Friday, 7 July 2017

[wanabidii] SEREKALI IWACHUKULIE HATUA WANAOTANIA JUHUDI ZA KUTHIBITI MAUJI YA KIBITI

KUNA HAJA KUBWA KWA SERIKALI KUWAFANYIA KWELI WANAO DHIAKI
JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA MAUJI.

Katika Kipindi hiki kigumu cha taifa kugubikwa na matukio ya mauaji na vitendo vya kigaidi katika wilaya za Mkuranga,Kibiti na Rufiji,na vyombo vya dola na usalama vikiwa katika juhudi za kutokomeza mauaji hayo na kurejesha hali ya amani kwa raia wa wilaya hizo,kumetokea tabia za ajabu na kusikitisha sana kuwa kuna watu au wasanii wanaounga mkono mauaji hayo kwa kutengeneza maigizo yenye kuwaunga mkono magaidi au wauaji hao na kurusha hewani video clip hizo,wanaigiza na kudhiaki juhudi za vyombo vya ulinzi ,kwa kuonyesha kuwa walinzi wa amani yetu wanapopambiwa kuenda KIBITI wanaogopa. waliogiza katika video hii kama waliigiza kwa kutumwa kama wapiga debe na kampeni za wauaji au kwa kutafuta KIKI kwa kutumia sura ya mauaji ya KIBITI tunaomba serikali na vyombo vya dola iwahoji waliotengeneza video hii hili watusaidie kuelezea ujumbe ulio katika video hii,pia wasaidie kuelezea aina gani ya vipimo au mizani wanayoitumia kupima nguvu ya dola na wauaji ?
inasikatisha sana kuona Polisi inafanya juhudi lakini baadhi ya watu wanaleta ukomedi katika maafa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment