Tuesday, 8 September 2015

Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA

Dada Ananelia,

Waingereza wanasema 'seek truth from facts'.  Ni muhimu sana. Mambo mengi unayoandika yamejaa hisia zisizoshabiana hata na chembe ya ukweli. Ni vizuri ukatafuta ukweli wote kuhusu ACT na hata mazungumzo yaliyofanyika kuhusu uwezekano wa chama hiki kuwa sehemu ya UKAWA na kitu gani hasa kilikwamisha-sababu za msingi na zisizo za msingi. Ongea na makamanda wenzako ndani ya UKAWA/CDM watakwambia ukweli. Ni muhimu sana. 

Angalizo: kwa mnaojiunga na vyama vya siasa vya upinzani ukubwani, kuwa mwanachama wa chama cha siasa sio lazima utetee kila kinachohusu chama chako. Kuna mengine unakaa kimya tu. Kwa maneno mengine, kuwa mwanachama wa chama cha siasa hakukufanyi ukapoteza uhalali wako wa kufikiria bila kujipendekeza kwa chama. Uanachama wa chama cha siasa sio kama ulokole ambao unakulazimisha kusema Bwana Asifiwe kwa kila jambo lililopo katika Biblia. Nalisema hili kwa sababu naona wanachama wapya katika vyama vya siasa vya upinzani wanatupa kwa kasi misingi ya kusimamia ukweli waliojijengea muda mrefu. Yaani hadi mnawazidi 'waliokoka' siku nyingi! 

Kitila. 

Kitila

2015-09-08 8:23 GMT+03:00 De kleinson kim <dekleinson@gmail.com>:

Mama Kiwasila,

Ni kweli tupu, ukisema sana wahafidhina watakujalia hapa wamefunga kanga nusu, na matarumbeta ati kukusuta.

Kumbe maskini ya Mungu hawaelewi muda, hawajui faida ya uongozi, hawafikiri taifa la kesho, hawafikirii maendeleo ya wengi, wao huamini wao ndio bora! hata hawaelewi kwa nini tunatakiwa kuendelea, hawajui kwa nini sie ni maskini?

Na kama wanajua hayo, si bure wameweka nafsi yao mbele, UMIMI!!

Kinachotusumbua watu weusi ni kile kilichopo ndani ya elimu. tunasoma kweli na kufaulu, lakini kama hiyo elimu haikupi akili ya kujiongeza, then still workdone = 0!!! umesoma utawala, sheria, IT, e.t.c but still you cant do logic ques.. we ni msomi wa aina gani sasa? labda wa mitihani!!

Kama tutaendelea hivi, tutaishia kuuliza na kusifiana "umekuwa wa ngapi?" "ana GPA ngapi" "Amepewa Honors" n.k. lakini suluhu ya matatizo ndani ya jamii yetu hakuna!!! tunashangilia qualification but not quality of it in return!!!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment