Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Dk. Abdirahman Duale Beyle amesema kuwa, balozi za Somalia nje ya nchi zimepunguzwa na kufikia 31 kote ulimwenguni.
Duale amesema kuwa, balozi hizo zimepungua tangu kulipofungwa balozi tisa za nchi hiyo barani Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na hata Ulaya. Ofisi hizo za uwakilishi wa kisiasa zilifungwa kwa muda kufuatia kuongezeka gharama za uendeshaji wake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia amesema kuwa serikali ya Mogadishu
imekwishachunguza sababu zilizopelekea kufungwa balozi hizo tisa na kubaini kwamba suala hilo halitaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Somalia na nchi husika zilikofungwa balozi hizo. Amesisitiza kwamba hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na matatizo ya kifedha na si kwa sababu nyenginezo.
Amezitaja nchi hizo kulikofungwa balozi za Somalia kuwa ni pamoja na Tanzania, Burundi, Syria, Ujerumani, Uingereza, Malaysia, Libya, Rwanda na Sudan Kusini.
Radio Tehran, Idhaa ya Kiswahili: Balozi tisa za Somalia zafungwa ikiwemo Tanzania
-- Duale amesema kuwa, balozi hizo zimepungua tangu kulipofungwa balozi tisa za nchi hiyo barani Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na hata Ulaya. Ofisi hizo za uwakilishi wa kisiasa zilifungwa kwa muda kufuatia kuongezeka gharama za uendeshaji wake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia amesema kuwa serikali ya Mogadishu
imekwishachunguza sababu zilizopelekea kufungwa balozi hizo tisa na kubaini kwamba suala hilo halitaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Somalia na nchi husika zilikofungwa balozi hizo. Amesisitiza kwamba hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na matatizo ya kifedha na si kwa sababu nyenginezo.
Amezitaja nchi hizo kulikofungwa balozi za Somalia kuwa ni pamoja na Tanzania, Burundi, Syria, Ujerumani, Uingereza, Malaysia, Libya, Rwanda na Sudan Kusini.
Radio Tehran, Idhaa ya Kiswahili: Balozi tisa za Somalia zafungwa ikiwemo Tanzania
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment