Saturday, 11 October 2014

[wanabidii] Radio Times FM yatozwa faini kwa maneno waliyotumia

Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema 'Times FM' imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha 'Hatua Tatu' kinachosikika saa 3 hadi 
saa 5 asubuhi na 'Mitikisiko ya Pwani', kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume na chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingewezwa kusikilizwa pia na watoto.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment