Thursday, 10 September 2015

Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU

Mimi ninaona kwa maoni yangu:
i) Sio kila oni la wananchi likubaliwe na serikali iliyo madarakani. wananchi wengine husema bila ya kuwa na ufahamu mzuri au kwa jazba bila ya kuangalia causes and effectsrelatioship. Na ni hivyo hata mzazi huwezi kumkubalia mwanao kila atakacho kwa sababu za msingi au mke/mume kusikiliza na kufuatia kila uambiwalo na ndugu kuhu mwenzako. Mfano hasa mawifi na wakwe au ndugu upande wa mume hutaka kumuamulia kaka yao na kumtawala wifi. Kicha cha familia lazima apime na kuchukua uamuzi wa busara. Hivyo maoni au kila proposal sio lazima ikubalike kama ilivyoletwa. Mfano maoni yanaweza kuwa-kutenganisha ZNZ na Tanzania bara kwamba kuna uonevu kuwe na serikali 3. Zanzibar huru iwepo. Gharama za administration, pili unaangalia -aina ya uonevu wakati wao wamejaa huku kila kona na biashara kibao, wamenunua nyumba kila kona na sasa wanalima hadi kilombero. Wanaonewa kivipi na hata bili ya umeme wa tanesco hawalipo. Kisha ndugu wa asili ya koo zao kibao bara. WEWE
mbara ukienda kule kuanzisha biashara-Tindikali! Unapima na historia na matokeo yake mazuri na mabaya kama tukijitenga na usalama wa nchi pia.

ii) Baadhi watasema mbuga za hifadhi ziondolewe wapewe walime, wafuge wanaonewa-utaangalia historia ya mbuga na mafao yake katika mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa nchi, maji na wanyamapori. Bila ya catchment protected forests na mbuga hizo-jangwa kama somalia. Mbona wazee wetu waliweka mila na desturi zilizolinda na miiko ilikuwa mikali kukata miti au mgeni toka kwingine kujiingilia tu. wageni walikaribishwa kwa sheria ya chief hapo sasa sisi tuna sheria kisekta na tunazivunja. tutakataa tutaluwa na alternative nyingine ya conservation with benefit sharing na hii ipo na bado hata viongozi wa mila mafisadi, wavijiji pia na bado vijana wao wanaingia kuwinda na kukata miti kiharam na wizi wa mazao shambani na wa mifugo vita waishipo walalamikao.

iii)Kama ni kufaidika na raslimali sera zipo kabisa na hata Public Private Partnership na Act yake NIC. Mbongo afaidike na raslimali awekeze lakini mbongo huyo akipewa estate farms-halimi anakodisha wananchi, anunue mazao badala ya serikali-anatia mawe, mchanga katika pamba, anawafundisha wauzaji kahawa uchafuzi na kulipa hela kidogo kwa kilo-apate afaidike yeye. Kama ni mkandarasi-anachakachua jengo hata liwe darasa wasomako watoto wake, barabara usiseme bora umpe mchina au kampuni ya kigeni. Umfanye nini mbongo? kwa kujimaliza mwenyewe na kuonea wazawa wenzake yupo kiwango cha juu. Waliopewa maendeo ya viwanda na viwanda-wameweka frame wanapangisha mikopo waliyopata wamejenga international schools au majumba wanapangisha kwa dola. Halafu-tunaonewa raslimali zetu kushikwa na wageni. hata huyo mgeni anapata tabu na rushwa kupata vibali vya kuanzisha investment. Kisha-tunaingia ubia nae na kumfundisha jinsi ya kuuibia serikali yetu wenyewe na ubia huo
tunaandika majina ya watoto wetu. Kisha-raslimali hazitufaidishi.

iv) Kama si kuweka ardhi chini ya Rais-kweli mashamba mengi na ardhi ya umma ingeuzwa sana. Asilimia 93 ya watanzania ni wakulima wadogo wadogo kati ya hawa 78% ya ardhi wanayomiliki haijapimwa hawana hati. Na ule uhuru wa kuhamahama kwenda kukote ukajenga, fyeka misitu, lima, hamia na mifugo ungekuwepo kama si katioka kuruhusu na kumlinda mwananchi kwa ardhi sio kuwa chini ya mikono binafsi bali ya umma na serikali chini ya Rais? Kule ambako gender NGO walikofundisha sheria ya ardhi na kuelimisha haki za mwanamke ktk ardhi, kugawa sheria ya ardhi iliyorahisishwa kwa kiswahili, kuunda kamati za ardhi na paralegals wa kusaidia mashitaka kwa msaada wa donor fund-ndio huko migogoro ya ardhi imepamba moto licha ya mafunzo na kuwepo kamati hizo. Cheza na mbongo wewe ubinafsi umemjaa na mtazamo finyu wa maendeleo yake mwenyewe. Mradi ukiishakabidhiwa-wanarudi kule walikotoka.
Unakuja mwingine ni hivyo-reinventing the wheel kila wakati. Utaanza na HIMA, utakuja na ASDP, DADPS na Village participatory Land use Planning na kufundisha sheria ya ardhi na kuunda kamati vijijini, utakuja na SUDPF mijini na mafunzo kama hayo na support kwa wajasiriamali, utakuja na WMA, TASAF support kwa kaya masikini na mbuzi wa maziwa wa kutoa lita 3 kwa siku chini ya msaada wa CONCERN wakiongezea kwa hizo kaya na vikundi vya ujasiriamali vya mbuzi utakuta vimekufa haoni haja ya kupanda yale majali ya mbuzi walizopewa mbuzi zinaachiwa kula mashamba ya shule na jirani. Kila mradi ukiiasha unaanza upya. Umasikini utaondokaje hatujitumi? hatuoni mbali. Donors tumewakuta wamegawana Mikoa in 1980s mpaka leo tupo pale pale!!

v) Masikini mwenye hasira-yupe anayefungulia choo kinamwaga barabarani anashindwa kupita kwa raha mwenyewe, anayeuza nyumba ya NHC ya 60,000/= 1974 kariakoo, magomeni kisha anahamia kinyesini jangwani. anapewa mabati, kiwanya chenye hati, simeti-anauza anarudi jangwani. anamuuzia mpemba Ilala anahamia kinyesini bwawa la vingunguti. anauza Mburahati nyuma hiyo anahamia bwawa la kinyesi ya kiwanda cha urafiki na municipaliti la mburahati. Kinyesi kimezunguka anatesa watoto haoni. kauza kariakoo kajumba na plot yake kwa milioni 400!? ana akili huyo? Umasikini haujui, hauoni? Kwa nini anafanya matendo ya pumba tupu. kaangalie maeneo yaliyopimwa kwa mkopo wa world bank DSM uone mji ulivyokuwa makorokoro n mihela hatujalipa. ona wanavyobomoa visima vya pampu vijijini kuuza chuma chakavu au kufungia mkokoteni wa ng'ombe. kisha wanawake kutembea kutwa kilometa 5 kufuata maji machafu yanayotia maradhi. Ona vyandarua walivyopewa bure wanavyobebea chupa waokotazo
wanafunga marobota. eti wakilalia itakufa hawatozaana Obama kaweka dawa dudu itakufa!? Halafu hawaendi kumeza prazquantel na dawa ntingine zinazotolewa bure kuua minyoo, ngirimaji, trachoma, usubi?! masikini hao ambao wataandamana. hao ambapo pakiungua moto ukizimwa-wanaziba upya kuliko kwanza kama vile hatari iliyopita ikaua, ikaharibu mali hawakuiona ubaya wake-Pumba tupu!!

vi) Ukitaka kuziona pumba zetu waTZ fika machimboni uone wanavyoharibu mito, misitu ya vyanzo vya maji na kuchezea mercury. Ona majumba ya zinaa, video za matusi, bar wanakomaliza hela wapatazo ni madeni tu kwa madalali wao. Pia wanaoana bila kupima ukimwi na mabango kibao. Sex bila condon na abnormal sex ndio bei ghali zaidi-Akili hiyo? kati ya 100 sita tu ukihoji ndio watakuambia wamefanya cha maana. wakimaliza kuharibu hapo wanahamia kwingine na kusambaza ukimwi na wanaoumwa wanasema wamelogwa. Mercury inatuletea kizazi cha vilema. Sema usikie wanadharau. sasa wamegundua madini Dodoma kitone ya gold unakipata baada ya kazi ngumu ya siku 2-wanamiminika kuhamia huko. wanataka kuchimba mashamba ya watu-customary land wenyewe owners wanakataa. wanalalamika kupitia TV-wanaonewa na wamiliki ardhi. Wingi wa watu, wizi, zinaa utoro shule-tayari. Jiulize-majumba ya kihistoria yapo Kilwa, bagamoyo, Mafia, tanga, Mtwara yanabomoka-matajiri wa TZ wapo wapi?
Maembe, nyanya zinaoza vijijini wapo wapi? raslimali zetu hazifaidishi watanzania-Kipima joto kitakupa 90% hawafaidiki huku wanaharibu mazingira na kubomoa majumba kuuza mawe. Wameuza Makongo, salasala, Bunju etca mashamba ardhi kubwa-wapo wamejenga mashimoni na barabarani. Njia ya bagamoyo wameondoa mawe ya Magufuli yanaoonyesha mpaka wa barabara-Tunaonewa. Hakuna nchi isiyotumia sheria kurekebisha maendeleo ya raia wake isipokuwa TZ kwenye kubweteka, uhuru wa kuharibu bila kuadhibiwa.

Sishawishiki kama atakuja kiongozi ambaye hatokuwa mkali wa kuwapelekesha watanzania tubadilike kiakili kukubali kuzingatia mikakati na misingi ya maisha ya maendeleo kama tutapata maendeleo hasa. Hata kama tubadili katiba jinsi gani. Suala si ubaya wa katika iliyopitishwa ni utendaji kisekta wetu wote. Sidhani kama kila lisemwalo lipite bila kuliangangalia mradi eti wananchi wametaka hivyo.

Tatizo ni kule kubweteka kwetu na kutaka vishuke kama mvua, externalization of errors sio internalization kwamba nasi tunahusika tubadilike, Fisadi tunamtolea dhamana kama tumtoleavyo mbakaji aliyekamatwa live. Mijibaba kifua kipana wenye nguvu ni madalali kila kona. Kinyesi kinafurika tupo tunakula hapo hatuoni tofauti-tutaona tofauti. Utabadilishwa vipi kimaendeleo kama hujitumi pale ulipo. Kila mtu aajiriwe itawezekana kweli? wazungu hawana tena haja ya kutumia kodi yao kutugharimia sisi. Andikeni katiba kumfurahishwa mwananchi kila asemalo lakini tujue mtanzania-tumebweteka politics of the belly and of the underwear zimezidi kutuharibu kutetea upuuzi kama sio ujinga. kutokuwajibika kiutendaji sijui tutafanyaje-kwa kufukuza watu daily na kuchagua wale wa kuchaguliwa kabla ya miaka 5-hafanyikazi mbunge mwaka mzima hakionekani kitu-out!! anyway-ni fielsworker sielewi siasa.

--------------------------------------------
On Thu, 10/9/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 10 September, 2015, 16:08

Amour maswali yako yana msingi.
Lakini Ilani ya  Chadema inaonyesha kuwa wataandika
Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Hiyo itajenga
msingi mzuri  wa kumdhibiti Rais. Kama unakumbuka
yaliyokuwa kwenye Rasimu ya Katiba  ya wananchi ni
pamoja na kumpunguzia Rais madaraka kw akiwango
kikubwa.   Hivyo hakuna sababu ya kuwa na
shaka maana  kinachoitesa CCM sasa  ni kosa
lililofanywa na Rais Kikwete, la kutotumia fursa  ya
kipekee aliyoipata-- kutoa uongozi wa kijasiri kuandika
Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.

Hivyo CCM wanachoogopa ni kwamba UKAWA  wakiingia
madarakani, pengine hawataandika hiyo Katiba Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi na hivyo
watajinufaisha  kwa fedha na rasilimali za nchi kama
walivyokuwa wanafanya wao CCM.

Hata hivyo, hakuna jinsi ambavyo CHADEMA/UKAWA
watakwepa  jukumu la kuandika Katiba Mpya 
inayotokana na maoni ya wananchi kwa sababu mamilioni
ya  wananchi wanaosumbuliwa na umaskini hawatakubali,
watawasha moto mkali. Kumbuka mamilioni ya wananchi masikini
hivi  sasa wana hasira na maskini wao ili hali watawala
wachache na wawekezaji  wakiwa wametajirika  kwa
rasilimali za  Tanzania.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 9/10/15, amour chamani <abachamani@gmail.com>
wrote:

Subject: Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Date: Thursday, September 10, 2015, 11:16 AM

Dada Nkya


Kwangu shida sio mabadiliko. Shida yangu nahisi
hao tunaotaka kuwapa dhima hiyo ni tatizo zaidi.

Lowasa anasemaje kwa mfano kuhusu Nyumba za serikali?

Naona hats CHADEMA hili halikuwa tatizo mpaka alipokuja
Prof. Safari.

Lakini kwa namna yoyote ile CCM hats wakishindwa watakuwa
na
wabunge wengi kwa maana watakuwa na waziri Mkuu.

Hiyo serikali itafanya kazi zaidi ya kukomoana?

Lakini hawa watu wamegeuza wimbo wao kwa sababu ya ujio Wa
Lowasa tuna hakika gani kwamba hawatabadilika wakifika
Ikulu?

Lowasa amewatesa CCM kiasi hiki he CDM wanaweza
kumdhibiti?

Lakini je tunawasemea wanyonge au nasi tunaangalia baadae
yetu?



Walewale
On Sep 10, 2015 12:23 PM,
"'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
UCHAGUZI
2015:  NI KURA YA MAAMUZI KUHUSU UMASKINI WA WANANCHI

Na Ananilea Nkya

Tanzania  ni  moja  ya nchi  chache barani Afrika
ambazo
zimejaliwa utajiri  mkubwa wa mali asili yakiwepo 
madini,
ardhi yenye rutuba iliyosheeni milima mabonde  na
wanyama 
lakini  mamilioni ya wananchi ni masikini  wa kutisha
ingawa  nchi  ilipata uhuru  zaidi ya miaka  50
iliyopita.



Ili nchi iweze kuondokana na umasikini hata kama inazo
rasilimali nyingi   inapaswa kuwa na rasilimali nyingine
muhimu—rasilimali uongozi –uongozi unaohakikisha
kuwa 
mali za nchi  zinanufaisha  wananchi wote na siyo
kikundi  kidogo cha viongozi.



Uongozi  wa  nchi kwa kawaida hupatikana kupitia vyama
vya
siasa. Hivyo  ni muhimu wanaotafuta  fursa ya uongozi 
katika uchaguzi  wa mwaka huu 2015, kutambua kuwa 
mamilioni ya Watanzania  hivi sasa ni maskini ili hali
kikundi kidogo cha viongozi  ni matajiri  sana.



Kibaya zaidi  mamilioni ya  Watanzania wanaotaabika kwa
umaskini  hivi sasa  wametambua kuwa   umaskini 
 wao
unatokana na  uongozi  unaotoa fursa  kwa  viongozi 
kuwa matajiri wa kupindukia  na  mamilioni ya wananchi 
kubaki maskini.



Mamimioni hayo ya wananchi  wanateseka kwa umaskini 
 mwaka huu  wanataka mabadiliko ya uongozi wa nchi yao.



Wanataka mabadiliko hayo baada ya kutambua kuwa  mfumo wa
utawala (Katiba)  uliotengenezwa na serikali ya CCM 
 ndio  unawezesha watawala wachache  kuwa  matajiri wa
kutupa kwa kulipana fedha   nyingi  za  umma na
kujigawia rasilimali za nchi kujitajirisha wao wenyewe.



Kwa mfano  wananchi wanajua kuwa watawala  walijiuzia
kwa  bei  chee  nyumba za umma  zilizojengwa kwa
mabilioni ya fedha za  kodi ya Watanzania  wanaoteseka
kwa
umaskini.

Kadhalika,  wananchi wanafahamu kuwa   viongozi  wa
serikali  walijigawina fedha za umma zilizoibiwa kwenye
akaunti ya  Tegeta escrow mwaka jana 2014.



Vilevile  wananchi  wanajua  kuwa  watawala  mfano
wabunge wanalipwa   mishahara mikubwa na kiinua mgongo
kikubwa katika muda wa miaka mitano tu huku watumishi
wengine wa umma  mfano walimu, wauguzi na madaktari
wakiwa  wanalipwa  mishahara midogo sana.



 Kwa sasa, mtu ambaye haijamuingia akilini kwamba
mamilioni
ya wananchi wamechoka na umaskini  ambao chanzo chake 
ni
uongozi  mbovu  katika nchi  yao—uongozi ambao 
 unatajirisha wachache na hivyo wanataka mabadiliko ya
uongozi wa nchi yao,  mtu huyo  atakuwa anajidanganya.



Jambo jema ni kuwa  hata  baadhi ya wagombea Urais  kwa
mfano mgombea wa  CCM,  Dr John  Magufuli na mgombea
wa 
CHADEMA, Edward Lowassa   kwa  niaba ya vyama
vinavyounda
UKAWA  wamekuwa wakizungumza wazi kwenye  mikutano yao 
ya kampeni   kwamba  wananchi wanataka mabadiliko ya
uongozi.



Tena wagombea  hawa wanatambua wazi kuwa  mabadiliko
watayaleta  hao Watanzania   wenyewe  wanaoteseka
kwa 
umaskini kwa kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe 25
Oktoba  mwaka huu 2015.

Kwa maneno mengine mamilioni ya wapiga kura maskini
wanajua
kuwa uchaguzi wa mwaka huu 2015 kura yao ni  kura  ya
maamuzi  juu ya maisha yao. Ni kura muhimu  ya KUAMUA 
 KUENDELEA KUWA MASKINI AU KUUKATAA UMASKINI.



Ni kura ya kuamua iwapo  wanataka watawala wachache 
wanaotengenezwa na   serikali ya CCM  waendelee kuwa
matajiri wa kutisha na mamilioni ya Watanzania waendelee
kuumizwa na umaskini ili hali nchi yetu ikiwa ni tajiri
mkubwa wa rasilimali za asili za kuwawezesha Watanzania
wote
kuwa matajiri na kuishi maisha ya furaha na yenye hadhi.



Wananchi wenyewe wanajua kuwa  mabadiliko  wanayoyataka
yanawezekana ingawa  kumekuwa na njama za kujaribu 
kupunguza nguvu ya umma inayodai mabadiliko kutumia baadhi
ya viongozi wa ngazi za juu kwenye vyama vya upinzani
vinavyounda UKAWA (CUF, CHADEMA, NCCR Mageuzi na
NLD)--vyama
vinavyoongoza wananchi katika kutafuta mabadiliko.



Wananchi  wameshuhudia baadhi ya viongozi wa upinzani 
wakiamua ghafla kuondoka kwanye uongozi  na kuungana na
watawala  ambao mfumo wa uongozi umewafanya kuwa matajiri
wa kutisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa
kutupa.



Lakini  pamoja na viongozi   hao  kuachia ngazi,
mamilioni ya wananchi hawajabadilika, hawajayumba, 
msimamo
wao uko pale pale na wanasonga  mbele  hadi waweze
kufanya  mabadiliko wanayoyataka.



Ni kwa nini wananchi wanataka mabadiliko ya uongozi wa
nchi
yao?

Wanataka nao  wawe matajiri  katika  kipindi cha miaka
mitano kama  ambavyo  wananchi wenyewe wameshuhudia 
wanaochaguliwa  kuwa viongozi  wakitajirika ghafla 
baada
ya kuchaguliwa  kuwa viongozi!



Wananchi   wamechoka kuwa mafukara katika nchi yao 
yenye
utajiri mwingi wa asili  lakini utajiri huo 
unatajirisha  makundi mawili tu-- watawala wachache  na
wawekezaji wa kigeni.



Tena baadhi ya mamilioni ya Watanzania  wanaotaka
mabadiliko wengi wao hawana vyama vya siasa
wanavyofungamana
navyo maana hata  fedha za kununua kadi ya chama cha
siasa
hawana.

Baadhi waliobahatika kuwa wanachama wa vyama vya siasa 
kikiwepo chama kinachotawala nchi kwa sasa CCM, lakini 
wengi wa  wanachama  hao ni mafukara wa kutupa pia
wanaohangaika kwa umaskini kama wananchi  wengine.



Kimsingi,  mamilioni  ya watu maskini (nguvu kubwa ya
umma) ambayo mfumo wa uongozi wa serikali ya CCM
umezalisha,
mabadiliko wanayoyataka ya uongozi hayaepukiki maana
hakuna
anayeweza kuizuia  nguvu ya umma inapoamua kuleta
mabadiliko.



Isitoshe, mamilioni ya wananchi   hawa maskini,   ni
kama bomu ambalo  serikali ya CCM  imelitengeneza kwa
kujua au kwa kutokujua  kwa miaka kadhaa  sasa  na 
hivi
sasa  linasubiri kulipuka lenyewe kwa  amani  kwenye
sanduku huru la kura  tarehe 25  Oktoba  2015.



Jambo la kuzingatia ni kwamba , atakayejaribu kuzuia  kwa
mkono bomu hilo lisilipuke kwa amani kwenye sanduku huru
la
kura---uwanja  wa wazi ambao  ndio pekee bomu hilo
linaweza  kulipuka bila kuleta madhara ya kuvuruga amani
ya
nchi,  mtu huyo  historia  ya taifa hili itamhukumu.
Mungu ibariki Tanzania.



NOTE: Naridhia anayetaka kuichapisha au kusambaza makala
hii
isomwe na Watanzania  wengi afanye hivyo.



Ananilea Nkya

 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment