,
lakini watoto
wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea
chakula
hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.



Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,
alisema Dk Slaa
aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa
urais wa
Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri
Mkuu wa
zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa
akiwasiliana na
viongozi hao.



Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na
CCM kugombea
ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa
kuomba ushauri.


Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza
kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama
chochote.



Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji
hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi?


Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk
Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.



Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa
akishindia mihogo
na familia yake ili aisadie Chadema ni lugha ya picha
ambayo haikuwa na
maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.



Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa
kuisaidia
Chadema kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia
yake na hata
wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni
ili chama
hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala
njaa.



Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba
alazimishe
kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha
Ukawa.


Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa
kisiasa na
CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata
yeye basi
anatumiwa na Ukawa kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?



Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha
familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho.

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment