Tuesday 24 December 2013

[wanabidii] Zitto Z Kabwe - Anayesema naidhoofisha Chadema ni muongo na apuuzwe.

Japo sina mashaka na influence yake kisiasa na wala sina chuki binafsi naye na pia si mwanachama wa chama chochote, nakubaliana na wengi wanaosema Zitto anadhoofisha Chadema. Zitto ameendelea kutokuwa 'team player' kwa kufanya mambo yake anayojua mwenyewe as if ana chama chake kingine ndani ya Chadema na hiyo inanipa mashaka katika skills zake za kiuongozi. Wakati wanachama wanachoma moto bendera , kuchana kadi na kufanya mambo mengine machafu dhidi ya Chadema wakishinikiza arejeshewe vyeo vyake, Zitto kama mlengwa mkuu alikaa kimya, hakuwakemea- simply because alitaka 'wapinzani wake' ndani ya chama waone 'nguvu yake' ili 'wakome'. Wakati yeye analaumu siasa za kukomoana, yeye mwenyewe pia ni mfuasi wa siasa hizo. Mbona Dr. mkumbo yeye katulia? Kwa nini yeye atapetape. Believe me, Zitto is not fit for a leader. Leadership skills siyo 'influencing' peke yake, kuna nyingine nyingi zaidi.

Wakati kuna mapungufu mengi sana ua uongozi wa sasa wa Chadema ambayo yanahitaji kurekebishwa ndani ya Chama, Zitto angetumia mapungufu hayo kama advantage kwake walau kwa kuonyesha kuwa ni mwanachama mwema kwa kukaa kimya hadi sekeseke hili liishe. kutapatapa kwake kwenye social media na kwa wananchi huku wadau kadhaa wa CCM wakionekana kuratibu mikutano yake, kunazidi kumfanya si tu kumuonyesha kama mtu asiye na utashi wa kusoma alama za nyakati bali pia kama mtu ambaye 'amenunulika' hasa kwa watanzania wachache wenye critical thinking!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment