Tuesday 15 October 2013

Re: [wanabidii] BARUA YA WAZI KWA WALIMU



On Friday, October 11, 2013 4:42 PM, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
Umetumia muda wako mwingi kutoa pendekezo lisilo na kichwa wala miguu. Ni kama unaiagiza serikali iivunje cwt. Serikali inayogombana na cwt kwa kutotimiza matakwa ya walimu. Hiyo ndiyo ichukue raslimali za cwt kuwagawia walimu. Sio bure .....

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "wanazuoni@yahoogroups.com" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Thursday, October 10, 2013 12:27:30 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] BARUA YA WAZI KWA WALIMU

CHAMA CHA WALIMU KIFUTWE!Ningependa
kuona Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kinafutiliwa mbali kabisa kwani
kimeshindwa kuondoa ama kupunguza matatizo yanayowakabili walimu. Chama hiki
kimeshindwa kutetea maslahi ya walimu na kimeonyesha udhaifu mkubwa katika
ufuatiliaji wa madai mbalimbali ya wanachama wake. Baadhi ya madai haya ni
posho ya kufundishia ktk mazingira magumu, kupandishwa madaraja, malimbikizo ya
posho mbalimbali na nyongeza ya mishahara.

Kwa jinsi hali inavyojionyesha, ni vigumu sana hiki chama cha sasa kuwatetea
walimu ipasavyo. Wakuu wa CWT (Gratian Mukoba, Ezekiel Olucho na wengine)
wanaofaidi matunda ya michango ya walimu katika chama, wameshindwa kabisa
kuwasemea walimu dhidi ya ukandamizaji wa serikali wa muda mrefu. Kwanza
nashangaa kwanini hawa viongozi wapo madarakani kwa muda mrefu hivi! Michango
ya walimu kwa CWT imetumika kuwekeza vitega uchumi mbali mbali, kama vile Mwalimu
House, ambapo matunda yake hayamnufaishi mwalimu isipokuwa mchwa wachache
wanaojiita viongozi wa CWT.

Walimu hukatwa jumla ya mabilioni ya shilingi kila mwezi kutoka kwenye
mishahara yao na pesa zote hizi hutumika kutunisha vitambi vya viongozi wa
walimu huku walimu wakifa njaa bila sababu ya msingi. Wala matumizi ya michango
ya uanachama hayajawahi kukaguliwa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) ili kuona jinsi gani michango ya walimu inavyotumika na kama
walimu wananufaika na pesa hizo au fedha inayotokana na uwekezaji wa fedha
hizo. Ingekuwa jambo la msingi endapo michango hii ingewarejea walimu kupitia
SACCOS au namna nyingine ambayo ingewanufaisha walimu kuliko kubunguliwa na
bungu wachache kwa maslahi yao binafsi. Hatuwezi kuwa na chama kimoja kikubwa
kabisa lakini ambacho hakina tija kwa wanachama wake.

Kwa kuwa chama hiki kimeshindwa kuleta tija kwa walimu, napendekeza kivunjwe kabisa
na kusahaulika katika ardhi ya Tanzania.
Chama hiki kivunjiliwe mbali ili kila mwalimu ashughulikie matatizo mwenyewe
badala ya kuendelea kuwakamua walimu michango ya chama ambacho hakiwezi
kuwatetea. Baada ya kuvunjwa, mali zake ziuzwe na pesa zitakazopatikana
zigawanywe kwa walimu kulingana na muda wa mwalimu kazini na kiasi alichokuwa
akichangia kwa mwezi.

Kufanya hivyo kutawapunguzia walimu wingi wa matatizo yanayowakabili kwani
inaonekana kwamba hata chama chenyewe ni mzigo kwa walimu. Ndiyo. Kiasi cha michango
kinachokatwa kutoka kwenye mishahara ya walimu kinatosha kabisa kupunguza
umasikini wa kipato unaowakabili walimu endapo CWT itavunjwa na hivyo makato ya
wanachama kusitishwa.

Lakini, kama nilivyodokeza hapo awali, adui wa walimu ni walimu wenyewe. Wengi
wao wana uelewa mdogo wa mambo, hivyo CWT imekuwa ikitumia udhaifu huo
kuwakandamiza walimu kwa muda mrefu sasa. Na serikali nayo, kwa upande
mwingine, imekuwa ikitumia mwanya huo huo kugoma kuwaboreshea walimu mishahara,
kuwapandisha madaraja au kuwalipa posho mbalimbali wanazostahili. Kwa mtaji
huu, walimu watazidi kukandamizwa hadi pale watakapojitambua, kumjua adui yao
wa kweli na kuchukua jitihada za kupambana naye hadi kumtokomeza.

Nategemea kwamba walimu mtaamuka kutoka usingizi wa pono mliolala na kuanza
kushughulikia matatizo yenu kwa njia nyingine badala ya kuendelea kukitegemea
Chama Cha Walimu ambacho kimeshindwa kushughulikia matatizo yenu ipasavyo.
Inavyoelekea ni kwamba viongozi wa chama chenu ama wameamua kuwasaliti kwa
kushirikiana na serikali kuwakandamiza au hawana uwezo wa kutosha kuikabili
serikali iweze kuwatatulia matatizo lukuki yanayowakabili na ambayo yamekuwa
yakichangia kushuka kwa ubora wa elimu. Na ni bahati mbaya kushuka kwa kiwango
cha elimu hakiwaathiri watoto wa vigogo ambao husoma kwenye shule za
binafsi zilizo walimu wa kutosha na bora, mazingira mazuri ya kujifunzia na
vifaa kufundishia vya kutosha. Watoto wanaotabika katika shule hizi mbovu za
serikali ni wale wa walalahoi ambao hata kula kwao ni kwa shida na taabu na
ambao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule binafsi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment