Wednesday 4 December 2013

[wanabidii] Rais Kikwete awapandisha vyeo Maafisa Wakuu 4 wa Jeshi la Polisi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa nafasi za madaraka katika Jeshi hilo kufuatia mabadiliko ya muundo wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na ambao wote walikuwa ni Naibu Kamishna wa Polisi 
ni DCPErnest Mangu, DCP Thobias Andengenye, DCP Abdulrahaman Kaniki na DCP Hamdan Omari Makame.

Rais pia amempandisha cheo SACP Athuman Diwani kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.

Walioteuliwa katika nafasi za madaraka katika Jeshi la Polisi ni CP Clodwing Mtweve ambaye anakuwa Kamishna wa Fedha na Utaratibu wa Ugavi na Usafirishaji wa Watu na Vitu (Logistics),CP Paul Chagonja ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Isaya Mungulu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya jinai (DCI), CP Mussa Ali Mussa ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.

Wengine ni CP Hamdan Omari Makame ambaye anakuwa Kamishana wa Polisi, Zanzibar; CP Ernest Mangu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Jinai, CPThobias Andengenye ambaye anakuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, CP Abdulrahman Kaniki ambaye anakuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Ushahidi wa Jinai na CP Abdulrahman Diwani ambaye anakuwa Naibu Mkurugenzi wa DCI.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Desemba, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment