Thursday 26 December 2013

[wanabidii] Re: WATANZANIA WALIOKO SUDANI KUSINI WAJIHIFADHI UBALOZI WA KENYA

Kuna kisa fulani kilinisikitisha .

Kuna mtanzania mmoja alikuwa anafanyakazi kwenye NGO moja huko Bor , sudani ya Kusini , basi ule mji ulivyovamiwa na mauji kuanza yule mtanzania aliingia kwenye mitandao kadhaa ya kijamii kwa ajili ya kuomba msaada , wakati wenzake wa kenya na uganda na mataifa mengine walichukuliwa na nchi zao , baada ya siku kadhaa ndio tunasikia taarifa ya waziri wa mambo ya nje , tena sio taarifa ila ni swali alilojibu kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV .

Sasa kwanini tunaendelea kulinda mawaziri kama Membe ambao hawajui dhamani ya watanzania ? dhamani inakuja pale wanapohitaji kura zetu tu ?

Tuseme hapana huyu ni mzigo na mpaka sasa hivi hajaweza kutoa taarifa yoyote kwa umma kuhusu watanzania huko sudani ya kusini .

Kiongozi ambaye anachindwa kupigania maslahi ya Tanzania kama nchi na watu wake nje ya mipaka ya nchi yetu tena hapo jirani tu hatufai na inaonyesha hata hana uhusiano mzuri na viongozi wenzake wa jumuiya au wa kikanda .


2013/12/27 Gabriel Bakilana <gbakilana@gmail.com>
 

Ndugu zangu..

Sudan Kusini ni nchi changa sana. Nchi zote changa zinahitaji kusaidiwa kwa namna mbalimbali..ikiwa ni pamoja na wataalamu na kupata bidhaa mbalimbali kupitia mahusiano ya kibiashara. Watanzania wengi walioko Sudan Kusini ni waajiriwa wa UN ama mashirika mengine ya kimataifa, na Wafanyabiashara. Mimi suala hili limenigusa moja kwa moja kwani nina ndugu na marafiki wanaofanya kazi huko, wakisaidia kujenga uwezo wa nchi hiyo kiusalama na kiuchumi. Mlitaka nani aende huko kusaidia kujenga hio nchi? Wao wenyewe? Hii Tanzania yetu kwani tunaijenga peke yetu¿ Mbona wenzetu wengine wako nchi za wenzetu wakisoma na kufanya kazi¿ Sudan Kusini kuna machafuko imekuwa nongwa? Mimi natarajia Serikali iwasaidie Watanzania wote popote walipo.. Ukiwa katika nchi yenye vita unadhani utajua huu ni Ubalozi wa Kenya ama wa Uturuki? Binafsi sina tatizo na Watanzania kuomba hifadhi Ubalozi wa nchi nyingine yoyote, cha msingi wawe salama. Labda niulize..hivi wangeambiwa waende kujihifadhi Ubalozi wa nchi nyingine (zaidi ya Kenya) ingekuwa sawa? Labda tatizo sio kushindwa kuwapa hifadhi Watanzania..tatizo ni Kenya. Nchi nyingine zimeona mbali na kuchangamkia fursa huko Sudan Kusini. Kama serikali yetu imeona muda bado, basi tuendelee kuikumbusha....cha msingi kuwe na namna ya kuwahudumia watu wetu walioko huko. Na laiti kama kuna wachache waliozamia huko kutafuta maisha (wakimbizi wa kiuchumi)..nani kasema kuwa hawana haki ya hifadhi? Suala la kusema ni nani kawaambia waende huko ama wamepelekwa na nani linanikera mno. Hamjui tu...

G>

On Dec 27, 2013 7:29 AM, "Mwanahamisi" <mishysingano@yahoo.com> wrote:
 

Kwa ufahamu wangu mdogo, Watu wengi wanaenda nje ya nchi kwa shughuli zao binafsi (bila kutumwa na serikali) zikiwemo kusoma, kutafuta rizki na kutii. Linapotokea janga kwenye hiyo nchi wajibu kwa kwanza wa kujihami ni wa mtu mwenyewe then serikali yake inawajibika kuwanusuru. Ni utaratibu sahihi na tumeona Mara nyingi nchi ziki evacuate raia wao na kutoa travel advice inapobidi! Na tumeona nchi ambazo hata raia mmoja tu akiwa matatizoni wanavyofanya jitihada za makusudi kuwasaidia. Ni hayo tu

Sent from my iPhone

On Dec 27, 2013, at 7:15 AM, Emmanuel Sulle <esulle46@gmail.com> wrote:

 

Mimi sifurahishwi na hii hali ya kudhani watanzania wanaoishi huko wanaweza kuwa wamedandia meli. Hii ni dhana potofu. Hata kama walidandia meli ni katika kutafuta maisha bora ambayo kimsingi hapa nyumbani yameshindikana. Kwahiyo, tusiwe wa kwanza kuwanyooshea mikono wenzetu. 

Ni wajibu wa serikali kuwalinda raia wake!


2013/12/27 Baruani Mshale <baruani.mshale@gmail.com>
 

Naunga mkono hoja ya Mobhare na nasisitizia maswali ya dada Hildegalda.


2013/12/26 Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
 

Yona una hoja lakini inabidi ujielimishe zaidi.

On Dec 26, 2013 1:26 PM, "Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com> wrote:
 

Ndugu zangu ,

Nimepata taarifa za kushtua na kudhalilisha sana .

Gazeti moja linalotoka nchini kila siku limeandika eti waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa akiwasihi watanzania walioko sudani kusini ambayo iko kwenye mgogoro sasa hivi kwenda kwenye ubalozi za kenya kwa ajili ya kujihifadhi .

Maneno hayo yamepatikana kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha dakika 45 kinachoonyeshwa na ITV .

Waziri na wizara ya mambo ya nje itueleze nini kimeshindikana kwa nchi yetu kutokuwa na ubalozi huko sudani kusini na hata kutokuwa na sehemu salama kwa ajili ya watanzania wanaoishi na kufanya kazi huko haswa juba kwa kipindi chote hiki .

Tukumbuke John Garang alianzisha vita iliyosababisha sudani kusini kupata uhuru ulisoma Tanzania na kupata mafunzo hapa pamoja na wapiganaji wengine wengi wa SPLM kwa kipindi cha miaka 20 hivi , sasa iweje leo kusiwe na sehemu salama kwa ajili ya watanzania mpaka wakimbilie kwenye balozi za nchi jirani ?

Pia , Sudani kusini imeomba kujiunga na Jumuiya ya afrika mashariki , sasa itajiungaje wakati hata raia wa nchi mwanachama wenzao anashindwa kuwa salama ndani ya nchi hiyo hata ubalozi wetu haujulikani unafanya nini huko ?

Halafu , huyu waziri wa mambo ya nje ni mtaalamu wa masuala ya Usalama iweje aruhusu tu wananchi wake kwenda kujihifadhi kwenda balozi ya nchi jirani ambayo ni Pinzani kwenye masuala ya Kibiashara kwenye eneo hilo na ambayo imekuwa inalalamikiwa na wananchi wenyewe ?

Yaani wameshindwa hata kukodisha ndege kwenda kuchukuwa raia hawa na kuwarudisha nyumbani ?

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa nae ni mzigo , hatuwezi kuendelea na mizigo kama hii kama nchi haswa kwenye masuala ya kimataifa kama haya yanayogusa maslahi yetu moja kwa moja .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya




--
Baruani Mshale
Doctoral Program
SNRE
University of Michigan


__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (10)
.

__,_._,___



--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment