Tuesday 3 December 2013

[wanabidii] Taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu CHADEMA, Dk Slaa mikoa ya Kigoma na Shinyanga

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma, kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.  

Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika majimbo ya mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani na viongozi pamoja na wanachama.

Siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment