Thursday 5 December 2013

[wanabidii] Tafakari ya Wananchi wa Tanzania Bara kuhusu Rasimu ya Katiba

Zaidi ya theluthi moja (36%) ya Watanzania Bara wameshiriki katika Marekebisho ya Katiba kupitia mikutano ya jamii, SMS, mahojiano, barua na barua pepe. Idadi kubwa walishiriki kupitia mikutano ya jamii iliyoandaliwa na Tume ya Kurekebisha Katiba (CRC). Pia, karibu nusu ya Watanzania Bara wanaweza kuelezea Katiba ni nini.

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika utafiti  uitwao: Kurasimu Sheria Mama ya Nchi: Tafakari  ya Wananchi wa Tanzania Bara kuhusu Rasimu ya Katiba. Msingi wa utafiti huu mfupi ni taarifa kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wenye uwakilishi kitaifa, uliotumia simu ya mkononi, ngazi ya kaya katika Tanzania Bara.

Taarifa zinaonyesha viwango vya juu vya ufahamu wa Katiba na ushiriki katika mchakato wa mapitio. Pia, karibu watu saba 
kati ya kumi (67%) ya Watanzania Bara wanafahamu kuwa rasimu ya Katiba ilizinduliwa, ingawa chini ya robo (23%) walijua jinsi ya kupata nakala ya Rasimu ya Katiba.

Wananchi kwa kiasi kikubwa walikubaliana na rasimu katika yote haya. Karibu wote (91%) ya Watanzania Bara wanataka kuwa na uwezo wa kumwondoa Mbunge wao kwa kushindwa utendaji, hiki ni kielelezo cha wazi cha kutaka uwajibikaji; na ni hali iliyofanya kifungu hiki kupendwa zaidi katika rasimu. Maeneo mengine ndani ya rasimu yaliyopata uungwaji mkono mkubwa toka kwa wananchi ni:

  • Mgombea urais lazima awe na umri zaidi ya miaka 40 (84% wanakubaliana)
  • Mawaziri na Manaibu wao wachaguliwe na Rais na kupitishwa na Bunge (77% wanakubaliana)
  • Bunge lazima liundwe na wajumbe 75, wawili kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara, wawili kila mkoa wa Zanzibari (76% wanakubaliana)
  • Spika na Naibu Spika, wanapaswa wasiwe viongozi wa vyama vya siasa kwa miaka mitano kabla ya kugombea nafasi hii (72% wanakubaliana)
  • Mawaziri na Manaibu wao wanapaswa wasiwe madiwani, wabunge au wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (70% wanakubaliana)
  • Wabunge wanapaswa kuwa katika ofisi kwa miaka isiyozidi 15 (70% wanakubaliana)
  • Wagombea huru waweze kuwania nafasi ya Urais na Ubunge (67% wanakubaliana)
  • Kuwe na tume Huru ya Uchaguzi, iliyoteuliwa na Rais (65% wanakubaliana)

Sauti za Wananchi
 pia iliwauliza Watanzania Bara kama waliunga mkono rasimu ya katiba. Pamoja na kuwepo makubaliano ya jumla katika masuala muhimu, wengi wao wangepigia kura rasimu ya sasa.

Endelea kusoma: maoni ya wananchi Sauti za Wananchi Tanzania utawala (bofya hapa).

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment