Jana baada ya taarifa za habari nimeandika hivi kwenye wall zangu kadhaa kwenye facebook:
[Waziri wa maji wa Misri amekuja tanania. Ameahidi msaada wa visima 40 vya maji kwa maeneo ya yenye matatizo ya maji. Viongozi wetu wameishukuru Misri. Mmoja kati ya watoto wangu akiwa mdogo nilikuwa nikifungulia projector wengine wanapoangalia ukutani kuona picha, yeye alikuwa anaangalia picha inakotokea. Maana yake alikuwa haoni picha maana kule inakotokea haionekani. Na mimi nataka kufanya hivyo kwa kuuliza swali "Waziri wa maji wa misri amekuja kufanya nini?".]
Baadaye nilifafanua kuwa Misri haitaki watu waguse maji ya Mto Nile na vyanzo vyake ikiwa ni pamoja na Ziwa Victoria. Iliwahi kutaka kuleta mgogoro wakati Serikali ya Mkapa inatengeneza bomba kutoka ziwa Victoria kwenda Shinyanga. Sasa kuja kwa upole na kutaka kuisaidia Tanzania visima ina nini nyuma yake?
Kama kawaida ya wabongo wakatoa maoni ambayo sitayatoa kwa undani. Wengine wakasema "mzee huyu anazeeka vibaya, sasa hii nini anatuletea hapa. Na maoni kadhaa ya namna hiyo. Lakini watu kadhaa tena walioko nje ya Tanzania wakajadili kama ifuatavyo:
# Mmoja: Mzee Elisa Muhingo, myaka hii sifikiri kwamba Misri inaweza tumia tishio la Vita ajili ya Maji.... nakumbuka Neno la Mwalimu Nyerere: Ilikuwa enzi zile, sio sasa. Kwani mgonjwa aliopo kwenye oxygen, anaweza pigana na mganga ambae anamuekea oxygen ili aishi...!
Mimi: Balinda, nani dr. nani mgonjwa? Wamisri ni wagonjwa kwa jambo moja na daktari katika jingine. Na Tanzania pia
Mwingine # Mzee Muhingo, Magonjwa hapa yanatofautiana. Ila Wamisri ajili ya maji...wako kwenye pampu la Oxygen. Chini ya Ardhi la Tanzania ingalao Lina maji. Na sikumoja visima vitakuwa vingi naku gawa Maji taifa nzima.
Mimi: Mimi naogopa kuendelea kuchimba visima. This is just depleting our preciuos underground waters. Nafikiri kuwekeza elimu ya kupunguza matumizi. Drip irigation. Kuna wakati natumia lita kumi za maji kuoga. JUZI nilitumia lita tatu with the same results. Kuna watu hawaoni tofauti kwa sababu 'tuna maji mengi'. Netanyahu alipotembelea Africa majuzi alisema Israel inaweza kutusaidia katika water management. Niliandika article nikasema huenda watu hawakuelewa. Misri ije kusaidia hapo.
Mwingine # Mzee ikiwa Wamisri, wanatumia maji vizuri, yaani kuwa na system nzuri ya water management...then inawezekana wawe waalimu wazuri kwa Tanzania, katika matumizi mazuri ya maji. Ila sasa, maji na hela ni sawa sawa. Watu wakiwa na hela na Kama hawana utaratibu mzuri wa kuifadhi hela, huwa wanazitumia kwa wingi...sawasa na maji, nchi ambazo Zina maji mengi, huwa watu wa nchi hizo, wanatumia maji mengi na yenye hawaitaji...yani waaribu liters ningi za maji. Ni kweli Mzee Muhingo: Continuing water management skills should be taught to our people.
Nafikiri, theories za Vita pia zinakaribia kwisha. Peace negotiations zimekuwa nyingi, ila zimewekwa kabatini ofisini kwa rais na diplomates. Ila sasa Maendeleo ya teknologia inaweka mambo yote Google...Peace negotiations zipo online, kwa hiyo sifikiri kwamba baada ya vita vya Siria kutakuwepo nyingine Vita Kali. Labda diplomatic war. Kwa sasa, Ni aibu kuu, kuona nchi inaingilia nyingine kivita...Tatizo la Mazingira, au Climate Change ziki ambatana na Energy sufficient, kidogo na Mafuta nafikiri itaweza leta migogoro, Kama iliotokea Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingerza ukapinga. Na sasa Kuna migogoro katika Climate Change practices...# Simon, labda Maji inaweza kuzusha diplomatic complications, upande wa Asia na Africa...
Mwingine: I disagree with you dear Jerome Sindano. Unasema after Syria hamna vita tena duniani? Kweli? Hamna inchi itakayo pigana na inchi nyingine kwa sababu yoyote ile! Inamaana wanasiasa (because it is them who decide to wage war or make peace) wamekua gafla watakatifu bila tamaa ya kupora mali za wengine, bila uchu wa madaraka...
Mimi: Ngenda Simon Natamani atusaidie bases za kufikiri baada ya Syria huenda vita isitokee. Sitaki kumsaidia lakini kitendo cha Trump kutoipika North Korea mpaka sasa kinaweza kuwa na maana aliyo nayo Sindano kuwa nchi zinaanza kupata kigugumizi kuanzisha vita.
Ngenda Simon Dear Jerome Sindano, Hosni Mubaraka amewahi kutishia Ethiopia kijeshi wakati walitaka kujenga bwawa huko Ethiopia. Mubaraka amewahi kutoa kauli ya military threat kwa yeyote atakaye subutu kuchafua Nile. I strongly believe that kwa Bahati mbaya Tanzania ikipuuza misri na inaonekana Nile imechafuka kwa ajili ya any activity by Tanzania. Misri itavamia tanzania kijeshi
Mjadala unaendelea.
Lakini kwa ufupi mjadala kwenye facebook umejadili nilichokuwa nacho kichwani wakati naandika maneno machache hapo juu. Si kila kung'aacho ni dhahabu. Lakini kama kuna uwezekano wa ushirikiano kwa faida ya nchi zote unahitaji kupaliliwa.
Pia hata kama watanzania tunaona tuna maji mengi, ipo haja ya kufikiri myaka hamsini ijayo. Tutafanikiwa kutoyaona. Huku juhudi za kulinda mazingira na kuyafufua yaliyoharibika na hatua za kutumia maji vizuri zinahitajika.
Kama lita ya maji inaweza kumwagilia nyanya ikastawi hadi mwisho, hamna haja ya kutumia debe kumwagilia. Haapo tunahimiza matumizi ya TEKE LINALOKUJA, kwa kihaya "Technology".
Elisa Muhingo
0767 187 507
0 comments:
Post a Comment