Daktari,
Hebu basi nawe tusimulie mikasa ya Muhimbili. Ni tofauti na anavotueleza Gikaro hiyo hospitali nyengine? 2013/12/8 Augustine Rukoma <rukomapekee@gmail.com>
Niishie kusema pole nikipata mda wa kutosha nitaandika kuhusu hili
--
On 12/8/13, Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com> wrote:
> USHUHUDA
> WA KUTISHA KUTOKA HOSPITALINI YA SERIKALI!!!!!
>
> Siku
> za hivi karibuni niliwahi kumuuguza rafiki yangu wakati akitibiwa katika
> hospitali
> ya serikali. Nilichoshuhudia huko kinasikitisha na kustaajabisha sana.
> Kimenipelekea
> niamini kwamba hospitali za umma ni makaburi ya kuzikia roho za watanzania
> wasiokuwa na hatia.
>
> Huyu
> jamaa yangu alikuwa hospitalized kwa ajili ya tatizo la kutapika na
> kuharisha
> damu. Alifikishwa hospitalini hapo takribani saa 2:00 za asubuhi lakini
> kutokana na ugoigoi na kutokujali kwa madaktari, alikuja kuchukuliwa vipimo
> mnamo
> saa 11:00 jioni. Wakati vipimo vinasubiriwa daktari alianza kumtibu kwa
> kuhisi.
> Kwanza alibashiri kwamba huenda mgonjwa anaumwa homa ya matumbo (typhoid),
> hivyo
> alimtundikia drip yenye dawa ya taifoidi. Kuanzishwa kwa matibabu haya
> hakumpa mgonjwa
> afueni yoyote, badala yake maumivu yalizidi huku akiendelea kujisaidia
> mabonge
> ya damu iliyoganda.
>
> Daktari
> alipoona hali inazidi kuwa mbaya, ikabidi ambadilishie dawa. Safari hii
> alibashiri ugonjwa tofauti kabisa—vidonda vya tumbo. Akamuandikia dawa
> zingine
> tena—zile za taifoidi tukaachana nazo licha ya kwamba tulishatumia pesa
> nyingi kuzinunua.
> Hata baada ya kumbadilishia dawa, hali ya mgonjwa haikuonyesha matumaini
> yoyote. Kadri muda ulivyosegea ndipo hali ilipozidi kuwa mbaya zaidi. Mimi
> na
> jamaa yangu tuliyekuwa naye pale hospitali tulishikwa na butwaa. Tulifikia
> hatua
> ya kutaka kumchukua mgonjwa wetu tumpeleke hospitali yoyote ya binafsi
> akatibiwe. Lakini kwa kuwa mgonjwa alikuwa mikononi mwa madaktari tulizidi
> kupiga moyo konde. Wakati huo ngozi ya mgonjwa ilishaanza kubadilika na kuwa
> ya
> manjano.
>
> Kwa
> bahati nzuri alikuja daktari mmoja kumpokea yule wa asubuhi. Wakati anagawa
> dawa kwa wagonjwa alimfikia mgonjwa wangu. Akautazama mwili wa mgonjwa na
> kugundua kwamba rangi imeanza kubadilika kutoka ya manjano kuwa ya kijivu.
> Alimchunguza
> kwa kumbonyeza kwenye kucha na kumchungulia chini ya macho yake. Alitanabahi
> kwamba
> mgonjwa ana upungufu mkubwa wa damu. Alimuagiza nurse achukue damu ya
> mgonjwa
> na kuipeleka maabara kupima kundi la damu. Ili kuepuka ucheleweshwaji
> kwenye
> maabara, mgonjwa alibainisha kundi lake la damu. Kumbe aliwahi kupima siku
> za
> nyuma, hivyo kundi la damu yake alikuwa analifahamu. Baada ya masaa kadhaa
> mgonjwa
> alitundikiwa chupa (unit) moja ya damu na ilipoisha akaanza kupata nafuu. Na
> yale
> maumivu ya kichwa na viungo aliyokuwa akiyapata yakawa yamepungua kwa kiasi
> kikubwa. Rangi ya ngozi yake ikaanza kurejea kawaida. Daktari alishauri
> atundikiwe drip ya maji huku akisubiri kuongezewa unit nyingine ya damu.
>
> Baadaye
> nilienda kwenye benki ya damu kuomba mgonjwa awekewe unit nyingine ya damu
> kama
> daktari alipokuwa ameshauri, nikaishia kupigwa danadana mpaka siku
> iliyofuata. Kesho
> yake nilifanikiwa kulazimisha mgonjwa awekewe damu nyingine—akafanikiwa
> kuwekewa
> chupa ya pili. Baada ya nusu ya damu kuingia, mgonjwa alianza kuhisi
> kuchefuchefu na maumivu makali ya kichwa. Hali ikazidi kuwa mbaya kadri
> muda
> unavyoenda. Nikamuita daktari na kumueleza kuhusu hali ile. Daktari
> akachukua
> uamuzi wa kuondoa ile chupa ya damu iliyokuwa imetumika nusu. Ndipo mgonjwa
> akapata afueni na kurejea katika hali ya kawaida. Nikaingiwa na wasiwasi
> kwamba
> huenda ile damu aliyokuwa ametundikiwa itakuwa na hitilafu ya kiufundi
> lakini
> daktari aliniondoa hofu kwamba hiyo ni hali ya kawaida kutokea—eti damu
> ili-react! Haya, bwana.
>
> Katika
> siku hizi zote bado majibu ya kimaabara yalikuwa bado hayajatoka na
> zilikuwa
> zimepita siku nne (4) tangu mgonjwa huyu alazwe hosiptalini pale. Mgonjwa
> alikuwa
> akitibiwa kwa kudhania na kuhisi. Mara ahisiwe kuwa na taifoidi, mara
> vidonda
> vya tumbo, nk—ilimradi hakuna anayejali! Lakini jambo la kusikitisha na
> kustaajabisha
> ni kwamba katika siku zote hizi mgonjwa alikuwa akitibiwa kwa dawa za
> kununua
> kwani tuliambiwa kwamba hospitali haina hata kidonge kimoja cha dawa. Hakika
> hakukuwa
> hata na kidonge kimoja cha bure kwenye stock ya hospitali. Dawa zote
> zilizokuwa
> zinaandikwa na madaktari zilikuwa zinanunuliwa kwenye duka la dawa lilipo
> kwenye
> lango la kuingilia hospitalini humo. Ikiwa dawa iliyoandikwa itakosekana
> kwenye
> duka hilo, kama ilivyokuwa inatokea mara kwa mara, ilinibidi niende
> nikainunue
> kwenye maduka ya dawa ya mjini. Yaani Hospitali ya rufaa eti inakosa hata
> bomba
> moja la sindano, kidonge kimoja cha panadol, piliton, diclofenac, nk!
>
> Baada
> ya kukaa hospitalini kwa muda wa siku tano (5), Mungu alitenda muujiza
> mgonjwa
> wangu akapata nafuu na kuruhusiwa kuondoka. Hakuwahi tena kuongezwa damu
> nyingine baada ya ile chupa ya pili kudunda. Mgonjwa aliruhusiwa bado tukiwa
> na
> madawa lukuki aliyoandikiwa na ambayo alipaswa kunywa ili kusaidia kubaini
> ugonjwa wake. Kuna dawa moja inaitwa barium meal (barium sulphate) ambayo
> alitakiwa anywe ili kusaidia kubaini kama alikuwa anasumbuliwa na vidonda
> vya
> tummbo au la. Lakini mpaka anaruhusiwa, hakuwa amejua ni nini hasa
> kilichokuwa
> kimemsibu hadi kuvuja damu ndani ya mwili (internal bleeding), hali
> iliyopelekea kujisaidia na kutapika mabonge ya damu. Ila tunamshukuru Mungu
> tu
> kwamba aliongezewa damu iliyosaidia kutetea uhai wake, vinginevyo hata
> tungeweza kumpoteza kutokana na upungufu mkubwa wa damu uliokuwa unamkabili.
> Tulikata
> shauri ya kutorudi tena hospitali ya umma kwani kupona kwa wagonjwa katika
> hospitali
> hizi ni kwa kudra za Mungu—kwa kuwa kule hakuna dawa wala vifaa tiba hata
> kidogo.
>
> Cha
> kushangaza na kukera zaidi, wagonjwa walikuwa wanaambiwa kwamba dawa za
> bure/kuchangia
> hakuna; lakini mtu akitaka za kununua zipo tele kwenye famasi ya hospitali.
> Inawezekanaje
> tuambiwe hakuna dawa lakini dawa za kununua zipo tele, tena kwenye famasi
> ya
> hospitali? Kama sio ufisadi ni nini? Labda huu ndio utaratibu wa
> serikali—kwamba
> dawa zote zinunuliwe lakini ushauri utolewe bure. Ama ni mpango mahususi wa
> kuwaua raia wasiokuwa na hatia? Haya maswali yanapaswa kujibiwa na serikali
> kwani ndiyo inayokusanya kodi kutoka kwa raia na kuahidi kutumia kodi hizo
> kwa
> manufaa ya umma. Ndiyo inayopaswa kujibu kodi zetu zilipo na kama huko
> ziliko
> zinamnufaisha nani zaidi ya wananchi. Wagonjwa wanachokifuata kwenye
> hospitali
> za umma ni kuandikiwa dawa za kununua na kupata ushauri wa bure. Kama hali
> ni
> hii, kuna umuhimu gani wa hospitali za umma basi? Si zifungwe zote ili
> wananchi
> wakatibiwe kwenye hispitali binafsi na wale wasiokuwa na uwezo wafie
> nyumbani!
>
> Hii
> ni moja ya hospitali za rufaa, ambayo tungetarajia itoe huduma nzuri na za
> kuridhisha lakini huduma zake ni tofauti na hadhi yake. Kwa mujibu wa
> utafiti
> wangu hospitali hii ina majengo na vyumba vya kutosha kwa ajili ya kutolea
> huduma za kitabibu na utawala. Ingekuwa majengo ndiyo tiba, basi hakuna
> mgonjwa
> hata mmoja ambaye angekufa kwa kukosa huduma za kiafya. Kama hali kwenye
> hospitali ya rufaa ndiyo hii, je huko kwenye hospitali za chini—mkoa,
> wilaya,
> vituo vya afya na zahanati—hali ikoje?
>
> Nilishuhudia
> sio chini ya wagonjwa watano wakifariki kila siku kutoka kwenye kila wodi
> katika wodi zisizopungua 12! Hii maana yake ni kwamba kila siku hospitali
> hii
> huua wagonjwa wasiopungua 60 kwa siku au 1,800 kwa mwezi. Kwa mwaka mzima
> idadi
> hii inafikia wagonjwa 21,600. Hii ni idadi ya watu wanaotosha kukaa kwenye
> kijiji kimoja. Kwa lugha nyingine ni kwamba hii hospitali huteketeza kijiji
> kizima cha watu kila mwaka. Na vifo hivi vinahusisha hospitali moja tu ya
> umma.
> Tukijumlisha idadi ya watu wote wanaouliwa katika hospitali zote za umma,
> hesabu
> yake inatisha! Mauaji haya ni makubwa na mabaya kuliko yale yaliyofanywa na
> M23
> au yanayoendelea kufanywa na vikundi mbalimbali vya kigaidi kama vile
> alqaeda,
> alshaabab, bokoharamu, nk. Hapa ndipo mtu unapogundua kwamba kwa mwaka mzima
> serikali
> hii inaua watu wengi zaidi ya wale wanaouliwa kwenye vita vya kigaidi.
>
> Matukio
> niyoshuhudia mle wodini yanatisha sana kuyasimulia. Kuna babu mmoja aliletwa
> mle
> wodini majira ya jioni. Alikuwa anaharisha na kuhisi maumivu makali ya
> tumbo. Tofauti
> na umri wake, maumivu yale makali yalimsababisha alie kama mtoto mdogo.
> Wakati
> akiendelea kulalamika na kulia, daktari alikuwa anamsikia na kumpita kama
> vile
> hamuoni. Hali ilipokuwa mbaya zaidi, kijana alokuwa ameambatana na yule
> babu
> akamsihi daktari amsikilize babu yake na kumsaidia kwa kadri atakavoweza.
> Daktari
> akamsadia kwa shingo upande—akamuandikia dawa za kununua. Alimuandikia
> akanunue
> maji ya dripu, vidonge vya maumivu (panadol/piliton/diclofenac?), gloves,
> mabomba ya sindano, set ya vifaa vya kutundikia maji, nk. Akamuelekeza
> akanunue
> vifaa hivyo kwenye famasi ya hispitali au kama atavikosa huko akanunue
> kwenye
> duka la dawa lilipo mkabala na lango la kuingilia hospitalini. Kwa bahati
> mbaya
> sana, yule kijana hakuwa na fedha za kununulia vile vifaa.
>
> Ikabidi
> wasamalia wema mle wodini wamsaidie baadhi ya vidonge walivyoandikiwa
> wagonjwa
> wao kwa makubaliano kwamba angevirejesha siku inayofuata. Babu alimeza
> hivyo
> vidonge vya kuazima lakini havikusaidia kitu. Bado alizidi kulalamika na
> kulia
> kama mtoto mdogo. Alianza kuharisha maji maji mwanzoni lakini kadri muda
> ulivyoenda,
> akaanza kuharisha damu na hatimaye akaishiwa nguvu kabisa. Aliendelea
> kuteseka
> hivyo usiku kucha hadi ilipofika saa tano asubuhi ya siku iliyofuata
> akafariki dunia
> hata kabla ya kupata tiba yoyote ya maana na bado akiwa hajachukuliwa
> vipimo.
>
> Kwa
> uzoefu wangu, yule babu alifariki kutokana na taifoidi iliyokomaa/sugu
> (chronic
> and severe typhoid) kwani dalili zote zilionyesha kwamba alikuwa akiumwa
> ugonjwa
> huo. Kwa mujibu wa mjukuu wake aliyeambatana naye hospitalini, alidai
> kwamba
> kabla ya kufikishwa pale alikuwa akitibiwa kwenye zahanati moja ya serikali
> na
> kwamba tiba kubwa aliyokuwa akiipata huko ni vidonge vya kutuliza maumivu
> alivyokuwa akivinunua—kwa kisingizio kile kile cha ukosefu wa dawa kwenye
> hospitali za umma!
>
> Katika
> wodi ile (Ward No.8) nilishuhudia wagonjwa wengine wasiopungua watano (5)
> wakifariki,
> sio kwa sababu ya kuugua magonjwa ya kutisha, ila kwa sababu ya ukosefu wa
> dawa. Wagonjwa walikuwa wakifariki kutokana na magonjwa ya kawaida kabisa
> kama
> vile malaria, typhoid, dysentery, safura, nk. Haya ni magonjwa ya kawaida
> kabisa yanayoweza kutibiwa kwenye zahanati na vituo vya afya au kwenye
> hospitali
> za wilaya na mkoa. Badala yake wagonjwa hukimbilia kwenye hospitali za
> rufaa
> wakidhani kwamba kule kuna afadhali kumbe yale nayo ni makaburi tu!
>
> Jambo
> lingine nililoshuhudia pale ni kwamba madaktari wapya (interns) huachiwa
> wafanye
> kazi wenyewe bila usimamizi wa dakari bingwa au mzoefu. Matokeo yake
> daktari
> mpya akipata kesi inayomshinda, hasa wakati wa usiku, hana wa kumuuliza.
> Hii
> hupelekea hawa madaktari wapya kubuni tiba na hatimaye kuua wagonjwa kwa
> kuwafanyia
> majaribio ya kitabibu. Jamani mwili wa mtu sio wa kufanyia majaribio hata
> kidogo. Mwili sio kipande cha mbao kwamba daktari akikosea upasuaji atakata
> kipande cha nyama au mfupa kutoka sehemu nyingine aje aunganishe kwa gundi
> kupata kiungo kipya.
>
> Ndugu
> zangu, kwa hali hii mtu asije akazidiwa kwenye zahanati au hospitali ya
> binafsi, akajifariji kukimbilia hospitali ya mkoa au rufaa ya serikali. Kule
> utakuwa
> unakimbilia kwenye kifo. Ni afadhali ubaki huko kwenye zahanati/hospitali
> ya
> binafsi ukafie huko kuliko kuwasumbua ndugu zako wakupeleke kwenye hospitali
> ya
> umma iliyo mbali uje uwape shida ndugu zako kusafirisha maiti yako umbali
> mrefu
> kwenda kuzika nyumbani. Mtu yeyote mwenye ufahamu simshauri aende akatibiwe
> hospitali ya umma. Labda upelekwe kule ukiwa kwenye ambulance na ukiwa
> hujitambui. Vinginevyo, usikubali kwenda kufa kirahisi na kwa haraka kwenye
> hospitali ya serikali. Bora ubaki kwenye hiyo hospitali/zahanati ya umma
> Mungu
> anaweza kufanya muujiza ukapona. Ugonjwa ukishinikana kwenye hospitali ya
> binafsi ni bora ukarudi kwenye tiba mbadala kuliko kujidanganya kwenda
> hospitali ya rufaa ya umma. Utakufa siku hiyo hiyo!!!
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni
> taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forum" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
mission without implementation is hallucination
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment