Wednesday 25 December 2013

Re: [wanabidii] AJALI YAUWA WATU 5 MAENEO YA IGURUSI , MBEYA

Bila ya kurekebisha tabia zetu za kutokuzingatia usalama barabarani, vifo na vilema vitakuwa vingi maana kwa sasa kila mmojaanajaribu awe na gari, bajaji au bodaboda.

 Baadhi ya waTz ni waajabu-anaweza kuovertake mlimani, mtelemkoni, kwenye kona na kwenye roundabout kiasi kwamba ukiangalia afanyavyo unashangaa kama mtu mzima huyo ana akili au vipi. Anaweza kuovertake kisha akapinda kona akaingia ghafla uelekeo wa hapo jirani akasimama. Huoni rationale ya yeye kufanya hiyo overtake ghafla na kusimama mbele yako au kushoto kwako.

Wanaua watu na kutia vilema wasio na hatia. Ifike mahala tuwe kama china ili kuondoa uzembe. unaweza ukaona mkokoteni wa hizi baiskeli za mikuu mitatu, mini-pickup, lori limejaza magunia ya mkaa, matambara ya spongi au mizigo kupita kiasi. Kitoroli hicho hata dreva wake haonekani kwamba yakisogea na kumfunika kwenye huo mkokoteni ni kwamba magari ya nyumba yatampanda na kuleta mtandao wa ajali. lakini anapita barabarani na traffic police wapo, wanaona. Raia tunaona.

Bado dreva wa bodaboda hana kofia na wengi wanaranda mjini hawakamatwi. abiria kuvaa kofia muhimu lakini watu huogopa uchafu wa kofia za kuchangia na maradhi ya fungus, chawa na mengineyo ndio maana abiria wengine wanakataa kuvaa. Sasa hawa wasiovaa mbona wanaachiwa wanapita kila mmoja anawaona na sisi abiria tunawakodisha? Kisha itafikia-waziri ajitoe!

Ukipanda daladala unakuta imepewa leseni lakini viti vimebadilishwa cha kukaa watu wazima wawili kinatosha kukaa mtu mmoja na nusu. Vyuma vimebana hata miguu haiingia ukae vizuri. Ikitokea ajali ni wazi kwamba vyumba vitaingia matumboni na kukata miguu ya watu. Haya yanakuja toka ulaya na standard space for human being. Sisi tunabadili ili kuongeza wingi bila ya kujali standard measurements bali hela tu na unalazimika upande basi la namna hiyo kutokana na kuwa yanakwenda kwa foleni penda usipende na mengi yapo hivyo. Kukagua space ilivyo kabla ya kutoa leseni ya biashara ni muhimu sana ktk mabasi ya mjini na ya safari ndefu.

 Ifike mahala kama sheria ya usalama barabarani ikakamata wenye ujazo wa mizigo kupita kiasi kwa mijini na iwe bila ya kuchukua rushwa-watanzania wataacha. Kukamata pia bodaboda na bajaji zinazopita mjini zimewema music sauti ya juu ambapo dreva hawezi kusikia warning ya tahadhari yoyote toka vyombo vingine na kuzuia usikivu wa wenzake. Traffic wanaona yote haya lakini ni vipofu kiakili. Huu uhuru tunaowaachia wavunjao sheria inakuja kuwa mazoea halafu sheria ikichukuliwa tunaona tunaonewa na kuanza mapambapo na tukipambana-waziri muhusika na sekta ajiuzuru!!

Bado-itatokea siku trela lililoshehena mizigo au tanker la mafuta litakosea njia au kukwepa ajali na kukanyaga waliotandaza biashara barabarani na sio tu kutoa fundisho na ukiukaji sheria/kanunu za biashara bali kutia vilema ambavyo vitatufanya kujuta maisha. Wakati umefika tubadilike ktk masuala ya vyombo vya moto kila mmoja azingatie sheria. tubadilike pia katika matendo yetu ktk makazi kwani tunajiongezea maradhi-kubabanisha nyumba na kuziba mapito; kuweka shughuli za mbao, welding, garage ambazo zinaingiza hewa za vumbi na chuma na kemikali za rangi hapo tulipo ktk viosk vya biashara mbanano na nyumba mbanano tunamoishi na watoto; bado moshi mweusi wenye risasi (lead) utokao ktk magari yapitayo barabarani. samaki zilizowazi na vyakula vingine-ngisi, nyamachoma zinazoingia risasi na mavumbi tunavyo barabarani. Bado hayo maji na nyama, maziwa na samaki tulao wenye accumulation ya mercury na kemikali nyingine yaingiayo toka uchimbaji dhahabu, uogeshaji mifugo na uoshaji magari mtoni na utupaji maji machafu ya hospitali, zahanati, viwanda mtoni-ziwani. Kwa nini hatuwezi kuwa kama nchi za wenzetu Ulaya wakati sheria husika zipo, sera na mikakati na tunaona tunavyoumia kwa kutokuzingatia hayo?

Heri ya mwaka mpya. Ila, ninaomba mvua za mafuriko DSM zizidi kuja tuzidi kuelea mabondeni ili tuzidi kupata fundisho zaidi labda tutabadilika sisi kwenye kaya sio Waziri wa mazingira pekee..


 



On Tuesday, 24 December 2013, 18:11, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Kuna ajali imetokea maeneo ya igurusi , mbeya na kusababisha vifo vya watu 5 .

Ni Gari ya mizigo imegongana na nyingine ndogo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment