Thursday 5 December 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA KIONGOZI WA KIKOSI CHA ULINZI CHA CHADEMA ( RED BRIGADE )

Wanabidii siku hizi limekuwa ni group la kusambazia ujinga! Linaondoa mvuto kwa wanachama na wananchi, yawezekana Moderator anaona ni njia rahisi ya kuvutia wanachama humu ndani kwa kutumia majina bandia na yenye lengo la kupoteza muda wa wanabidii!


2013/12/5 F Kitigwa <kitigwa@gmail.com>
Tuondoleeni upuuzi huu


2013/12/5 MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com>
Ndugu Wanahabari,
Awali ya yote kwa jina naitwa Jumanne Samwel , ni mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo mwenye kadi namba 0154352 ya mwaka 2007,nimekuwa kiongozi wa redbrigedi mikoa mingi tu hapa Tanzania 

Nimekuwa mwanachama mwaninifu wa chadema kuanzia mwaka huo mpaka leo hii.

Katika tamko langu hili nitajikita katika mambo makuu matano;- 

1.Ubaguzi
2.Ukabila
3.Ubinafsi 
4.Uhafidhina
5.Utapeli
Tangia nimekuwa mwanachama wa hiki chama , chama chetu kimekuwa kikisumbuliwa sana haya matatizo niliyoyaweka hapo juu, nitaeleza moja baada ya linguine.

UBAGUZI
Ubaguzi ni kitu ambacho kimekuwa ni kama donda ndugu ndani ya chadema, 

Ndugu wana habari,
Kwa kuanzia tu tangu viongozi hawa wa juu wa chama wachukue chama , wamekuwa na ubaguzi wa wazi wazi wa wanachama na viongozi wengine ambao kwao wanaonekana si watiifu kwa mwenyekiti na timu yake ile inayoamini kwenye zidumu fikira za mwenyekiti , 
Kila aliyejaribu kuhoji hili swala aliitwa majina mbali mbali, wengine waliitwa sisimizi , wengine wasaliti na wengine waliitwa ni wahaini ilimradi kila mtu alitwa kwa jina lake ,
Swala la posho za vikao lilikuwa ni msimamo wa chama kuwa viongozi wetu hasa wabunge wasichukue , mzee shibuda alisema ni mhimu posho zikachukuliwa akaonekana ni msaliti na kila mmoja ndani ya chama hasa upande wa mwenyekiti ulionekana kulichukulia bango swala hilo na mpaka ilifikia kipindi aliaandikiwa barua ajieleze na kamati iliundwa ya kumchunguza, 

Miezi michache tu baadaye mbunge wa Rombo selasini alikuja na swala hilo hilo la posho akidai ziongezwe lakini si mwenyekiti wala katibu mkuu wala kiongozi mwingine yoyote aliyeinua mdomo wake kumsema, na Lema pia naye muda si mrefu kadai posho ziongezwe na viongozi wote wako kimya , hapo ndipo swali likaja je Shibuda aliandamwa kisa yeye msukuma au kwa kuwa hatokei kaskazini? Maana wenzake wote waliotokea kaskazini hawakusemwa na chama .

Ndugu wanahabari,

Kama hiyo haitoshi, mmoja wapo wa waasisi wa chama hiki alikuwa anatokea Mkoa wa shinyanga na amekuwa mwenyekiti wa Taifa wa chama hiki kwa kipindi kirefu tu , amekitumikia chama kwa uaminifu mkubwa sana na wakati mwingi ametumia raslimali zake mwenyewe kukijenga chama na hata hayo makao makuu ya CHADEMA aliyenunua yeye enzi za uongozi wake wakati chama kikiwa na wabunge watatu tu na ruzuku ikiwa ni kidogo sana .

Leo chama kina ruzuku ya kutosha bado chama wilayani na mikoani ofisi ni kama vibanda vya kuchomea kitimoto au kwa kifupi ni kama bucha na viongozi wa wilaya na mikoa wanaambiwa wafanye kazi za kujitolea wakati watumishi wa makao makuu wakilipwa mishahara bila kodi na kuziita posho ambazo ni kati ya 1.5m na 2.5m kwa mwezi.Lakini afya yake ilipoanza kuyumba na kutakiwa kwenda kutibiwa india chama kilisema hakina pesa kina pesa za kufanya maandamano na kukupeshana , maana katibu mkuu alijikopesha million 40+ utadahani hii ni saccos na mpaka leo haijulikani kama alishalipa au bado,lakini pesa ya matibabu kwa muasisi haikuwepo , hata musiba wake ambao wanahabari naamini ingekuwa si BOT leo tungekuwa tunaongea mambo mengine maana chama kilisema hakina pesa ya mazishi.

Pia mtakumbuka kifo cha aliyekuwa mshindi wa ubunge wa jimbo la shinyanga mjini ambaye bahati mbaya hakutangazwa ndugu shelembi, msiba wake ulitikisa nchi nzima lakini cha ajabu viongozi wa taifa wa chadema walisema hawana pesa za kugahramia mazishi na wakamuomba mh. Shibuda atoe pesa yake mfukoni kwa ajili ya mazishi na kuahidiwa kuwa pesa zake atarudishiwa kipindi pesa zitakapokuwepo lakini mpaka leo tunapoongea hakuna kilicholipwa na hawataki kumsikiliza na zaidi anatishiwa kufukuzwa ndani ya chama .

UKABILA ,
Hili limekuwa likizungumzwa sana na viongozi wamekuwa wakilitolea majibu rahisi rahisi tu kuwa hizi ni propaganda za chama cha mapinduzi, napenda leo niwahakikishie tunaposema kuna ukabila ndani ya chama chetu tunataka watanzania wote wajue kuwa ukabila upo na ukanda, hata katika kurungezi sita za chama kurugenzi nne zinaongozwa na watu wa kutoka mkoa mmoja ,kama hiyo haitoshi ukijaribu kuangalia uwianao wa kura za urais na idadi ya wabunge wa viti maalum utagundua kuwa baadhi ya mikoa pamoja na kutoa wabunge wengi wa kuchaguliwa na kupata kura nyingi za urais bado wabunge wa viti maalum hawakuweza kupatikana katika hayo maeneo mfano mzuri ni mkoa wa shinyanga kabla mkoa wa simuyu haujazaliwa , kwa taarifa tu ni kwamba huu ndiyo mkoa pekee Tanzania nzima uliotoa kura nyingi kwa mgombea urais wa Chadema Mzee slaa, pamoja na kutoa kura laki tisa kwa mgombea urais na kutoa wabunge watano pamoja na kwamba mmoja hakutangazwa bado hauna mbunge wa viti maalum aliyetoka ndani ya mkoa huu zaidi ya usanii wa kuletewa mbunge mmoja kutoka makao makuu asiyekuwa na uwezo wowote kisiasa na kuambiwa akawe ndiyo mbunge wa viti maalum shinyanga, ilhali mikoa kama Kilimanjaro ambapo wana wabunge wawili lakini mkoa una wabunge wa viti maalum wawili na hata dsm kuna wabunge wa viti maalum wawaili na wabunge wa kuchaguliwa wawili, hii ni dalili kubwa sana ya ubaguzi na ukabila hata kwenye kupeana vyeo, na hata ukiangalia sura nyingi za wabunge wa viti maalum ni either ni ndugu au hawara wa viongozi wakuu wa chama chetu na hata wakiwa bungeni utadhania wako sebuleni.

UBINAFSI.
Ubinafsi wa baadhi ya viongozi wa chama makao makuu ya kutumia ruzuku zote bila kujali wilayani na mikoani kunaendeleaje ni swala pia linalokisumba chama change, juzi mwenyekiti wa taifa katoka kumfukuza mwenyekiti wa chadema mkoa wa Mara kisa hafanyi mikutano bila kueleza waliwahi hata kumpelekea vifaa vya chama mkoani kwake??, kadi, bendera na hata ruzuku hazifiki mkoani walitarajia huyo mtu afanye mikutano kwa kutumia raslimali zake ilhali wao wanajikopesha ruzuku na hata wakitumia za kwao huwa wanakikopesha chama tena kwa riba ya ajabu. Kuna baadhi ya wagombea wa chama mwaka 2010 ambao ni kaa vile walikuwa wagombea binafsi tu maana vifaa vyote vya chama havikufika jimboni mfano mzuri ni mtela mwampamba aliyekuwa mgombea wa Chadema jimbo la mbozi mashariki alijitahidi ana alipata kura 32,000 na mshindi wa jimbo alimzidi kura chache tu , lakini mwisho wa siku alifukuzwa ndani ya chama kisa alihoji matumizi ya ruzuku na vifaa vya chama kutokufika mbozi.

UHAFIDHINA
Hili jambo limekisumba sana chama changu hasa pale uchaguzi mkuu ndani ya chama unapokaribia kuna watu lazima wafukuzwe kisa eti wanapanga mbinu chafu za kuwatoa viongzi waliopo kwa njia zisizo za kikatiba , kafulila na Danda juju walikumba na hilo tatizo mwaka 2009 hasa baada ya kuonekana ni vinara wa kumuunga mkono zitto kugombea uenyekiti na mwaka huu Samson mwigamba, zitto mwenyewe na dr kitila mkumbo yamewakumba kwa kuandaa waraka wa siri wa ushindi wa mwaka 2013, sijawahi kuona duniani kote mbinu za ushindi kuwekwa wazi , hata sisi wapinzani tunataka kuingia ikulu na mbinu za kushinda uchaguzi hatuwezi kuziweka wazi kwa adui zetu na wapinzani wetu ambao ni chama cha mapinduzi
Ndugu wanahabari kwa kweli hii ni dalili mbaya sana kwa demokrasia ya chama chetu na hata upinzani kwa ujumla , kama mtu anayeandaa waraka wa siri ya ushindi anaitwa MHAINI , kwa maana hiyo hata wapinzani wote ndani ya nchi hii ni wahaini maana hata wao wana nyaraka zao za siri kwa ajili ya kuitoa ccm madarakani. Tunahitaji kuwa makini sana na hawa watu maana kama wanafanya hivi na ukiwakosoa unafukuzwa uananchama siku tukiwapa nchi tutkiwakosoa watatunyang'anya uraia. Hawa ni waoga wa demokrasia na hawaishi kwa yale wanayoyahubiri , wanapaka chokaa makaburi ili yapendeze lakini ndani yake ni mifupa mitupu, sisi kama vijana wapenda mabadiliko hatupendi na hatutakuja kupenda hilo litokee. Muda si mrefu katibu wangu mkuu Dr Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kuulizwa juu ya tarehe ya uchaguzi mkuu ndani ya chama alitoa majibu ambayo kwa kiasi kikubwa ilinisabibishia nilie machozi, alisema kuwa CHADEMA haitafanya uchaguzi mpaka pale chama kitakaojiimarisha , wazo la harala haraka lilokuja kichwani mwangu ni kuwa kama hawa watu hawataki kufanya uchuguzi ndani ya chama , je siku tukiwapa nchi hawa watu hawatafanya uchaguzi tena mpaka uchumi wan chi utakaopkuwa imara.

UTAPELI
Kumekuwa na utapeli wa wazi wazi ndani ya chama change , mwenyekiti wa ngu wa taifa amegeuka kuwa ndiyo supplier na purchasing officer wa chama , hata kadi amekuwa akiagiza yeye kinyume na katiba ya chama. Hata lile gazeti la Tanzania daima ambalo liamilikiwa na freemedia ilikuwa ni msaada kutoka ujerumani kwa ajili ya chama lakini watu walijimilikisha likawa la kwao, kama hiyo haitoshi mamilioni ya Sabodo leo ukiuliza yalienda wapi hakuna atakaye kujibu badala yake utatishishiwa kufukuzwa kwenye chama , na hata pesa za M4C amabzo wananchi wa Tanzania walikichangia chama lakini hata leo ukiuliza hizo pesa ziko wapi au zilifanya kazi gani bado unajitakia matatizo
Ndugu wanahabari , wakati wa mazishi ya mgombea ubunge wa Shinyanga mjini Marehemu shelembi mwenyekiti wa CHADEMA taifa aliahidi kuimalizia nyumba ya marehemu lakini hadi leo tunavyoongea hakuna kilichofanyika zaidi ya vijana wachache waliojitolea kuijenga hiyo nyumba kwa vijesent vyao vidogo wanavyopata , waliamua kufanya vile baada ya kusikia mbunge wa sasa wa hilo jimbo bwana Masele na CCM kwa ujumla walikuwa na huo mpango wa kuijenga hiyo nyumba. Hiyo ilikuwa ni aibu kwa chama hasa ukichukulia nguvu aliyokuwa nayo marehemu ndani ya chama na ndani ya mkoa wa shinayanga kwa ujumla.

HITIMISHO
Kwa hayo yote niliyoyaeleza hapo juu ndugu wanahabari , nakumbuka tarehe 27 mwezi huu Brigedia Nyakarungu alitangaza uasi dhidi ya wahafidhina ndani ya chama na mimi naungana naye kwa nguvu na moyo wote, Natangaza kuwa sisi Red brigedi hatttawalinda tena viongozi hawa wabinafsi kwa kujitolea mpaka kwanza wataje mapato na matumizi ya pesa za ruzuku na zile za M4C na wale viongozi waliopewa uongozi kinyemela ifikapo tarehe kumi mwezi wa December wawe wameachia .
Tunaomba pia hawa watu waliovuliwa nyadhifa zao warudishiwe mara moja vinginevyo patachimbika.
Asanteni sana kwa kunisikiliza ni mimi 
Jumanne Samwel 
Mwenyekiti wa Redbrigedi
Tanzania

0767 777761

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Ipyana Lwinga
Email:    ipyanalwinga@gmail.com

"Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment