Thursday 26 December 2013

[wanabidii] WATANZANIA WALIOKO SUDANI KUSINI WAJIHIFADHI UBALOZI WA KENYA

Ndugu zangu ,

Nimepata taarifa za kushtua na kudhalilisha sana .

Gazeti moja linalotoka nchini kila siku limeandika eti waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa akiwasihi watanzania walioko sudani kusini ambayo iko kwenye mgogoro sasa hivi kwenda kwenye ubalozi za kenya kwa ajili ya kujihifadhi .

Maneno hayo yamepatikana kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha dakika 45 kinachoonyeshwa na ITV .

Waziri na wizara ya mambo ya nje itueleze nini kimeshindikana kwa nchi yetu kutokuwa na ubalozi huko sudani kusini na hata kutokuwa na sehemu salama kwa ajili ya watanzania wanaoishi na kufanya kazi huko haswa juba kwa kipindi chote hiki .

Tukumbuke John Garang alianzisha vita iliyosababisha sudani kusini kupata uhuru ulisoma Tanzania na kupata mafunzo hapa pamoja na wapiganaji wengine wengi wa SPLM kwa kipindi cha miaka 20 hivi , sasa iweje leo kusiwe na sehemu salama kwa ajili ya watanzania mpaka wakimbilie kwenye balozi za nchi jirani ?

Pia , Sudani kusini imeomba kujiunga na Jumuiya ya afrika mashariki , sasa itajiungaje wakati hata raia wa nchi mwanachama wenzao anashindwa kuwa salama ndani ya nchi hiyo hata ubalozi wetu haujulikani unafanya nini huko ?

Halafu , huyu waziri wa mambo ya nje ni mtaalamu wa masuala ya Usalama iweje aruhusu tu wananchi wake kwenda kujihifadhi kwenda balozi ya nchi jirani ambayo ni Pinzani kwenye masuala ya Kibiashara kwenye eneo hilo na ambayo imekuwa inalalamikiwa na wananchi wenyewe ?

Yaani wameshindwa hata kukodisha ndege kwenda kuchukuwa raia hawa na kuwarudisha nyumbani ?

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa nae ni mzigo , hatuwezi kuendelea na mizigo kama hii kama nchi haswa kwenye masuala ya kimataifa kama haya yanayogusa maslahi yetu moja kwa moja .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment