Tuesday 10 December 2013

Re: [wanabidii] MHE FREEMAN MBOWE APIGWA DONGO BUNGENI

Sasa kama mtu aliisha kulipwa posho na kulipiwa gharama, akikatisha safari atarudisha posho aliyopewa?

Ni gharama kubwa sana tena sana kupeleka team za wabunge wa TZ nchi mbali mbali kujifunza hili na lile. mara Dubai, Nowary kuhusu Gas; Mara China kuhusu hili na lile. lakini matokeo yao yanakuwa hayaonekani. Badohiyo posho ya kuwalipa. Hizi hela watumiazo zingejenga barabara, majosho na handpump wells ngapi. Unawapeleka wakirudi malumbano na vijembe na kufukuzana ktk vyama. Ifike wakati TZ tuamue kuacha uroho na ubinafsi tufanye kazi za maendeleo. Viongozi waangalie ukubwa wa posho zao waone kama ni haki kumtendea mwananchi masikini hivyo. Serikali ikataze posho za vikao kijiji, kikata, wilaya, mkoa, wizara, vyuo. Watu wanakutana wakati wa muda wa kazi au wa bunge, wanalipwa posho nawanapokea mshahara. wale waliajiriwa unakuta kuna workshop ya kuwahusisha katika kupanga mradi labda wa maji au barabara, mazingira, uhifadhi wa bonde. Muda wa kazi. anapewa soda na lunch. Lakini anadai posho 45,000/=-65,000/= kulingana na cheo chake. Hii ni gharama mara mbili na ndio maana hela zinatumika vibaya. kama kapewa soda au maji na vitafunwa inatosha. Amekuja na gari ya serikali na mafuta na ni sehemu ya kazi yake mafuta ya mikutano tayari budgeted for. Anarudishiwa hela za mafuta, anapewa lunch na posho na hela hizo za marejesho ya fuel hazifiki ofisini. Tuyaangalie haya. Wanaotupa hela za grants na mikopo wanaangalia na wakati mwingine kushindwa kuitisha vikao vya participatory planning kutokana na kukwepa gharama ya kuwalipa viongozi wote na staff wanaohitajika hela za kikao hicho ni milioni kubwa ambayo consultancy team or company haiwezi kumudu. Kisha wanasema hawajausishwa kutokana na vikao vya posho kutokuwepo.

Tujiangalie sasa sisi waafrika wa Tanzania, tunajirudisha wenyewe nyuma ktk maendeleo na kutumia gharama nyingi ktk mambo sio muhimu. Niambie, baada ya safari za timu makumi ulaya au nje ya nchi kujifunza-itaonekana wapi mabadiliko ya kujifunza. ikiwa pale mtaani, kijijini, jimbo , kata-Diwani hajali lolote katika mambo rahisi ya kuonekana kwa macho hafanyi kitu. Nyumba zipo wazi za wananchi wake, mvua inanyesha, tope la bure, vyoo hawana, wanakoga mtoni na kuchota maji kunywa hayo hayo, visima havihifadhiwi na kuhara ni ugonjwa unaoongoza na hafanyi kitu kuhamasisha wakandike nyumba, wakate nyasi na kuezeka na kujenga choo. Kichangisha shs 200 kila kaya wanunue siment wahifadhi kisima. watu elfu 3 kijiji kimoja ni @ mmoja 200/= ni shs 300,000/= ni mifuko mingapi ya cement ya kuhifadhi kusima kisiingie uchafu na matofari ya kuchoma wanafyatua wenyewe na kuuza na fundi wanao vijijini na nguvu kazi ipo-Na hafanyi hivyo. Unampeleka china kujifunza kufaidika na kilimo cha Miwa au gas-itamsaidia nini. Mbunge watu wanahamia mabondeni, wanatesa watoto ktk mazingira machafu, wanauza majumba kwa gharama na kuishi maisha mabaya zaid; Minazi na miembe na misitu imejaa Mtawa, mtawa na uwele, ufuta unakuwa kama takataka gari. Mikorosho usiseme, makumbi na kifuu na magogo ya mnazi kibao-hajafanya kitu. Mtu kazungukwa na makuti na nyazi na miti, mchanga, mto jirani na analima mpunga na vinginevyo-nyumba unamchungulia ndani, hakandiki, hana choo, kutwa yupo anacheza bao na kusikiliza mechi za mpira. Vitoto havisomi shule sana sana vinakwenda madrasa. Huyu ataleta mabadiliko gani kama anashindwa pale ambapo natural resources zote hizi zipo na hajahamasisha kitu cha maana. Vijana wanaweza kuzalisha mtama, ufuta-kujaza lori kupeleka DSM. Kujaza nazi, maembe-DSM, Arusha-wanahamia DSM kutembeza used items hadi siridia na vyupi used ulaya. Yupo anapiga kelele bungeni na kuona kufaidika na gas ndio issue. Uzembe katika kutumia raslimali zilizopo juu ya ardhi na maisha duni bila ya kujituma na uzururaji kijijini pamoja na raslimali zilizopo sasa sio issue kubwa. Tutaacha lini mitazamo hii finyu, usiasa, ulalamikaji, upigaji kelele tu bila ya kujituma? akija mchini kuchukua ardhi hiyo kulima na kusafirisha ufuta na mtama nchi-tutapanga foleni ya vibarua, kuypiga kelele kuibiwa ardhi ambapo sisi hatuzalishi. Next to Uyole au Sokoine na mbegu bora za muda mfupi-tupo tupo tunaliza zisizostahimili ukame kutokana na radha ya kulamba wakati wa kunywa uji. hatutaki kupanda za muda mfupi kulingana na mabadiliko ya tabia nchi. Viboko vya mjerumani virudi, kukakua nyumba, vyoo na mashamba. labda itasaidia kujituma. Kukagua mashamba yalimwe endelevu na kudhibiti wingi na aina ya mifugo. Kukataza kilimo na ufugaji usio endelevu. wakizurura na mifugo ikamate iuzwe, ukiwakuta wameingia kulima mbuga ya hifadhi-choma moto mazao kwani ukiwafunga utawalisha jela zitajaa.

 Bila ya kutumia ubabe sasa-hatutafika. Viongozi wawajibishwe kufanikisha haya ya maendeleo ktk maeneo yao. Hizi safari zao za nje zinaongeza gharama tu. Mbona wameshindwa kuhamasisha maendeleo pale kila kitu kipo hata mikakati ya sekta mbali mbali, sera na sheria zipo. wakienda Dubay, Norway itasaidia nini na mazingira, mitazamo ya binadamu, kujituma, utayari kiakili, utafakari kiakili, upendo kwa nchi yako, kujitolea mhanga kwa nchi na jamii yako ni tofauti? Tunapenda tu misifa, kusifiwa na kulaumu kutwa kusoma sera, sheria na kutafuta pa kupinga sio pa kujenga hata kimapendo. Ni kupinga hiki au kile na kukomoana ndio tija. Tuwapime wao wamefanya nini katika majimbo, wilaya, vijiji vyao katanai kwao. Wapingane madongo tu sisi sasa tupime field wamefanya nini katk akipichi chao cha uongozi ndio tuwachague.


On Tuesday, 10 December 2013, 19:36, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
MWENYEKITI WA CHADEMA MHE FREEMAN MBOWE APIGWA DONGO BUNGENI KUHUSIANA NA SUALA LA WABUNGE WA VITI MAALUMU KUCHUKUWA HELA MARA MBILI WANAPOKUWA KWENYE SAFARI ZA KIKAZI NA JUZI ALIVYOLAZIMISHA MBUNGE MMOJA ARUDI NCHINI KWA KULE KINACHOELEZWA KWAMBA NI WIVU WA KIMAPENZI 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment