Friday 4 October 2013

Re: [wanabidii] Tamko la Jukwaa la Wahariri kuhusu kufungiwa kwa magazeti ya Mwananchi na Mtanzania

ajabu hawakulaani kufungiwa kwa Redio Iman na ile redio ya mwanza ya
nimeiosahau jina sijui walisahau,

On 10/4/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
> Kikao cha Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri kilichofanyika leo, Alhamisi,
> Oktoba 3, mwaka 2013, kimejadili uamuzi wa serikali kuyafungia magazeti ya
> Mwananchi na Mtanzania.
>
> Wajumbe wa kikao hicho wamesikitishwa kwa hatua zilizochukuliwa na serikali
>
> dhidi ya magazeti hayo. Baada ya mjadala wa kina, wajumbe wa Jukwaa
> wameazimia yafuatayo.
>
>
> *1. Kupinga uamuzi wa serikali:*
>
> Jukwaa linapinga hatua hiyo dhidi ya magazeti hayo kwa sababu adhabu hiyo
> imetolewa kwa kutumia sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo
> imekuwa ikilalamikiwa na wadau kwa miaka mingi sasa.
>
> Hii ni moja ya sheria ambazo Tume ya Jaji Francis Nyalali ilipendekeza
> ifutwe kwa sababu mbalimbali ikiwamo kukiuka misingi ya haki za binadamu,
> utawala bora na kwenda kinyume cha Katiba ya nchi pamoja na maazimio ya
> kimataifa ya haki za binadamu.
>
> Hivyo, tunaungana na taasisi nyingine kupinga adhabu hii kwa magazeti ya
> Mwananchi, Mtanzania na wakati huo huo tukikumbushia kifungo cha gazeti la
> Mwanahalisi kwa sababu sheria iliyotumika haifai.
>
>
> *2. Tunalaani kufungiwa kwa magazeti hayo:*
>
> Utaratibu uliotumiwa na serikali kwa kujigeuza kuwa mlalamikaji, mwendesha
> mashitaka na mtoa adhabu kamwe haukubaliki katika jamii yoyote
> iliyostaarabika kwa sababu ni kinyume cha utaratibu wa kutoa haki ya asili
> (natural justice). Hili si jambo la kuendelea kufumbiwa macho na jamii
> ambayo inafuata misingi ya Kidemokrasia na utawala bora.
>
> Hivyo, tunalaani kwa nguvu hatua hizi zilizochukuliwa kwa kukiuka misingi
> hii yote, hasa ukizingatia kuwa ni serikali hii ambayo imesaini makubaliano
>
> ya kimataifa kuhusu uwazi katika uendeshaji wa serikali (open government
> initiative).
>
>
> *Nini kifanyike:*
>
> Tunafahamu kuwa kuna kesi ya kuipinga sheria ya Magazeti ya mwaka 1976
> ambayo ilifunguliwa mwaka 2009. Ni jambo la bahati mbaya na kusikitisha
> sana kuwa hadi hivi sasa, miaka minne baadaye, bado kesi hiyo haijaanza
> kusikilizwa kwa sababu haijapangiwa majaji.
>
> Jukwaa la Wahariri linapenda kutoa mwito kwa Mhimili wa Mahakama
> kurekebisha kasoro hii kwa kupanga majaji kwa ajili ya kuisikiliza.
>
> Kufanya hivi kutahakikisha si tu haki kutendeka, bali pia haki kuonekana
> inatendeka. Kuchelewesha haki ni sawa na kunyima haki.
>
> Tunasikitika zaidi kwamba serikali inaendelea kutumia sheria hii kandamizi
> huku ikiwa imeikalia kwa miaka mingi sasa miswada ya sheria mbili muhimu
> zinazohusu haki za habari bila ya kuziwasilisha bungeni. Kwa hiyo tunaitaka
>
> serikali kuwasilisha miswada hiyo bungeni ili kupatikana kwa sheria mpya ya
>
> kusimamia tasnia ya habari nchini.
>
>
> *Hitimisho:*
>
> Hivyo basi, tunatoa mwito kwa serikali kuyafungulia magazeti hayo.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment