Dr Williamson akiwa "Sorting Room" na lundo la almasi
Mtambo wa Kuzalisha umeme mgodi wa Mwadui -1950's
Mwalimu wa Shule Ya Msingi Mwadui aliyeletwa na Dr Williamson
Gazeti la Australia mwaka 1952 likielezea ukubwa wa bwawa la Songwa Mwadui lililokuwa bwawa kubwa la kutengenezwa(Artificial Dam) duniani
Meli iliyotumiwa na Wafanyakazi wa Serikali ya Kikoloni,kutoka Londo kuja East Africa,wakati wale wa Mwadui walitumia ndege
Uwanja wa Ndege Mwadui uliojengwa miaka 1940's wakati
Mbwa wa Mwadui,waliokuwa na mafunzo hodari ya kutumwa dukani na kupeleka barua maofisini.
Band ya Jeshi la Polisi Mwadui ilianzishwa mwaka 1949
Ujio wa Princess Mwadui akiambatana na Gavana Twinning
Club inayoelea katika bwawa la Songwa Mwadui,sehemu pekee ya Starehe ambayo hata Gavana wa Tanganyika alifika kujivinjari.
Hii biashara ya madini toka enzi na enzi imekuwa ni "vita",tena ni vile vita ambayo havijawahi kumuacha mtu "salama".Iwe ni mfanyabiashara au mwanasiasa anayetazama maslahi ya watu wake kuliko yale ya mabepari wanunuzi wa madini husika.
Vita hii ilimkumba Dr John Williamson,mwanajolojia Mcanada mwanzilishi na mmiliki wa mgodi wa Mwadui,vita hivi vilimsumbua Julius Nyerere,mwana wa Afrika na Rais wa Tanzania.Mapambano haya hayakuziacha salama nchi zenye ukwasi wa madini kama DR Congo,Angola na Siera Leone.
Report ya pili ya Kamati ya Rais juu ya maboso(mchanga wa madini)inaenda kufungua ukurasa mpya wa "vita" ya moja kwa moja kati ya Rais wa Tanzania yeye binafsi dhidi ya wafanyabiashara wakubwa wa madini duniani.Tumuunge mkono Rais,kwa kumuelekeza vizuri na kwa staha pale anapokosea,na pia kwa kumpongeza kwa kiasi pale anapopatia mikakati katika mapambano haya.Tunaenda kuanza "vita" rasmi na "wamiliki" wa madini wa dunia,tusikate tamaa...Aluta Continua!!!
Biashara ya madini duniani,imekamatwa na familia MBILI tu za Kiyahudi.Moja ikijielekeza kwenye madini ya dhahabu (na jamii zake) ambao ndio BARRICK na moja katika madini ya almasi ambao ndio DE BEERS.Hawa ndio "wamiliki" wa madini yote ya dunia,bila kujali mipaka ya nchi walipo na kule yalipo madini.
Familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer (waliohamia South Africa) wenye kampuni ya "De Beers Group of Co.",ndiyo "imejimilikisha" madini yote ya almasi yaliyopo katika dunia hii baada ya "kumpoka kwa nguvu" umiliki wa kampuni Cecil Rhodes.Kuanzia madini ya India na Brazil,Afrika Kusini na Angola,Siera Leone na Botswana,Mwadui Shinyanga hadi Siberia ni "mali" ya De Beers.
Mwaka 1940,Dr John Williamson alifungua mgodi wa almasi Mwadui,nje kidogo ya mji wa Shinyanga.Mwadui ilikuwa na mkanda wa "kimberlait" wenye hifadhi nyingi ya almasi.Dr Williamson raia wa Canada,akautengeneza mji mdogo wa Mwadui na kuwa moja kati ya miji bora sana kusini mwa jangwa la Sahara (Mwadui Township).
Kufikia mwaka 1947,Dr Williamson alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi,hospital ya kisasa,shule za msingi tatu,mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika.Akajenga chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya mgodi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi,chuo cha kilimo na shule ya upili.Huko kwao waliita "School Near The Equator".Ilikuwa shule bora na ya kisasa.
.
Dr Williamson akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1940's,akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya Dakota DC 3 na Cessna180 wakati huo hata serikali ya Kikoloni ya Muingereza ikiwa haina wazo la ndege,wakati serikali ya Tanganyika ikiwa haina uhakika wa uwanja wa ndege kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC4,Dr Williamson alikuwa tayari na uwanja huo,ambapo wageni toka London Uingereza,ndege zilitua Malta,Khartoum-Sudani na baadae Nairobi (Wakati huo ukiitwa Embakasi Airport),na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa moja mpaka Mwadui Shinyanga,ambapo Serikali ya Kikoloni ilikuwa na afisa mmoja wa uhamiaji. Dr Williamson alijenga kanisa na msikiti bora na wa kisasa kwa ajili ya wafanyakazi wake.
Wakati huo,usafiri pekee wa watumishi wa serikali ya Kikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya "The Braimer Castro" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa.Yeye Dr Williamson na wafanyakazi alioajili walikuwa wanapanda ndege kupitia Embakazi na baadae Mwadui.
Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata jiji la Dar es Salaam achilia mbali mkoa wa Shinyanga.Wakati huo umeme wa Dsm ulikuwa unategemea ule mtambo ulioweka pale makao makuu ya Wizara ya Nishati kama makumbusho.
Ndani ya mgodi wa Mwadui,Dr Williamson alijenga "Sailing Club",yaani Club inayoelea katika bwawa alilichimba eneo la Songwa.Hii ndio ilikuwa Club pekee inayoelea Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara.
May 2,1952,Gazeti Kongwe la "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya uwepo wa bwawa la Songwa,Mwadui-Shinyanga,Tanganyika.Gazeti hilo la Australia lilielezea bwawa la Songwa kama moja kati ya "Artificial dam" kubwa zaidi duniani,lenye uwezo wa kuchukua "two thousands million gallons of water".Mradi ambao hata serikali ya mkoloni iliushangaa.
Mwadui kulikuwa na mfumo wa maji safi na maji taka yaliyotibiwa na wataalamu waliosomeshwa na mgodi.Huduma ya elimu ya watu wazima na elimu ya uchumi wa nyumbani "home economics" kwa wamama waliokuwa nyumbani.Kufikia mwaka 1970,karibu 97% ya wakazi wa mgodi huo ambao walifikia 60,000 walikuwa wanajua kusoma na kuandika,na wamama wakiwa na ujuzi wa ushonaji,upishi nk.
Dr Williamson aliajiri mpishi maarufu toka Ufaransa,ambaye alikuwa akipika na kuandaa chakula katika "mesi" kubwa ndani ya mgodi wa Mwadui.Mfaransa huyo alifundisha wapishi wengi wa Kiafrika na alikuwa kama "chuo" cha wapishi wengi wa maafisa wa serikali ya kikoloni,na hata wapishi wa mwanzo wa Ikulu ya Dsm baada ya Uhuru,walipita katika mafunzo ya "mesi" ya Mwadui.Kufikia mwaka 1950,Tanganyika ilikuwa na vyumba viwili tu vyenye hadhi ya kulala familia ya kifalme ya Uingereza,chumba kimoja katika Ikulu ya sasa ya Dsm na kingine kwenye "rest house" ndani ya mgodi wa Mwadui.
Mgodi wa Mwadui chini ya Dr Williamson,uliweza kujenga kiwanja cha golf chenye mashimo tisa,ambacho kilikuwa ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa Afrika nzima.Mwaka 1952,Dr alishawishi mpaka mashindano makubwa ya kombe la Malikia la Golf nchini Canada yafanyike Mwadui,kila kitu kilikubalika isipokuwa hali ya uwanja wa Embakasi Kenya haukuwa sawa sababu ya vuguvugu la vita vya Maumau lililotishia usalama wa kiwanja.Swimming Pool za viwango vya Olympic tatu ndani ya mgodi
Viwanja vya tennis,pamoja na viwanja vitatu bora vya mpira wa miguu vilivyokuwa na viwango vya kimataifa vilijengwa ndani ya mgodi wa Williamson.Timu ya mpira ya Mwadui Mining ilishiriki mashindano ya kitaifa kwa ubora mkubwa.Waamuzi wakongwe wa viwango vya kimataifa kama Mshangama na Mashishanga(RC wa zamani) ni matunda ya Dr Williamson.
Ustawi wa maisha ya mgodi na kushamiri kwa faida ya Dr Williamson kuliwauzi "wamiliki" wakubwa wa biashara ya madini ya almasi ambao ni De Beers Group of Co.Almasi ya Mwadui iliingia kwa kasi sana katika soko la dunia jijini London.De Beers wakashindwa kumdhibiti Dr Williamson na almasi yake,akafanya almasi ya Afrika Kusini kushuka thamani katika soko la dunia,njia pekee iliyobaki kwa De Beers ilikuwa kumtaka Dr Willy aungane nao katika biashara.
Dr Willy alikataa,akataka kuupeleka mgodi kwa namna yake,hakutaka kuwanyonya Waafrika na wafanyakazi wake,ndoto zake ilikuwa ni kuijenga "Quebec ndogo ndani ya Tanganyika",alitaka kuonyesha tofauti ya thamani ya madini na maisha ya wazawa kwa kuutumia mgodi wa Mwadui.Aliiishi Afrika Kusini na kuona jinsi wazawa wa kando ya migodi na wafanyakazi wasivyofaidika na madini katika ardhi yao.
Dr Willy hakutaka hali hiyo itokee.Mkoloni na De Beers walichukia uamuzi wa Dr Williamson kuufanya mgodi wa Mwadui kama "Ulaya ya Afrika".Walim-fustrate kwa kukataa kuipokea almasi yake katika viwanda vya wachonga almasi kule London (diamond Cutting).Mwaka 1950,Serikali ya kikoloni kwa Shinikizo la familia ya Oppenheimer wakataka kuutaifisha mgodi wa Mwadui ili uwe mali ya serikali ya mkoloni na si mtu binafsi.
Hali hii ilichanganya sana Dr Williamson,akawa mlevi wa kupindukia wa whisky ya Scotland,akawa "chain Smoker" na kwa sababu alikuwa "bachelor" hakuwa na mtu wa kumtuliza mawazo.Mwaka 1952,mwezi Machi, kampuni ya De Beers ilimtuma mtoto wa kwanza wa mmiliki wa kampuni,Herry Oppenheimer kuongea na Dr Williamson namna ya kuuza sehemu ya hisa kwa De Beers ili aweze kuwa "salama",Dr Williamson alisitasita sana,akawaza jinsi wafanyakazi wake wa kiafrika na wale aliowaleta toka Ulaya watakavyonyanyasika,akawaza jinsi ndoto yake ya kujenga "Mji wa Quebec wa Afrika" inavyopotea.
Mwaka 1956...Princess Margareth akiambatana na Gavana wa Tanganyika na ujumbe wake walitembelea mgodi wa Mwadui wakiwa ndani ya ndege aina ya Dakota DC4 mali ya Dr Williamson.Ulikuwa ni ushawishi kumfanya Dr aachie sehemu ya hisa za mgodi
Kwa shingo upande akatoa 50% yake kwa kuwauzia De Beers kwa £ 4 milioni,miaka michache baadae akagundulika kuwa na saratani ya koo, ugonjwa uliochukua maisha yake miaka michache baadae(japo ilisimekana ulipandikizwa ili kumuondoa).Aliomba kuzikwa ndani ya eneo la Mwadui kwani kwake Mwadui ndio ilikuwa nyumbani.
Mwaka 1958,Herry Oppenheimer ndio akawa mwenyekiti wa Mgodi wa Mwadui,sehemu ya hisa za Dr Williamson aliachiwa dada yake,na kwa sababu hakuwa na uzoefu wa mambo ya madini,De Beers wakamshauri aziuze.De Beers na serikali ya kikoloni wakawa na 50/50 ya umiliki wa mgodi na almasi yote ya Mwadui.Ndoto za De Beers na familia ya Oppenheimer ikawa imetimia....Nayo ni "KUMILIKI MADINI YOTE YA ALMASI CHINI YA ARDHI YA DUNIA
Julius Nyerere alipochukua nchi 1961,baadae aliamua kutaifisha mali zote,akaunda Stamico isimamie sekta ya madini.De Beers iliwauma sana kufurushwa na Nyerere.Hawa Waisrael wakaunda team ya namna ya kumkomesha Julius Nyerere,kwanza waliweka fitna katika soko la almasi pale London,wakazishawishi "Diamond Cutting and Polishing Companies" kule London ziisusie almasi ya Mwadui,Mwalimu akawa mbishi na kuimarisha "TunCut Diamond Co" pale Iringa.
De Beers akazidi kuweka fitna kwenye viwanda vinavyotengeneza vipuri vya mitambo iliyopo Mwadui.Kuanzia mitambo ya kuchimba,kusafisha na kuchambua almasi.Mwishowe vifaa vikachakaa bila kuwa na ukarabati.Uzalishaji ukapungua na almasi ya Mwadui ikapotea katika soko la dunia.Wataalamu toka nje waliokuwa katika mgodi wa Mwadui wakaondoka.Ikawa ni hasara juu ya hasara.
Mwaka 1993,De Beers kupitia Herry Oppenheimer yuleyule wa enzi za Dr Williamson walirudi Tanzania kupitia mtoto wao Nicolaus
Oppenheimer,wakaishawishi serikali ya Tanzania,na hatimaye De Beers Group of Co. wakauziwa 75% ya hisa za mgodi wa Mwadui.Hatimaye ile ndoto yao ya kumiliki madini yote ya almasi ya dunia ikaendelea kutimia.
Hawa ndio De Beers,familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer.Wanaosadiki kuwa almasi yote inayopatikana katika uso wa dunia hii ni mali yao.Walimsurubu Dr John T. Williamson,mzungu-msukuma aliyetaka mali ya ardhi ya Mwadui ilete thamani kwa Waafrika na Tanganyika.Hawa ndio De Beers waliomtikisa Mwalimu Nyerere,hawa ndio familia ya almasi duniani,wanaochochea yale ya Angola ya Savimbi,Siere Leone ya Foudah Sankho na DR Congo ya M23 ili waendelee kuchota utajili wa Afrika.
Ndugu zao ni hao Barrick na familia ya Kiyahudi iliyopo Canada.Sisi tumeanza na Barrick,ama zao ama zetu...Tusikate tamaa,cha muhimu ni kujua tu "mbinu" za adui yetu.Tuliokula ugali wa unga wa manjano na uji wa bulga tunastahimili,vipi hawa watoto wa chips mayai na kuku wa boila??Kumekuchaaaa
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment