Kuna mtu alisema maswali haya hayatajibiwa. nimeamini ukweli huo. Nimemkumbuka marehemu Horace Kolimba. Alikuwa akiulizwa sawali akianza kujibu anatumia maneno mengi kutojibu swali.
--------------------------------------------
On Tue, 9/22/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] CCM WANAJIDANGANYA
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Tuesday, September 22, 2015, 1:09 AM
Mwalimu Malata
Nianze kwa kukushukuru kwa kusoma makala zangu
ninazoweka kwenye jukwaa hili la
mabadiliko. Niwashukuru pia wengine wote
kwa kusoma na kuchangia hoja niliyoandika kuhusu CCM
kujidanganya.
Mwalimu Malata nashukuru kwa maandishi
yako ambayo uliyosema ni
maswali. Lakini nilipoyapitia mengi
hayakuwa ni maswali kwa
sababu kama umekuwa ukisoma
hoja ambazo nimekuwa nikiandika humu jukwaani tangu
kampeni za uchaguzi zianze, usingeuliza
maswali haya. Hata hivyo sikulaumu sana hii ndiyo
shida ya bora elimu ambayo Watanzania
wamekuwa wakiipata.
Ninachokushauri, hata kama wewe ni mwanachama wa CCM au
chama kingine cha siasa, ni vema ukasoma na kutafakari
kwa kina hoja zinazoandikwa na watu mbali mbali
humu jukwaani maana zitakusaidia kupata upeo
kama kweli wewe ni mwalimu na kama unaamini kwamba
Tanzania inahitaji mabadiliko ya
uongozi vinginevyo haya mafuriko ya
wananchi maskini yaliyotengenezwa na serikali ya CCM
yakiachiwa kuendelea kuzalishwa kutahatarisha
amani ya nchi yetu tuendako.
Nimejibu kama ifuatavyo:
(A) Umesema "…Chama cha Mapinduzi (CCM) na
serikali yake wanapaswa wasijidanganye
kwamba kwa kumteua Dr John Magufuli kuwa mgombea wa
Urais chama hicho kimekuwa kisafi..."
1. Je, usafi na AU uchafu wa chama
unatokana na nini?
Jibu: Usafi au uchafu
wa chama cha siasa unatokana na misingi ambayo chama
kinakuwa kimejiwekea. Kwa mfano CCM zama za
Mwalimu Julius Nyerere iliweka Azimio la Arusha kama msingi
wa kujenga usafi wa wanachama na viongozi .
Lakini baada ya Mwalimu kuondoka
madarakani CCM ilizika Azimio la Arusha na hivyo
kiliagana na usafi kikaanza kukumbatia uchafu.
CCM ya leo haiamini tena katika usafi uwe ni wa wanachama
wake mmoja mmoja au chama kizima. Tangu CCM
kilipozika azimio la Arusha --kilizika
misingi yake ya usafi na kikaasisi misingi ya
uchafu—ufisisadi, rushwa na ubabe na ndiyo sababu
kwa kuwa ndicho kimekuwa kikiongoza serikali nchi
nzima sasa inanuka uchafu wa ufisadi na
rushwa. Kibaya zaidi CCM iliondoa
Azimio la Arusha bila kuweka kitu kingine badala
yake. Hata wananchi walipoamua kuandika Katiba
Mpya inayotokana na maoni yao kama mbadala wa Azimio
la Arusha serikali ya CCM imekataa hiyo
Rasimu ya Katiba na iliizika
rasmi pale Dodoma mwaka jana 2014 tena kwa kufanya
ufisadi mchana kweupe kwa kuwalipa wanaCCM wajumbe wa
Bunge la kila mmoja shilingi laki tatu kwa
siku kwa siku karibu mia moja.
Tangu kuzikwa Azimio la Arusha, kila
wakati CCM ilipochaguliwa kuingia madarakani serikali yake
imekuwa inafanya ufisadi kwa sasabu CCM na serikali yake
ndiye mnufaika wa ufisadi. Kumbuka mfano ufisadi
wa EPA,Meremeta, Richmond na Tegeta escrow.
Kadhalika tangu kuzikwa kwa azimio la
Arusha kulikoiondoa CCM kwenye usafi na
kukipeleka kwenye uchafu, wananchi wengi ambao wanajua
shughuli zao siyo safi vya
kutosha wanaingia CCM. Mtu ukiwa ni
mwanachama wa CCM hata kama unapata fedha kwa njia chafu
wewe uko salama-utalijwa na hakuna mashtaka yatakufika hata
kama umehusika kwenye ufisadi. Kama huamini
angalia mawaziri waliohusika na Tegeta escrow kwa
ushahidi kabisa mwaka huu wanateuliwa kugombea ubunge
CCM na wananadiwa kama vile hawajawahi kuhusika na
ufisadi.
Lakini hata kama una tuhuma tu za
kupakaziwa kama vile Edward Lowassa ukithubutu
kujiunga na chama cha upinzani utaiona jehanamu ya
moto. Hivyo watu wengi wako CCM kimaslahi zaidi si kwa
vile chama hicho ni chama kisafi makini kinachotetea maslahi
ya mamilioni ya Watanzania. Watu wengi
wako CCM wasitiwe misukosuko hasa kama wanataka
kupata utajiri wa haraka iwe
ni kupata tenda za miradi kutoka serikali
ya CCM au uongozi ili kujitajirisha huku
mamilioni ya wananchi wakibaki maskini. Lakini subiri baada
ya tarehe 25 Oktoba, kama mamilioni ya
Watanzania maskini ambao serikali ya CCM
imewazalisha baada ya kuacha misingi ya kuongoza
nchi kwa usafi wataamua kuiondoa
CCM madarakani—utaona jinsi CCM itakavyokufa
kutokana na kukimbiwa na wanachama maslahi.
2. Kwa mtazamo wako CCM si kisafi?
Ulitegemea CCM wafanye nini ili kuwa safi katika kipindi
hiki kuelekea uchaguzi mkuu? Jibu: soma majibu
ya swali No 1.
3. Je, Unaamini katika
"KUJISAHIHISHA"? Jibu: soma majibu
swali No 1.
(B) Umesema "…Hivyo hakuna
mamtiki yoyote kwa CCM kutumia propaganda kwamba kwa
mgombea wake wa Urais kupata watu kwenye mikutano
ya kampeni basi tayari kimeshinda kwa asilimia
69.3…… Kama umati wa watu ndicho
kigezo cha ushindi wa CCM ….".
1. Bila shaka ni wazi kuwa unatambua
kuwa CCM ni taasisi na si kijiwe cha wahuni. Kwa maendeleo
endelevu ya Taasisi yoyote ni budi iwe na idara/kitengo
maalumu kwa ajili ya M & E. N a kama taasisi bila shaka
CCM ina "policy kuhusu namna ya kutathimini mwelekeo
wake.
2. Je ni dhambi kwa taasisi kufanya
tathmini na kutoa matokeo kwa umma?
Jibu: Kujitathmini siyo dhambi. Dhambi ni kujitathmini bila
kutumia vigezo vya kutoa tathmini ya ukweli.
Watanzania wanaojua hali halisi ya
umaskini unaowakabili mamilioni ya Watanzania
wanajua hiyo asilimia
69.3 ambayo CCM imejinasibu kuwa
itapata kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2015
haiwezekani katika Tanzania ya leo kama
uchaguzi utakuwa huru. Kama
hiyo tathmini ni ya kweli leo CCM
katika kampeni zake isingekuwa inatoa kauli
za kutisha wananchi
kwamba vyama vya upinzani hasa
CHADEMA ndani ya
UKAWA vikichaguliwa nchi itaingia
kwenye machafuko. Au kauli za kuweweseka
zinazotolewa na baadhi ya na
viongozi waandamizi wa CCM wanaposimama kwenye
majukwa mchana kweupe na
kusema kwamba katika jambo lolote ambalo CCM
haiwezi kufanya ni kuwapa wapinzani nchi
waongoze. Jiulize je nchi hii ni mali ya
CCM? Ni kwa nini viongozi wa
CCM wanang'ang'ania madaraka kama siyo
madaraka hayo yananufaisha viongozi
wachache na kufukarisha wananchi? Muhimu
zaidi jiuliza hivi chama cha siasa ambacho kimefanya utafiti
na kikabaini kweli kwamba kuna kila dalili ya
kushinda kwa asilimia 69.3 ni kwa nini basi kiwe na
wasiwasi na kutoa kauli za uvunjivu wa amani
na kutaka kuvuruga uchaguzi?
Kwa mwenye akili yake ya kufanya uchambuzi
atabaini kuwa hizo data ni propaganda
na pengine ni mbaya kwa chama
hicho pengine kuliko 2010 ilipochakachua kura za
Rais kwa zaidi ya wiki mbili. Hivyo inachokifanya sasa ni
ufisadi wa maneno kutisha
wananchi wasijitokeze kupiga kura. Lakini
CCM wanajidanganya maana Watanzania wengi wa leo
HAWADANGANYIKI kama wameamua kufanya
mabadiliko ya uongozi wan chi yao hapo tarehe 25 Oktoba
mwaka huu 2015. Watavaa kanga, kofia, fulana, watakula
na kunywa, watapokea fedha n a hata fedha za
ufisadi wa Tegeta escrow zilizochotwa kwa tandarusi na
magunia zikitumika kuwalipa gharama za
kusafiri kwenda kuhudhuria mikutano ya kampeni
mikoa mingine kujaza uwanja kutengeneza taswira
ya kupendwa watafanya hivyo, lakini tarehe 25
watafanya maamuzi --kubadilisha uongozi unaofukarisha
mamilioni na kutajirisha mamia kadhaa tu ya watawala.
3. Una ushahidi gani wa kutuaminisha
kuwa CCM wametumia kigezo cha wingi wa watu katika kampeni
kutoa tathimini yao? Jibu: soma hiyo taarifa ya CCM.
4. Je propaganda ni nini na
kwa nini? Jibu: Ni kujifurahisha na kujihami)
5. Je, unachokifanya ni sehemu ya hizo
propaganda au? JIbu: Utakavyoona wewe . Una
haki ya kuwa na mtazamo na maoni yako sikuzuii)
(C) Umesema "…Rais Jakaya Kikwete katika
kipindi ccha utawala wake amesafiri nje ya nchi mara
409 na safari hizo ziligharimu shilingi
trilioni 4.5……Maana yake angalao kila mwaka Rais
alisafiri nje ya nchi mara 40 akipoteza siyo tu fedha
alizotumia kwa safari hizo bali pia muda mwingi wa
kuwatumikia Watanzania…."
1. Katika maelezo yako hayo hapo juu,je
unaweza kutuainishia bajeti ya serikali kwa Idara ya Itifaki
kwa mwaka kuanzia mwaka 2005 hadi sasa? Jibu:
Kama una tofauti na hiki nilichoandika hapa ni wajibu
wako kutuwekea hapa. Kama huna kaa kimya)
2. Kama hujakurupuka na kumeza matango
poli kasha kuwatapikia watanzania kuhusu jambo hilo, Je
unaweza kutuaninishia kutuainishia safari hizo na
bajeti yake kwa kila safari ili tujiridhishe na tarakimu
uliyotaja hapo?
Jibu: Soma majibu No
1 hapo juu. Kadhalika niongeze hapa kwamba kwa wewe
mwenyewe kutumia lugha chafu hapa unaendelea
kutuaminisha kuwa hiyo tathmini ni ya
kujidanganya na kujenga saikolojia ya goli la mkono au
ufisadi wa maneno ili kuvuruga uchaguzi)
3. Unaposema alipoteza muda wa
kuwatumikia watanzania kwa hizo safari, Je zilikuwa safari
zake binafsi [I mean was it for the personal issues/family
matter or for the sake of our
country? Jibu: Alipoteza muda wa umma
kwenda kuomba net na kuchukua digrii za heshima ili
hali nchi yetu inawalipa mabalozi mishahara kufanya kazi
hizo.
4. Ikiwa unaamini, kama mimi ninvyoamini
kuwa zilikuwa safari za kikazi; Je unaweza kuueleza umma wa
Tanzania Impact ya kila safari ya Mh.Raisi with reference to
matumizi kwa kila safari? Jibu: Madhara ya hizo
safari ni kutengenezwa kwa mamilioni ya
Watanzania maskini ambao ndio wamejiandaa kuing'oa CCM
madarakani hapo tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015.
(D) Umesema "…Je CCM na serikali ya CCM
yake mwaka huu 2015 watatumia kwa 'goli
la mkono' kuzuia maamuzi ambayo wananchi wa
Tanzania watakuwa wamefanya kupitia sanduku huru
la kura kuhusu hatma ya uongozi wa nchi yao …?"
1. Napata shida kuitafakari kauri
(sahihisho hili neno linaandikwa kauli) hii,Je
umetumia kigezo gani kusema " ..watanzania watakuwa
wamefanya kupia sanduku huru.." Je tayari una majibu ya
jambo ambalo hatujalifanya? Kama hivyo ndivyo ni hatari sana
kwa kuwa ni sawa na mtu anayeingia uwanjani akiwa na matokeo
mkononi.Nini kitatokea ikiwa
atashindwa? Jibu: Inaelekea
hufuatilii kwa makini kampeni za chama chako
CCM kusikia na kuelewa
wanachokisema. Kama hukumbuki ni nani
aliyesema CCM itashinda kwa goli la mkono basi siyo kazi
yangu kukuelimisha hilo.
2. Ikiwa na wengine watakuwa na mawazo
kama yako,huoni kama ni hatari kwa kuwa hamtakuwa tayari
kupokea matokeo kwa kuwa tu mnaamini kuwa "mtaibiwa
kura" na ccm hata kama haitakuwa hivyo? Jibu
: Kuiba kura ni ufisadi. Wenye
historia ya ufisadi
wanaotegemewa kufanya kila giliba iwe
ni kutumia maneno machafu nay a vitisho,
kuteneneza wenyewe au kutumia
taasisi za wasomi uchwara kufanya
tafiti uchwara kuonyesha wanashinda. Lakini
ukweli utabaki pale pal—maamuzi ya mamilioni ya Watanzania
maskini ambao wamefukarishwa na utawala wa serikali ya CCM
ni tarehe 25 Oktoba 2015. Tusubiri.
Nitashukuru ikiwa maswali haya yatapatiwa majibu.
Asante
______________________________
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
A D D R E S S
John J. Malata
Tutor. Vikindu TC
P.O Box 16268
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Mobile: +255 782366090
Blog:http://pengotz.blogspot.com/
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Sat, 9/19/15, 'Malata.' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: Re: [wanabidii] CCM WANAJIDANGANYA
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Saturday, September 19, 2015, 11:47 AM
Kwako Mama
Nkya
Salaam!!
Kwa muda mrefu
nimekuwa nikifatilia mwenendo wa mijadala unayochangia
katika majukwaa
mbalimbali. Wewe ni mmoja wa watu/wanaharakati
mliojipambambanua mbele ya jamii
kwa muda mrefu na kutuaminisha kuwa ninyi watu wa aina
gani.
Nimesoma kwa
umakini sana makala yako uliyoipa jina "CCM
WANAJIDANGANYA", kimsingi ni makala nzuri japo sio
bora kama ambavyo
nilitegemea kitu bora kutoka kwa mtu wa kariba
yako.
Napenda
kujadili sana mada hiyo ila tafadhali naomba nisaidie
majibu
ya maswali yangu
yafuatayo yanayotokana na mkanganyiko nilioupata kwa
maneno
yak ohayo.
(A) Umesema
"…Chama cha Mapinduzi (CCM) na
serikali yake wanapaswa wasijidanganye kwamba kwa
kumteua Dr
John Magufuli kuwa mgombea wa Urais chama hicho
kimekuwa
kisafi..."
1. Je,
usafi na AU uchafu wa chama unatokana na nini?
2. Kwa mtazamo wako CCM si kisafi? Ulitegemea
CCM
wafanye nini ili kuwa safi katika kipindi hiki kuelekea
uchaguzi mkuu?
3. Je,
Unaamini katika "KUJISAHIHISHA"?
(B)
Umesema "…Hivyo hakuna mamtiki yoyote kwa CCM kutumia
propaganda kwamba kwa
mgombea wake wa Urais kupata watu kwenye mikutano ya
kampeni
basi tayari kimeshinda kwa asilimia 69.3…… Kama
umati wa watu
ndicho kigezo cha ushindi wa
CCM ….".
1. Bila
shaka ni wazi kuwa unatambua kuwa CCM ni taasisi na si
kijiwe cha wahuni. Kwa
maendeleo endelevu ya Taasisi yoyote ni budi iwe na
idara/kitengo maalumu kwa
ajili ya M & E. N a kama taasisi bila shaka CCM ina
"policy kuhusu namna ya
kutathimini mwelekeo wake.
2. Je
ni dhambi kwa taasisi kufanya tathmini na kutoa matokeo
kwa
umma?
3. Una
ushahidi gani wa kutuaminisha kuwa CCM wametumia kigezo
cha
wingi wa watu
katika kampeni kutoa tathimini yao?
4. Je
propaganda ni nini na kwa nini?
5. Je,
unachokifanya ni sehemu ya hizo propaganda au?
(C) Umesema
"…Rais Jakaya Kikwete katika kipindi
ccha utawala wake amesafiri nje ya nchi mara 409 na
safari hizo
ziligharimu shilingi trilioni 4.5……Maana yake
angalao kila mwaka
Rais alisafiri nje ya nchi mara 40 akipoteza siyo tu
fedha
alizotumia kwa
safari hizo bali pia muda mwingi wa kuwatumikia
Watanzania…."
1. Katika
maelezo yako hayo hapo juu,je unaweza kutuainishia bajeti
ya
serikali kwa Idara
ya Itifaki kwa mwaka kuanzia mwaka 2005 hadi
sasa?
2. Kama
hujakurupuka na kumeza matango poli kasha kuwatapikia
watanzania kuhusu jambo
hilo, Je unaweza kutuaninishia kutuainishia safari hizo
na bajeti yake
kwa
kila safari ili tujiridhishe na tarakimu uliyotaja
hapo?
3. Unaposema
alipoteza muda wa kuwatumikia watanzania kwa hizo safari,
Je
zilikuwa safari
zake binafsi [I mean was it for the personal issues/family
matter or for the
sake of our country?
4. Ikiwa
unaamini, kama mimi ninvyoamini kuwa zilikuwa safari za
kikazi; Je unaweza
kuueleza umma wa Tanzania Impact ya kila safari ya
Mh.Raisi
with reference to
matumizi kwa kila safari?
(D) Umesema
"…Je CCM na serikali ya CCM
yake mwaka huu 2015 watatumia kwa 'goli la
mkono'
kuzuia
maamuzi ambayo wananchi wa Tanzania watakuwa
wamefanya
kupitia sanduku huru la kura kuhusu hatma ya uongozi wa
nchi
yao …?"
1. Napata
shida kuitafakari kauri hii,Je umetumia kigezo gani
kusema " ..watanzania watakuwa wamefanya
kupia
sanduku huru.." Je tayari una majibu ya jambo ambalo
hatujalifanya? Kama hivyo
ndivyo ni hatari sana kwa kuwa ni sawa na mtu anayeingia
uwanjani akiwa na
matokeo mkononi.Nini kitatokea ikiwa
atashindwa?
2. Ikiwa
na wengine watakuwa na mawazo kama yako,huoni kama ni
hatari
kwa kuwa hamtakuwa
tayari kupokea matokeo kwa kuwa tu mnaamini kuwa
"mtaibiwa
kura" na ccm hata
kama haitakuwa hivyo?
Nitashukuru ikiwa
maswali haya yatapatiwa majibu.
Asante
______________________________
Without
"Ethical Culture" there is No Salvation for
Humanity
______________________________
A D D R E S
S
John J.
Malata
Tutor.
Vikindu TC
P.O Box
16268
DAR ES
SALAAM
TANZANIA
Mobile:
+255 782366090
Blog:http://pengotz.blogspot.com/
On Friday, September
18, 2015 10:54 PM, 'Leonard Elias' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Kaz nzuri sana mama
Inkya
Nadhan mkapa anaigiwa na hofu na ccm
ikianguka igakuaje kuhusu yy na mali zake ndo maana ana
weweseka
Sent from my
iPhone
> On Sep 18,
2015, at 19:26, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
> CCM
WANAJIDANGANYA
>
>
Na Ananilea Nkya
>
>
Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wanapaswa
wasijidanganye kwamba kwa kumteua Dr John Magufuli kuwa
mgombea wa Urais chama hicho kimekuwa kisafi na na
hivyo
kinaweza kuwatumikia wananchi na kuondoa umaskini
unaoumiza
mamilioni ya wananchi nchini hivi sasa.
>
> Hakuna chama chochote cha siasa
duniani kimeweza kujisafisha kikiwa madarakani.
>
> Zaidi siyo dhambi
wala aibu kwa chama cha siasa kushindwa uchaguzi. Ni
jambo
la kawaida na ni heshima pia kama chama cha siasa
kinakubali
kushindwa uchaguzi ikiwa imetokea hivyo.
>
> Chama cha siasa
kinaposhindwa uchaguzi na kukubali kushindwa kinastahili
kupongezwa na kuheshimiwa.
>
> Hivyo hakuna mamtiki yoyote kwa CCM
kutumia propaganda kwamba kwa mgombea wake wa Urais
kupata watu kwenye mikutano ya kampeni basi tayari
kimeshinda kwa asilimia 69.3. Huku ni kujidanganya na
kudanganya umma.
>
>
Kama umati wa watu ndicho kigezo cha ushindi wa
CCM takwimu hizi zinapingana na hiki kigezo kwa
sababu viko vyama vingine pia ambavyo vimekuwa vikipata
umati mkubwa wa watu kwenye mikutano—tena wanaokwenda
kwa
hiari na gharama zao.
>
> Je vyama hivi na vyenyewe vikifanya
propaganda na kutangaza kwamba kutokana na wingi wa watu
wanaohudhuria mikutano yao vinaweza kushinda kwa
asilimia
80 nchi itakuwa imewekwa katika hatari kiasi gani
baada
ya uchaguzi ?
>
>
CCM na serikali yake inapaswa kutambua kuwa siasa
za
ushindani katika nchi zikiendeshwa vema bila chama
chochote kuendesha propaganda kwa lengo la kubaki
madarakani
hata wakati kimekataliwa na umma ni kuvuruga amani
na
kuongeza umaskini katika nchi.
>
> Imetokea katika nchi kadhaa duniani
vyama vilivyotawala muda mrefu vimeondoka madarakani na
nchi hizo zikabaki salama na kupiga hatua kubwa ya
kimaendeleo.
>
>
Mfano nchi jirani za Kenya na Zambia vyama vikongwe
vimeshindwa na vyama vingine vimepewa ridhaa na
wananchi
wan chi hizo na vimeendesha nchi bila matatizo yoyote na
maisha ya wananchi yanasonga mbele.
>
> Vyama vingi vinawezesha chama kinachopewa
ridhaa kikishindwa kutekeleza ahadi zake kupunzishwa
kwa
muda ili kujipanga upya nan a kwa kufanya hivyo
kinalazimika kuacha jeuri dhidi ya wananchi, uzembe ,
ufisadi na rushwa.
> Chama cha siasa
kikishapunzishwa kwa muda na kujisafisha, hulazimika
kubuni sera nzuri za maendeleo na mikakati ya
kuzitekeleza na chaguzi zinazofuata kikiomba tena ridhaa
kwa wananchi na kinakubaliwa.
>
> Hapa ndipo mfumo wa vyama vingi unakuwa na
manufaa kwa nchi husika. Kuondoa umaskini miongoni
mwa
wengi na kuiletea nchi maendeleo.
>
> Vinginevyo rasilimali za nchi zinabaki
kunufaisha watawala wachache na wawekezaji wa nje katika
zama hizi za utandawazi wizi, soko holela na
utandawaziwizi
wa zama za ukoloni mpya kibepari duniani
unaofukarisha mafukara mamilioni ya wananchi.
>
> Wanaoitetea CCM
ibaki madarakani wanapaswa kujiuliza : Ni kwa nini
CCM
ing'ang'anie madaraka na isipewe muda wa
kupunzika, kujitafakari, kujisafisha na kupata nguvu na
maono na sera ya mapya za kuongoza nchi yetu ili
Tanzania ipae kimaendeleo?
>
> Ni kwa nini nchi yetu iendelee kuongozwa
na CCM ilichochoka kiasi kwamba sera zake kila uchao
zinazaa mamilioni ya wananchi maskini wa kutisha
wakiwepo
wanachama wengi wa CCM na huku viongozi wakiwa
matajiri
wa kutishwa kutokana na ufisadi, rushwa, uzembe, uvivu na
watawala kutafuna fedha za wananchi kwenye miradi ya
umma na kujipangia safari za nje ya nchi tena kwa
kupanda
ndege daraja la kwanza kwenda kuomba misaaada kama
neti
za mbu au kuchukua digrii ya heshima?
>
> Hebu fikiria kwa mfano Mwenyekiti
mwenza wa UKAWA, James Mbatia ameweka bayana kwamba
Rais Jakaya Kikwete katika kipindi ccha utawala wake
amesafiri nje ya nchi mara 409 na safari hizo
ziligharimu shilingi trilioni 4.5.
>
> Maana yake angalao kila mwaka Rais
alisafiri nje ya nchi mara 40 akipoteza siyo tu fedha
alizotumia kwa safari hizo bali pia muda mwingi wa
kuwatumikia Watanzania.
>
> Mbatia alisema safari hizo za nje
zingepunguzwa kwa asilimia 80 zingepatikana fedha
ambazo zingetosha kujenga vyuo vikuu 80 nchini
kila
chuo kikigharimu shilingi bilioni 50.
>
> Aidha fedha hizo zingeweza
kujenga vyuo vya ufundi 200 nchi nzima kila chuo
kikigharimu bilioni 20. Kadhalika fedha hizi zineweza
kujenga hospitali 100 na kila hospitali ikigharimu
bilioni 30.
>
> Je
kwa hali hii kuna Mtanzania hata awe mwana CCM
mwenye
akili timamu na anayeipenda Tanzania kwa dhati kabisa
na anayeweka mbele maendeleo ya nchi yetu na
mamilioni ya watu wake ambaye atatelea CCM
iendelee
kuongoza nchi yetu miaka mingine mitano kuanzia tarehe 25
Oktoba mwaka huu 2015?
>
> Ni mwanaCCM wa aina gani asiye na
huruma na mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa
umaskini ambaye atataka CCM iendelee kuwa madarakani
huku watawala wakijinufaisha kwa kusafiri nje ya nchi
kwa fedha ambazo zingeweza kutoa elimu bora hadi
chuo
kikuu, huduma bora za afya maji safi na salama au kujenga
barabara au viwanda vya kutoa ajira ?
>
> Mbona hata CCM wenyewe wanajua kuwa
sera za chama chao hakiuziki katika uchaguzi wa
mwaka
huu na ndiyo sababu badala ya kuuza chama na sera zake
wanauza mgombea wao wa urais Dr John Magufuli?
>
> Hata hivyo
wananchi wanafahamu kuwa makubaliano ya uongozi wa
nchi
ni kati ya chama/vyama vinavyoomba uongozi wa nchi
na
wananchi na siyo kati ya mgombea Urais wa chama fulani
na wananchi.
>
> Hii
ina maana kuwa mwisho mwa siku ni chama/vyama husika
vinavyoomba ridhaa ya kuongoza nchi ndivyo
vitawajibika
kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Ahadi
zisipotekelezaka
uchaguzi unaofuata wananchi wanachukua maamuzi sahihi
kupitia sanduku huru la kura.
>
> CCM isijidanganye kuwa Dr Magufuli
ndiye CCM maana CCM ni taasisi ni chama cha siasa na kwa
taratibu za uchaguzi makubaliano ya kuongoza nchi
hufanyika baina ya vyama vya siasa na wananchi na siyo
baina ya mgombea Urais na wananchi.
>
> Makubaliano ya kuongoza nchi
yanakuwa ni kati ya vyama vya siasa na wananchi kwa
sababu
mgombea kama binadamau anaweza kuondoka katika
chama
kwa sababu mbali mbali lakini chama cha siasa kama taasisi
kinabaki, hakiondoki na hivyo kitakuwa kitadaiwa
utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.
>
> Hebu fikiria kama
vyama vinavyounda UKAWA vingekuwa vimeingia
makubaliano na mtu mmoja mmoja mfano CUF
(Prof
Ibrahim Lipumba) au CHADEMA (Dr Wilbroad Slaa). Je
leo
hii UKAWA ingekuwa ipo na kuendelea kufanya kazi nzuri
ya kisiasa kwa maendeleo ya nchi yetu kama ambavyo
imekuwa ikifanya hadi sasa?
>
> Kwa hiyo ni vema wanaCCM na viongozi
wa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu 2015 wakaanza
kujiandaa kisaikolojia kwamba CCM inaweza ikashindwa au
ikashinda kwenye uchaguzi badala ya kufanya
propaganda
zinazoashiria kuwa hakiko tayari kuondoka madarakani
hata
kama kitakuwa kimekataliwa na wananchi kwenye sanduku huru
la kura.
>
> Aidha
ni muhimu hasa viongozi waandamini ndani ya CCM na
serikali
yake kutambua kuwa katika siasa za vyama vingi
maendeleo ya nchi yanapatikana kwa haraka zaidi na
umaskini miongoni mwa wananchi walio wengi unapungua kwa
kasi endapo uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
>
> Kadhalika watambue
kuwa ni kawaida na ni afya kwa nchi kama chama
kilichokaa
madarakani muda mrefu kikishindwa kukubali kushindwa
bila kulazimisha ushindi kwa goli la mkono.
>
> Vile vile watambue
kuwa kitendo chochote cha CCM na watawala wa
serikali
ya CCM kuzuia chama kingine cha siasa kisiongoze
nchi yetu katika kipindi cha miaka mitano ijayo, hata
pale wananchi watakapokuwa wameamua hivyo ni sawa na
kukwamisha maendeleo ya Tanzania na kutaka
mamilioni ya
Watanzania wanaoishi kwa umaskini waendelee na umaskini
wao kwa miaka mingine mitano.
>
> Hiyo haitakubalika. Itakuwa ni sawa na
kuanzisha vurugu zenye lengo la kuitumbukiza nchi yetu
katika vitendo vya kusababisha kuvunjika kwa amani.
> Ni pale tu demokrasia ya vyama vingi
inapofanya kazi bila hila kwa Tume ya Uchaguzi kufanya
kazi
kikamilifu, ubunifu bila upendeleo, chama kilichopo
madarakani kuacha kuendesha kampeni kwa kutumia lugha
za
vitisho, dharau kwa vyama vingine, giliba, rushwa,
uchakachuaji na ubabe ndipo wananchi na nchi
inaponufaika na mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa
kutokomeza umaskini.
>
> Mwaka 2011, Rais Kikwete aliwahi
kuulizwa na mwanahabari mmoja kutoka nje ya Tanzania
kuwa ni kwa nini Tanzania ni maskini ili hali ina
rasilimali nyingi za asili zinawezeza kutumika kutajirisha
Watanzania wote na alimjibu kuwa hajui.
>
> Hata hivyo, Rais
Kikwete anapaswa kutambua kuwa moja ya sababu
zinazochangia
umaskini kuitafuna Tanzania ni CCM kutokukubali
kwa dhati mfumo wa vyama vingi vya siasa
ufanye
kazi inavyotakiwaili hali chama hicho kimeshaacha
falsafa ya Ujamaa iliyoendana na mfumo wa chama kimoja
nabadala yake imebeda falsafa ya ubepari inayoendeana na
mfumo wa vyama vingi.
>
> Kuthibitisha kuwa CCM bado haijakubali
mfumo wa vyama vingi ufanye kazi, Rais mstaafu
Benjamini Mkapa akipiga Kampeni kule Bukoba
katika
uchaguzi wa mwaka huu 2015 alikaririwa na baadhi ya vyombo
vya habari akisema kuwa vyama vya upinzani havistahili
kupewa dhamana ya kuongoza mpaka vifikishe umri wa
miaka 50.
>
>
Wananchi wanajiuliza ni kwa nini CCM isubiri hadi
vyama
vya upinzani vizeeke ndipo vipewa ridhaa ya kuongoza
nchi?
>
> Hii
kauli ya Mkapa inatukumbusha Watanzania zama za ASP na
TANU vilipokuwa vinapigania uhuru kutoka kwa wakoloni
mbapo mwishoni mwa miaka ya 50 ambapo wakoloni kama
anavyofanya Mkapa walikuwa wanadai kuwa ASP na TANU
vilikuwa bado ni vyama vichanga hivyo havikustahili
kupewa ridhaa ya kuongoza Tanzania (Zanzibar na
Tanganyika).
>
>
Lengo la wakoloni lilikuwa ni kuchelewesha uhuru.
Hata
hivyo TANU NA ASP vilikaza buti na viliwapuuza
wakoloni na uhuru wa nchi yetu ulipatikana bila
kuchelewa
kama walivyotaka wakoloni.
>
> Hivyo watawala wa CCM wanaotaka CCM
iendelee kuongoza nchi wanapaswa kujiuliza ni kwa
nini
Watanzania wakubali kuacha mali za nchi yao zikiwa
zinatajirisha watawala wachache na wawekezaji
kutoka
nje ya nchi ili hali mamilioni ya Watanzania wakiwepo
wanachama wa CCM wengi wakiendelea kubaki maskini na
mafukara?
>
> Ni kwa
nini CCM isipumzishwe kwa miaka mitano kiweze kujitafakari
na kujipanga upya kama kweli kimekubali mfumo wa vyama
vingi
kwa dhati kabisa na kwa kutambua kuwa siasa za vyama
vingi
zikiendeshwa kwa uhuru ndipo nchi yetu itaweza
kukomesha
uzalishaji wa mafuriko ya wananchi maskini katika nchi
yetu
ili hali nchi yetu ni tajiri wa mali asili—madini, gesi,
maji, misitu an ardhi yenye rutuba?
>
> Nadhani Rais mstaafu Mkapa alitoa
kauli hiyo au kwa vile hajatafakari vema manufaa ya siasa
za
vyama vingi na umuhimu CCM kukubali kushindwa uchaguzi
kwa uhuru na haki kwa kusikiliza na kuheshimu maamuzi ya
umma .
>
>
Vinginevyo alitoa kauli hiyo kwa sababu hajaishi
maisha
wanayoishi Watanzania walio wengi ambao wanateseka kwa
umaskini.
>
> Hata
hivyo ni vema Rais mstaafu Benjamin Mkapa akatambua kuwa
wajibu wake kama Rais mstaafu kwa taifa hii kwa sasa
siyo kulinda maslahi ya watawala wachache wa CCM
ambao
wanadhani kwa CCM kuondoka madaraka Tanzania
itaharibikiwa.
>
>
Mkapa pia anapaswa kuwaonya baadhi ya viongozi wa CCM
wanaopanda majukwaani na kuweweseka kwa kusema kuwa
CCM kamwe haiwezi kuviachia vyama vya upinzani
kuongoza
nchi.
>
>
Wanaoweweseka na kusema CCM haiwezi kuviachia vyama
vya upinzani kuongoza nchi wanathibitisha kuwa
serikali
ya CCM inaendesha mfumo wa vyama vingi kama geresha
lakini watawala wa serikali ya CCM hawako tayari kuona
CCM
inaondoka madarakani kwa amani hata kama wananchi
watakuwa
wameamua hivyo kupitia sanduku huru la kura. Hii
haikubaliki.
>
>
Ndiyo sababu baadhi ya wananchi wanajiuliza: Je CCM
na serikali ya CCM yake mwaka huu 2015 watatumia
kwa
'goli la mkono' kuzuia maamuzi ambayo wananchi wa
Tanzania watakuwa wamefanya kupitia sanduku huru la
kura
kuhusu hatma ya uongozi wa nchi yao ?
>
> Kama serikali ya CCM watafanya
hivyo, watakuwa wamejidanganya na kudanganya Watanzania na
ulimwengu kuwa Tanzania nchi nchi ya vyama vingi vya
siasa.
>
> Badala
yake Tanzania itakuwa inaendelea kuwa nchi ya chama kimoja
cha siasa maana vyama vingi vya siasa havitaweza
kuendeshwa kwa uhuru na ufanisi unaopaswa bila kuwekwa
misingi ya kuondoa umaskini nchini --misingi ambayo
itawekwa na Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi
haitaandikwa.
>
>
Lakini zaidi CCM na serikali yake watakuwa
wamejidanganya
kwa sababu watakuwa wamefanya maamuzi mabaya ya kutaka
kuendelea kutengeneza bomu la mamilioni ya Watanzania
maskini na kikundi kidogo cha watawala matajiri wa kutisha
hali ambayo itahatarisha zaidi amani na utulivu wa
Tanzania tuendako.
>
> Tukifika hapo wawekezaji wa kigeni na
wafadhili (wakoloni wa zama hizi mpya za utandawazi wizi
)
watachekelea sana maana watakuwa wamepata mwanya mpya
wa
kuibia zaidi Tanzania . Mungu ibariki Tanzania tusifike
huko
>
> Note:
Naruhusu anayetaka kuchapisha Makala hii afanye hivyo.
Lengo tuelemishane kwa manufaa ya nchi yetu na wananchi
wote.
>
> Ananilea
Nkya
> E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email
kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the
sole responsibility for any legal consequences of his or
her
postings, and hence statements and facts must be presented
responsibly. Your continued membership signifies that you
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are
subscribed to the Google Groups "Wanabidii"
group.
> To unsubscribe from this group
and stop receiving emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
>
<CCM WANAJIDANGANYA.docx>
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment