Friday 8 September 2017

[wanabidii] MADHARA YA VIPODOZI VYA KEMIKALI YAWATISHA WAKULIMA

mMADHARA YA VIPODOZI VYA KEMIKALI YAWATISHA WAKULIMA


MATUMIZI ya vipodozi vyenye kemikali ya sumu yamewatisha wakulima katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Hofu hiyo ilitanda jana baada ya Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare, Euphrasia Shayo kuwasilisha mada yake kwa kundi hilo la wakulima wanaoshiriki tamasha la jinsia kutoka maeneo anuai.

Alisema kemikali za sumu kama zebaki na mericuri zilizomo katika vipodozi na mikorogo isiyo rasmi inayotumiwa hasa na akinamama kujichubua na kubadili nyele zao zina madhara makubwa katika kilimo.

Alisema kemikali hizo mbali na kukaa ardhini kwa muda mrefu zaidi zikiharibu mazao pia vinamadhara makubwa kwenye miili yao, hivyo kuwashauri kuachana navyo mara moja kwa watumiaji.

Alisema kemikali hizo mara baada ya kutumiwa hutelekezwa ardhini na mara mvua zinyeshapo husafirishwa hadi katika vyanzo mbalimbali vya maji hivyo kujikuta vikitumiwa tena na jamii jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na mifugo.

"…Vinamadhara makubwa katika miili yetu, ndio maana sasa hivi magonjwa ya ajabu ajabu ikiwemo kansa vimeendelea kushamiri kwetu, vinginea husababishwa na kemikali hizi zenye sumu. Wapo akinamama wameathiriwa vibaya sana na kemikali hizi zenye sumu," alisema Bi. Euphrasia Shayo.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wakishiriki katika mjadala waliiomba Serikali kuwatumia wataalamu kama Bi. Euphrasia Shayo kutoa elimu ya madhara kwenye redio na luninga ili kila mmoja aelewe madhara ya vipodozi hivyo.

Haya hivyo waliiomba kuendeleza oparesheni la kuwakamata na kuwachukulia hatua kali waingizaji wa vipodozi vyenye viambata vya sumu ili kupunguza madhara kwa jamii.



MAELEZO YA PICHA:-

IMG_8548

Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.


IMG_8650, IMG_8646

Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare, Euphrasia Shayo (kulia) akiwasilisha mada yake juu ya madhara ya kemikali za vipodozi na mkorogo kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. 


IMG_8623

Sehemu ya washiriki katika semina hiyo.

 

IMG_8623

Sehemu ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 wakifuatilia mada anuai toka kwa wawasilishaji. 


IMG_8636

Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo akiuliza swali mara baada ya uwasilishaji.



--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment