Friday 25 October 2013

[wanabidii] Mtanzania kuweka historia Kenya

Mlinda mlango wa zamani wa Taifa Stars aliyeibukia Prisons na baadaye Yanga, Ivo Mapunda, siku chache zijazo atakuwa golikipa wa kwanza Mtanzania kutwaa ubingwa wa Kenya akiwa mlinda mlango wa kwanza wa timu yake. Ivo anaidakia Gor Mahia ambayo inahitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa huku ikiwa na michezo minne kibindoni. 

Hakuna kipa wa nchi yeyote ya CECAFA aliyewahi kufanya hivyo ugenini zaidi ya Idi Pazi wa Simba ambaye aliwahi kuwadakia mabingwa wa Sudan, El Hilal, kwenye miaka ya 1980 mwanzoni. 

Nyota ya Ivo ilififia wakati akiwa Stars kutokana na nuksi ya kipa wa Simba, Juma Kaseja, kunyanyaswa na kocha wa Stars aliyekuwa mnazi wa jezi za njano, Marcio Maximo. Aidha kuichezea Yanga kulimletea mkosi mwingine na kujikuta akikimbilia nje ya nchi hadi alipotua Gor Mahia.

Kila la heri Ivo Mapunda.

Matinyi (Simba damu).


From my Android phone on T-Mobile. The first nationwide 4G network.

0 comments:

Post a Comment