Thursday 10 October 2013

[wanabidii] Re: Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Hii maana yake nini? Nimesoma habari hii mtu huyu anasema siku Mbunge wake akihitaji kuongee na wazee wa eneo hilo yeye ata kuwa wapi! Ni mawazo mfu haya, inamaana kuliko na wabunge wa CCM hakuna viongozi/labda tuachilie mbali swala la viongozi niseme wanachama wa CCM?
Bwana Mngula, asijione kuwa kiongozi wa chama chake amebadilika na kuwa siyo raia wa Tanzania, kukuwa na kikao cha wazee wa eneo akipenda kuhudhuria aende kama raia wengine wasio na vyeo, mkuu wa kikao siku hiyo kwa akili ya kawaida ni huyo mbunge wake.
Za nini kauli za kiuhasama? Siyo lazima kumtoa ubunge safari ijayo, ni kupiga kampeni za haki huku mkitoa ahadi zinazotekelezeka kwa kipindi kinachoahidiwa. Hakuna nguvu wala lugha ya nguvu kwenye kunyang'anya mtu ubunge, ni uzuri wa muwakilishi na uadilifu na wala siyo kutumia nafasi za uongozi mlizo nazo.

0 comments:

Post a Comment