Saturday 9 September 2017

[wanabidii] Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii

[caption id="attachment_81542" align="alignnone" width="500"]<img src="http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2017/09/10022017/IMG_9114-500x308.jpg" alt="" width="500" height="308" class="size-medium wp-image-81542" />  Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu.[/caption]

[caption id="attachment_81541" align="alignnone" width="500"]<img src="http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2017/09/10022012/IMG_9092-500x300.jpg" alt="" width="500" height="300" class="size-medium wp-image-81541" /> Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.[/caption]

<strong>Na Mwandishi Wetu, Dodoma</strong>

<strong>MTANDAO</strong> wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania.

Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.

Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.

Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku  shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.

Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.

Walishauri Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu kutenganishwa na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu.

Kilio kingine kilichofikishwa katika kamati hiyo ya Bunge ya Huduma za Jamii, ni pamoja na kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwashukuru wanachama wa TEN/MET kwa kuwa wazalendo kuipigania elimu nchini, hivyo kuwataka watoe muda kwa kamati hiyo ili iweze kuzifanyia kazi hoja hizo kwa maendeleo ya taifa.

[caption id="attachment_81543" align="alignnone" width="500"]<img src="http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2017/09/10022026/IMG_9128-500x313.jpg" alt="" width="500" height="313" class="size-medium wp-image-81543" /> Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).[/caption]

[caption id="attachment_81544" align="alignnone" width="500"]<img src="http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2017/09/10022031/IMG_9139-500x368.jpg" alt="" width="500" height="368" class="size-medium wp-image-81544" /> Afisa Programu toka HakiElimu, Makuba Mwemezi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa TEN/MET akichangia hoja katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.[/caption]

[caption id="attachment_81545" align="alignnone" width="500"]<img src="http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2017/09/10022036/IMG_9143-500x280.jpg" alt="" width="500" height="280" class="size-medium wp-image-81545" /> Kikao hicho kikiendelea jana mjini Dodoma.[/caption]

KAWAIDA:-

______Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii 

Na Joachim Mushi, Dodoma

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania.

Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.

Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.

Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku  shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.

Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.

Walishauri Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu kutenganishwa na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu.

Kilio kingine kilichofikishwa katika kamati hiyo ya Bunge ya Huduma za Jamii, ni pamoja na kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwashukuru wanachama wa TEN/MET kwa kuwa wazalendo kuipigania elimu nchini, hivyo kuwataka watoe muda kwa kamati hiyo ili iweze kuzifanyia kazi hoja hizo kwa maendeleo ya taifa.

Mwisho

MAELEZO PICHA
IMG_9114
Mwanachama wa TEN/MET na Mratibu Kitaifa wa taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu.

IMG_9128
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).

IMG_9092
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.

IMG_9139
Afisa Programu toka HakiElimu, Makuba Mwemezi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa TEN/MET akichangia hoja katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.

IMG_9145
Sehemu ya Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) wakiwa na kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma.
_____________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

1 comments:

  1. Je! Unahitaji mkopo rahisi kwa kuridhika kwako? Tunatoa mkopo wa kiwango cha riba 3% kwa wakopaji wa ndani na wa kimataifa. Tumethibitishwa, tunaaminika, tunaaminika, bora, haraka na nguvu na tunashirikiana. Tunatoa mkopo wa muda mrefu kwa kiwango cha juu cha miaka 2 hadi 50.

    Je! Unahitaji mkopo wa moja kwa moja, rahisi na wa bei nafuu kulipa deni lako, kuanzisha biashara au kwa sababu nyingine? Ikiwa ni hivyo, tafadhali wasiliana nasi kwa mkopo.

    Ofa hii ni ya watu wakubwa.

    Ikiwa una nia, tafadhali wasiliana nasi kupitia: Barua pepe: fredmorefinance@gmail.com
    fredmorefinance@hotmail.com
    WhatsApp: +2348071917956 +919654763221

    Tumethibitishwa,
    ya kuaminika, yenye ufanisi, ya haraka na ya nguvu.

    Kwa dhati,
    Fred zaidi
    fredmorefinance@gmail.com

    ReplyDelete