Wednesday 4 December 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA CHASO TAWI LA MOROGORO KUHUSU ZITTO KABWE NA KITILA MKUMBO

Good! Nyie ni wanachama wa Chama, siyo wanachama wa mtu!!!!!!!!!!!
Binafsi, naunga mkono wanachama wa "mtu" waendelee kujitoa tu!



--------------------------------------------
On Mon, 12/2/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] TAMKO LA CHASO TAWI LA MOROGORO KUHUSU ZITTO KABWE NA KITILA MKUMBO
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, December 2, 2013, 12:09 AM

CHAMA
CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO 


CHASO
MKOA


S.
L. P 1976,


MOROGORO


30
November, 2013




TAARIFA
RASMI YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA CHADEMA VYUO VIKUU (CHASO)
MKOA WA MOROGORO KWA VYOMBO VYA HABARI. 




Ndugu
Wanahabari,




Ni
matumaini yangu kuwa mu wazima na hongereni kwa kazi ya
kupasha habari kwa umma wa watanzania. 

Tumewaita
hapa kuzungumza na umma wa Watanzania kupitia ninyi, na tuna
mambo machache ya kuzungumza na kupasha umma kuhusu
yanayoendelea ndani ya chama chetu.




Kufuatia
kikao cha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHASO Mkoa wa Morogoro
kilichofanyika tarehe 30.11.2013, kuanzia saa 4.00 asubuhi
hadi 8.00 mchana katika ofisi za CHADEMA Mkoa wa Morogoro,
kilichohudhuriwa na viongozi wa vyuo vikuu vya Mkoa wa
Morogoro (Wenyeviti, Makatibu,na makatibu wenezi), wajumbe
wa mkutano kwa kauli moja wameunga mkono maamuzi
yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya Chama dhidi ya Zitto Zuber
Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.




Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama makini na
umakini wake umethibitishwa na maamuzi yake dhidi ya
wahujumu chama na wanaojiona miungu watu ndani ya chama
chenye sura na matendo ya kidemokrasia, na kinachomthamini
kila mtanzania.




Kwa
mantiki hii na kwa tukio hili lililofanywa mbele ya
watanzania, ni dhahiri kwamba CHADEMA kimekomaa na kinafaa
kupewa jukumu la kuiongoza nchi kwani maamuzi magumu (na
yenye manufaa kwa umma) ndiyo maamuzi stahiki kwa chama
chochote cha siasa nchini na kote ulimwenguni.




Vipo
vyama vingi vya siasa nchini (mathalan CCM) ambavyo vimekuwa
vikiwaingiza wananchi kwenye nyakati ngumu na dimbwi la
umaskini kwa kuwa tu, wanawalinda mafisadi, wasaliti, na
watu wenye maslahi yao binafsi.

Taswira
aliyoionesha Zitto Kabwe ni taswira mbaya na haifai kuigwa
na kijana au mtu yeyote kwani kinachoonekana ni kwamba
ameyatanguliza mbele maslahi yake binafsi na kuyaacha ya
taifa na chama chake.




Zitto
Kabwe amehasi chama na taifa kwa ujumla na ameshindwa
kutekeleza majukumu yake sawia kama chama kilivyokusudia
hadi kumpa jukumu la Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi ambayo
ni nyeti sana ndani ya chama kinachokuwa kwa kasi kama
CHADEMA. 




Kama
kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama, alikuwa na uwezo wa
kuwashauri viongozi wenzake wa ngazi ya juu ndani ya chama
pale walipokosea (kama kweli makosa yapo) na siyo kutumia
nafasi hiyo kujitafutia mtaji binafsi wa kisiasa (personal
political capital).




Kwa
misingi ya hoja hii, hata kama kuna makosa yaliyofanywa na
viongozi wenzake ndani ya chama, bado Zitto Kabwe hafai
kuendelea kupewa jukumu lolote kwani kushauri mfumo (system)
unapokosea ni jukumu la mwanachama yeyote na siyo kutafuta
umaarufu ndani ya chama kwa kuombea viongozi kufanya
kosa.




Wapo
wanachama wanaokesha kwenye mitandao ya kijamii kuandika
kwenye kurasa (pages) za viongozi waandamizi wa chama,
wakiwa na lengo la kurekebisha au kutoa taarifa ya kukikuza
chama hiki na kukilinda. 




Hii
ni kutokana na kutokuwa na ukaribu wa kutosha na viongozi
hawa ili wawashauri. Tunamsikitikia ndugu Zitto Kabwe mwenye
ukaribu na access ya kuonana na kiongozi mwenzake yeyote
anayemhitaji na wakati wowote anayahifadhi mapungufu ya
chama mfukoni ili kesho anunue umaarufu binafsi yeye na
familia yake.




Pia
CHASO Mkoa wa Morogoro kupitia viongozi na wawakilishi wa
vyuo vikuu, tunawataka wanachama wa CHADEMA kuwa na subira
na utulivu katika kipindi hiki cha mpito ndani ya chama
kwani chama kinategemea nguvu ya umma katika kufanya maamuzi
yake na CHADEMA ndilo tumaini jipya kwa
Watanzania. 




Pia
tunawasisitiza wanachama na viongozi kutoterereka na
kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi au kikundi chochote
chenye itikadi kinzani na ya chama na kuepukana na
propaganda za wapinzani kwamba hoja giza katika maamuzi haya
ni Hofu ya uongozi wa juu ndani ya chama (uenyekiti) jambo
ambalo halina ukweli wala haliwezi kusadikika kuwa na ukweli
wowote kwani yeye (Zitto) siyo mtu wa kwanza kuadabishwa na
chama kwa utovu wa nidhamu binafsi na ya umma, wapo wakina
David Kafulila, Danda Mjuju na wengine wengi ambao
waliwajibishwa pale tu walipokwenda kinyume na chama na
matakwa ya kanuni na katiba ya chama.

Ahsanteni
sana kwa kunisikiliza,


Wenu
katika Mapambano, 


Ebenezer
F. Kwayu.


Mwenyekiti
CHASO, Mkoa wa Morogoro 


Na


Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Mkoa BAVICHA, CHADEMA 


0764013330


ekwayu@ymail.com





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment