Tuesday 29 October 2013

Re: [wanabidii] Historia ya Tanganyika kabla ya miaka ya 1900s

Haswa, maana nkama ni mlima-ndiko wakiabudu, kama ni ziwa victoria-ndiko wakivua samaki na kulitegemea katika maisha yao. Vivyo hivyo bahari-watu wa Iringa walifika Kisiju wakavuka kufika Mkuranga na Rufiji wakiufuatia Mto Rufiji unaishia wapi mpaka baharini pori kwa pori. wakatembea mwambao wa pwani wakaona bahari inashangaza. wakafika kisiwa kimoja kiitwacho-Koma karibu na Kisiju lakini ni cha Mafia. Huko Mtoto mmoja wa Sultan wa Kilwa kisiwani aliwekwa alikuwa na Ukoma. walimtenga na kumpelekea chakula kwa vyombo vyao vya baharini. wale wa Iringa walifika maji kupwa wakamkuta binti wakamwambia tutakuletea dawa mwezi ukiwa pale juu. wakarudi na dawa-akapona. Walipomletea chakula kutoka Kilwa Kisiwani wakamkuta kapona wakashangaa na kuahidi kurudi kuwaona hao jamaa wakija tena kama walivyoahidi. wakakutana nao-mfalme akasema 'Ruksa' ondokeni naye mkamuoe ninyi mmemponya. Chief Ngwira wa watemekwira alipewa mke na mwarabu. katika wake mwarabu aliyekuwa anaiba meno ya tembo Ruaha, Mikumi, Kilombero mmojawapo alichoka sana alikuwa mgonjwa hamu ya kuongozana na mume ikamuishia. Kubekwa ilishindikana-hivyo akafika kwa Ngwira na kumpa huyo nmke abaki naye akitaka awe mtumwa wake au mkewe. Wakamtibia kienyeji kisha akamuoa akawa mke mmojawapo. Huko nako kunakoo zenye nywele za kiburushi na watu weupe. Usishangae katika vikabila vingine mbali kusikofikika kwa urahisi ukakuta machotara. kufuatia mto Ruvu, Rufiji, Ruaha unaishia wapi, bahari hii inapita maeneo gani kuliteta wageni mbali mbali kama hao waliokuwa wakizunguka dunia na kupeleleza mito, milima n.k. Ila, wao hawakuandika, hawakujulikana, walipopapenda wakahamia, wakakaa ikawa himaya yao. Na ndivyo makabila yalivyokuja yakikimbia vita, ukame na njaa au maradi. wakagundua eneo, mito ya kuyapa majina. Na hata aliyewahi kuzunguka dunia kuliona bara la Marekani na kufika mapori hadi australia sio Vasco Da Gama-hawamtaji tu-kitabu kimeandikwa hakijulikani ni Msenegali kutoka Senegal.

Uchunguzi kwa kwenda bara hadi bara uliwapeleka kwa vyombo vya bahari na kwa miguu waswahili kutoka west africa bara la ulaya na marekani wakati huo dunia zimeungana na wamepakaza virangi vyao huko unamkuta mtu mchanganyiko nwele wa kisiwa fulani na mapua ya kiswahili. Huo utumwa umekuja baadae tu na kupeleka watu huko. Nasi watu wa bara hili tuligundua kwao hawatutaji tu. tuliwauzia mpaka madini ya maana ambayo wao waliyataka sisi huku ilikuwa ni hela ya kubadilishana au vito vya kumpa chief mapambo yake. hayo madini na hela za mwarabu akipita akilipa kwa Chief Ngwira wajerumani walipoingia himaya ya Ngwira wakakuta yamejaa makasiki wakachukua yote wakamwita jina la 'Bwana Fedha'. wakaondoka na mapambo yake kumbe ni hela kwao!!



On Tuesday, 29 October 2013, 22:00, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
Hao wazungu wanaojidai kuvumbua, walivumbulia wazungu wenzao may be,
but for us we knew it kabla yao.

--
*"Anyone who conducts an argument by appealing to authority is not using
his intelligence; he is just using his memory." Leonardo daa Vinci
*

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment