Tuesday, 8 September 2015

Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA

hao ndo maprofesa tulio nao, kuna mmoja anaitwa prof. maji marefu; angejibu hivyo nisingeshangaa, lakini hata huyu anaweza kujibu kirahisi namna hii! Kazi tunayo.



On Wednesday, September 9, 2015 2:15 AM, 'salhabakari' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Hapa Naona mwandishi umeamua kufanya unyanyasaji wa kijinsia tu.Ina maana dada Nkya Ananilea si mtu huru wa kujadili na kutoa mapendekezo yake.This is not good.Tuwe wamoja! Please tusitishane!
SB
On Sep 8, 2015 9:47 PM, Magora Hassan <magorah15@gmail.com> wrote:
Hili swali la mama Nkya linakusudia kujua ukweli au ni sehemu ya mwendelezo wa tuhuma dhidi ya wale wote wasiokubalina na kile anachokiamini? ACT WAZALENDO waliandika barua kuomba utaratibu wa kujiunga na UKAWA,badala ya kujibiwa aliibuka Mh John Mnyika tena kwenye mkutano wa hadhara na kusema kuwa adui yao mkubwa ni ZZK. Swali la kwanini ACT hawakujiunga na ukawa linapasa kujibiwa na wana ukawa/cdm hai na hata wale UKAWA /CDM MFU kama  Mama Nkya ambaye bado anajificha nyuma ya utetezi wa maslahi mapana ya taifa.
On Sep 8, 2015 4:25 PM, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mwalimu wangu Prof Kitila.
Nimesoma hoja yako. Hata hivyo nikusahihishe kwamba sina chama chochote cha siasa  ninachofungamana nacho. Kama umekuwa ukifuatilia vemakwenye hoja zangu zimekuwa zikilenda kutetea maslahi ya  mamilioni ya Watanzania ambao siasa zetu zimekuwa zikiwafanya maskikini ili hali watawala wachache wakitajirika kupindukia.

Nimetoa hoja kwamba  hali hii inasababishwa na mfumo wa vyama vingi nchini kutofanya kazi kwa sababu vyama vya upinzani vilipaswa kuunganisha nguvu ili kuleta siasa zenye ushindani  mkubwa.

Ndipo nikauliza swali ni kwa nini ACT-Wazalendo hawakujiunga na UKAWA  ili vyama vya upinzani viwe na nguvu kubwa zaidi? Wewe umenijibu kwa kebehi kwamba nikaulize UKAWA. Sijui ni kwa nini unataka nikaulize UKAWA  swali ambalo linapaswa kujibiwa na ACT-Wazalendo. Mwalimu ni kwa  nini unataka swali linalohusu chama chako lijibiwe na UKAWA?


Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Tue, 9/8/15, Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA
 To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Tuesday, September 8, 2015, 9:05 AM

 Dada
 Ananelia,
 Waingereza
 wanasema 'seek truth from facts'.  Ni muhimu sana.
 Mambo mengi unayoandika yamejaa hisia zisizoshabiana hata na
 chembe ya ukweli. Ni vizuri ukatafuta ukweli wote kuhusu ACT
 na hata mazungumzo yaliyofanyika kuhusu uwezekano wa chama
 hiki kuwa sehemu ya UKAWA na kitu gani hasa
 kilikwamisha-sababu za msingi na zisizo za msingi. Ongea na
 makamanda wenzako ndani ya UKAWA/CDM watakwambia ukweli. Ni
 muhimu sana. 
 Angalizo: kwa mnaojiunga na vyama
 vya siasa vya upinzani ukubwani, kuwa mwanachama wa chama
 cha siasa sio lazima utetee kila kinachohusu chama chako.
 Kuna mengine unakaa kimya tu. Kwa maneno mengine, kuwa
 mwanachama wa chama cha siasa hakukufanyi ukapoteza uhalali
 wako wa kufikiria bila kujipendekeza kwa chama. Uanachama wa
 chama cha siasa sio kama ulokole ambao unakulazimisha kusema
 Bwana Asifiwe kwa kila jambo lililopo katika Biblia.
 Nalisema hili kwa sababu naona wanachama wapya katika vyama
 vya siasa vya upinzani wanatupa kwa kasi misingi ya
 kusimamia ukweli waliojijengea muda mrefu. Yaani hadi
 mnawazidi 'waliokoka' siku nyingi! 
 Kitila. 
 Kitila

 2015-09-08 8:23 GMT+03:00
 De kleinson kim <dekleinson@gmail.com>:
 Mama Kiwasila,
 Ni kweli tupu, ukisema sana wahafidhina
 watakujalia hapa wamefunga kanga nusu, na matarumbeta ati
 kukusuta.
 Kumbe maskini ya Mungu hawaelewi muda, hawajui
 faida ya uongozi, hawafikiri taifa la kesho, hawafikirii
 maendeleo ya wengi, wao huamini wao ndio bora! hata
 hawaelewi kwa nini tunatakiwa kuendelea, hawajui kwa nini
 sie ni maskini?
 Na kama wanajua hayo, si bure wameweka nafsi
 yao mbele, UMIMI!!
 Kinachotusumbua watu weusi ni kile kilichopo
 ndani ya elimu. tunasoma kweli na kufaulu, lakini kama hiyo
 elimu haikupi akili ya kujiongeza, then still workdone =
 0!!! umesoma utawala, sheria, IT, e.t.c but still you cant
 do logic ques.. we ni msomi wa aina gani sasa? labda wa
 mitihani!!
 Kama tutaendelea hivi, tutaishia kuuliza na
 kusifiana "umekuwa wa ngapi?" "ana GPA
 ngapi" "Amepewa Honors" n.k. lakini suluhu ya
 matatizo ndani ya jamii yetu hakuna!!! tunashangilia
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment