Friday 4 October 2013

[wanabidii] Wizara inahitaji maoni yako ya kuboresha Mitaala ifuatayo ya Elimu

Mitaala ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu imewekwa katika tovuti ya Wizara.

Mitaala hii ni ile iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2005 ambayo ilizingatia ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana badala ya ule wa awali unaozingatia maarifa. Mitaala hii imekuwa ikitumika kwa 
kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa.

Mitaala imeboreshwa kufuatia mchakato wa majadiliano katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyofanyika mwezi Februari 2013, pamoja na maoni na hoja mbalimbali zilizotoka kwa wadau wa elimu. 

Pamoja na maboresho yaliyofanyika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweka mitaala hii wazi kwa wadau wote wa  elimu na jamii kwa ujumla ili kuendelea kupata maoni zaidi ya jinsi na namna ya kuiboresha mitaala hiyo. 

Aidha, katika kipindi hiki cha kukusanya maoni, mitaala hii itaendelea kutumika hadi hapo mchakato wa kuihuisha utakapokuwa umekamilika. 

  1.  MTAALA WA ELIMU YA AWALI (90.51 kB)
  2.  MTAALA WA ELIMU YA MSINGI (129.81 kB)
  3.  CURRICULUM FOR ORDINARY LEVEL SECONDARY EDUCATION (184.15 kB)
  4.  CURRICULUM FOR ADVANCED SECONDARY EDUCATION (240.27 kB)
  5.  CURRICULUM FOR CERTIFICATE IN TEACHER EDUCATION (332.33 kB)
  6.  CURRICULUM FOR DIPLOMA IN TEACHER EDUCATION (192.09 kB)

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment