Tuesday, 8 September 2015

RE: {Spam?} Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA

Samwel,

Najaribu kufikiri hatma ya Tanzania kama tutaendelea kuwa na viongozi wa aina ile ile, vyama vilivyojaa mambo yale yale, utawala wenye tabia zile zile.
Bila mabadiliko!!

Haya basi, mkisema mnaweka matumaini kwetu vijana napo kuna matatizo yake!! wengi tunarithi mfumo ule ule tilioukuta kuanzia makazini, maofisini n.k.. Kielimu napo tunajua ukweli wake, pamedorora. jangwa kabisaa. Hakuna elimu ya uhakika inayoweza kutengeneza taifa la kuaminiwa hapo baadae. na kama ipo ni 1 katika 100,000. Situkani walimu, ila angalia na walimu wanaopelekwa kufundisha mashuleni sasa hivi!! Fikiria haya, upeo wao, ari yao ya kazi, ni taaluma wanayoipenda au wanatafuta mshahara? Wameenda ualimu kwa kupenda au ni mfumo umewalazimisha kwenda? Jibu la maswali haya lina picha halisi ya matokeo ya elimu yetu miaka mingi ijayo itakuwa ya namna gani!!

Ikifika miaka flani mbele and then hiki kizazi kinachosoma ndio kikatakiwa kutoa marais, wabunge, mawaziri, maofisa, n.k. watakuwa na serikali ya namna gani?

Tupo karibuni kutolewa mfano na dunia kwa aibu na si mazuri kama hatutarekebisha kitu mapema. Wote tutakuwa tumekufa ila makaburi yetu yatatemewa mate na vilembwekeze, vining'ina n.k. kama hatutajiandaa. wakati huo watakuwa na akili tofauti mbele sana zaidi yetu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment