Lucas, maandamano yapo kwenye katiba na sheria. Soma vizuri Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa 1992 na regulations zake. Kama maandamano hayapo kikatiba na kisheria ina maana hata wanaondamana kumpongeza Rais au kuchangia damu au kupata pesa za mradi fulani ni wanavunja katiba/sheria za nchi.
2017-07-26 13:01 GMT+03:00 'lucas haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Sina hakika kama maandamano yapo kwenye sheria na katiba, sina hakika kama kufanya mikutano ya vyama vya siasa au kazi ya siasa ni kosa kisehria na katiba,Sina hakika kama kwenye haki na usawa ndani ya bunge, kama mtu anatoa lugha/ kashfa, matusi wakati kamera hazimoni akahukumiwa na ambaye sauti na kamera zinamuona akaacha kuhukumiwa.Mimi mwoga sana juu ya Mungu dhidi ya binadamu, ushogha ni kosa kwasababu ni kinyume na maumbile ya binadamu.Mwenyezi Mungu alipo muumba binadamu, alimtofautisha binadamu na viumbe wengine wakiwamo malaika. Hii ndiyo inapelekea malaika wanatamani wangekuwa binadamu wangetenda vizuri zaidi kwa sababu wanajua taji linalomsubiri binadamu aliyepewa zawadi ya kufikiri, utashi wa kuamua. Kama mtu anataka kuwafanya binadamu kuwa malaika, kwamba hawapaswi kuwaza kinyume na yeye huyu anaenda kinyume cha Mungu au anaenda sawasawa? ( kwa imani yako laikini hili la malaika)Hivi mtu kumwambia mkewe ya kuwa; mimi narudi nyumbani usiku na nimelewa pamoja na kunukia harufu ya wanawake wa nje una, badala ya kunisifu unalalamika. Mwenzio wajuma mumewe analala hukohuko na alalamiki zaidi humwekea maji ya kuoga!Huyu anajipima kwa wema na ustaharabu ama?Yaya ni mtu wa kundi lipi?Anasifa za kiuanamu sawa, je, anazosifa za kuwa mume?Mtu mmoja aliniambia, je, mbuzi aweza kuwa na ushahidi wa kumfanya chui asimtafune?( Wanaojaribu kuangalia maendeleo bila utu ) Baba ngida aliletea maendeleo nchi yake au hakuleta?Bokasa aliletea maendeleo nchi yake au hakuleta?Hitler aliletea maendeleo nchi yake au hakuleta?Idd Amin dada aliletea maendeleo watu wake au hakuleta?Ukilazimisha kuonyesha mheshimiwa anafanya hivi kwa hulka yake utakuwa unasema ambalo sikusema. Bwana Yesu alizoea kusema " wewe umesema ndiye"Ushahidi wangu kuwa ccm ndiyo inalazimisha vyama vifutwe au yenyewe ibebwe na polisi / serikali ninao.Fungua hotuba angalia au sikiliza wakati wa kampeni wa uchaguzi wa ndani wa ccm.Mwana diplomasia wa kuaminika, tena amepata kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, kwa Aibu kubwa alisema " kama ccm ikifanya vizuri, ikatimiza mahitaji ya wananchi, tukapambana na mafisadi. Tuna haja gani ya vyama vya upinzani?Kwa lugha hii, hata angeingia Lowasa hili angelifanya ukandamizaji kwa wapinzani( hayo ya ufisadi sina hakika).Tusimchafua Magufuli kwa hasira zetu dhidi ya wale tusiowapenda. Matokea ya haya ni hasara kwa taifa, umoja na utamaduni wetu.WakatabahuOn Tuesday, July 25, 2017, 11:33:08 PM GMT+3, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:Nakushukuru sana kwa tathmini yako.Umekosea kitu kimoja. Hukupitia reply to all kwa hiyo kuna watu umewaacha. na hao walikuwa wateja wangu katika makala haya. Ni akina Mbowe, Lisu na wengine. Sina uhakika kama samo humu lakini ungepitia huko ungewapata.Mimi sikubaliana nawe kuwa wasaidiza wa magufuli ndio wanaomchafulia.magufuli anajichafulia mwenyewe.Kuwafungia mikutano ya hadhara ilikuwa halali. Ninakumbuka ilikuwa wao walipoanza kumpinga katika mambo ambayo hawakuwa na sababu ya kupinga. bahati mbaya akaendelea kuwafungia. Kuendelea kuwafungia ni tabia yake ya kutopenda kubishiwa. Kuwafungia kwa kwanza ilikuwa kuwashikisha adabu na kuuonyesha umma kuwa huu ni wakati wa kazi. Mfano wito uliotolewa wa kutaka tuombe chakula kwa sababu ya ukame wa mwaka mmoja. Kuwakatalia na kuagiza watu watumie mvua fupi kuzalisha chakula imezaa matunda.Ni kweli kuwafungia wanasiasa wenzake kufana mikutano kunaendelea kumuumiza yeye kwa kuongeza watu wanaovionea huruma vyama hivyo. Kumbe angeviacha vikapayuka na kufa kifo asili. Ninatarajia 2018 ndiyo itakuwa kazi kuelekea 2019 na 20 myaka ya uchaguzi. lakini kwangu heri avizime vihurumiwe vipate kura za hasira na huruma ili viwepo. Kuwepo huko hakuna maana sana kama vingekuwepo kwa manufaa ya taifa kama 2007 hadi 2015. hata magufuli mwenyewe kama sio vyaama hivi CCM h\aikuwa na adabu ya kumteua mtu aliye katika "ukoo wa wafalme".Ninatamani Vyama hivi nielewe ili vijijenge kwa watu kwa kuyaangalia yanayowagusa. Ninaamini Serikali iliyoko madarakani ina makosa mengi ambauo vikiyasemea vitapata sapoti inayostahili.Mfano wafanyakazi walioachishwa kazi kwa sababu ya vyeti feki. Ulikuwa ni udhaifu wa serikali ya CCM kwa hiyo serikali ya CCM inastahili kuwapa kifuta machozi.Katiba. Hili la katiba najua Magufuli atawapiku na ataharibu maana ya UKAWA.Serikali ikipongezwa kwa kupondoa wafanya kazi hewa wanamwacha magufuli anazifanyia miradi isiyo kwenye bajeti.mambo haya na mengine yanahitaji mkakati kuyasemea na kuyaffuatilia na wananchi wakaelewa.Kuzuiwa kufanya mikutano kulitokana na kutaka wananchi wandamane kwa sababu kuna wafanyakazi wamesimamishwa kazi. Bunge limeanza kutumia kanuni zilizosahaulika.haya yaliwachafulia kiasi walipofungiwa hakuna aliyewaonea huruma. wakijielekeza katika niliyoyataja na mengine mengi watasikiwa. Hii itawasaidia angalau kuendelea kulinda wabunge wao bungeni uchaguzi ujao. hapo katika "pingili" ya 2025 wanaweza kujaribu Ikulu.Bila mabadiliko sasa tutapata wabunge wachaache wa upinzani.tena mimi ningeshauri vyama kuliko kuendelea kutafuta haki ya mikutano ya hadhara hoja hizi wazilete bungeni kwanza.Nadhani.
From: 'lucas haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, July 25, 2017 8:11 AM
Subject: Re: [wanabidii] TABIA HII YA LISU: SIKU MOJA ITALIAIBISHA TAIFA
Kaka Elisa MuhingoNimependa uchambuzi wako na kwakweli niseme umemwongelea Magufuli katika njia njema na ya haki kwake.Nahisi hisia zikakupanda ulipoanza kumwongelea Tundu Antipas Lissu, nafahamu ukiona jambo zuri na baadaye ukaona mtu anatia mkono kulichafua mazoe ya kibinadamu unahemkwa.Kama ulikuwa kijana wakati Mwinyi anamalizia utawala wake, utakuwa wewe na mimi tulimpenda au kusisimkwa na Augustini Lyatonga Mrema.Alikuwa alama ya machozi ya wanyonge, mtetezi na kila kitu.Tulipo ambiwa Mrema pamoja na uzuri wake, hapiti katika miimili ya sheria anaposhughulikia matatizo, tuliwazomea waliosema hivyo, kuanzia Marando,Ringo Tenga, Joseph Selasini n.k.Magufuli Rais wa mfano, anachafuliwa na watu wa chama, watendaji na viongozi wengine.Wanamchafua kwa kumwelekeza avunje katiba na sheria kwa kuzuia vyama vingine visifanye kazi kasolo chama pinduzi.Mimi ni mwanachama wa chma hiki kwazaidi ya miaka 25.Mimi ni muumini wa kutenda haki kwa wote ili kuleta afya ya akili, mahusiano mema, maendeleo na ukuaji wa kila mmoja.Leo Magufuli angawaacha vyama shindani vifanye kazi yake, vingeisha futika, kuvifanyia ukatilia unavikuza pasipo sababu, kumbuka kuna kura za hasira, kuna kura za huruma, hizi ndiyo nyingi.Unapopanda chuki ukadhani utawatisha wengine haiwezi kukiacha chama chako salama, kwanza kitakosa mbinu sahihi za siasa za kiushindani zitategemea jeshi la polisi. Hapa ndiyo mwanzo wa matumizi makubwa kutumika kwenye ulinzi bila sababu ya maana.Chama kuwa legelege kwakuwa kinabebwa na jeshi na serikali.Wote tusaidiane kumwambia Magufuli umefanya na unafanya vizuri lakini katika usawa, haki na katika jichungulie visije vikaondoa ile thamani na tunu uliyopewa na Mungu.Narudia kusema, Magufuli hana tatizo, tatizo ni watendaji wa chama kumtaka yeye afanye kazi serikalini kama katibu wa chama.On Monday, July 24, 2017, 11:14:29 PM GMT+3, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:Toka rais Magufuli alipoingia madarakani kumekuwa na sura mbili duniani.Nje mataifa mengi yanamuunga mkono. Baadhi ya wananchi wanatamani angekuwa rais wa nchi zao.Ndani ya nchi wananchi walio wengi wanamuunga mkono. Wanaanza kuona adha walizolalamikia zimepungua, au kuna matumaini kuwa mbele kuna matumaini.Makundi haya mawili ni sehemu ya sura moja. Yote yana sababu zinazofanana.Mataifa mengi hasa ya uchumi mdogo, yaani mataifa maskini wamechoshwa na Rushwa, ufisadi, wizi, ukosefu wa uwajibikaji nakadhalika. Viongozi walio wengi wamekuwa wakijilimbikiza mali na kwa kweli wakishaingia madarakani wanaanza kuishi kama wale walio katika mataifa tajiri huku wananchi wao wakiumia. Wanaumia kwa kubeba serikali kubwa na zenye marupurupu yasiyoneneka huku huduma za kijamii zikibaki chini na watawala wakisingizia hali mbaya ya umaskini.Tanzania hatukupona hilo. Nisamehewe kwa kutaja mifano ya karibu. Serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani ilionekana kugawa vyeo si kwa manufaa ya wananchi bali waliopata vyeo. Tukumbushane mgawanyo wa Wizara ya mambo ya ndani kwa kuanzisha wizara ya usalama wa raia. Mpaka tulipopiga kelele kwa usikivu wa rais akazirudisha zikawa moja. Lakini tumeshuhudia mgawanyo wa wilaya na mikoa huku hayo hayaleti tija bali mzigo kwa walipa kodi. Tumeshuhudia utumbuaji wa mali ya umma kupitia misafara mirefu na safari za mara kwa mara za viongozi. Tumeshuhudia watu Fulani wakiwa na uhakika kwamba hawawezi kuguswa na vyombo vya dola. Tumeshuhudia kashfa zinatokea, uchunguzi unafanyika, inaonekana wazi kuwa Fulani na Fulani wana kesi ya kujibu lakini hawashtakiwi. Ikafika mahala wengine wakataka kugombea na kutaka kulitawala taifa. Ukweli tulifika mahala maneno ya kuchochea maasi yakaanza kutoka. Nakumbuka kusoma mahala mtu akitania (au akimaanisha) kuwa kama Mwamnyange akiingia ikulu atashangilia. Tulifika mahala pabaya. Ukweli tulifika mahala watu wakadhani uchaguzi hauwezi kutusaidia kutoka kwenye shida hizi. Hayo yakiwa hapa nchini ndivyo ilivyo kwenye mataifa yote yanayomshangilia na kumpongeza magufuli.Mataifa na mashirika yanayotufadhili katika miradi mbalimbali walifika mahala wakaamua kuacha kutusaidia. Ikawa viongozi watoke nje kubembeleza misaada. Wakawa wanakwenda nchi kumi wanaahidiwa sehemu mbili tu.Baada ya uchaguzi, 2015 na Dr. John Magufuli kushinda Tanzania na ulimwengu tulishuhudia mabadiliko. Mtu aweza kuandika mengi; lakini napenda kuyaandika kwa muhtasari:= Tumeshuhudia Serikali ikipunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima. Safari ziliachwa na sasa zinadhibitiwa. Vikao visivyo vya lazima havifanyiki na vinavyofanyika havitumii posho za ajabu au kutumia matumizi ya anasa huku tukiwa maskini.= Wizi wa ajabu umedhibitiwa. Wafanyakazi hewa wameondolewa na kama wamebaki basi ni kwa kiwango kidogo sana. Mikataba iliyokuwa inatuibia imerekebishwa na kwa kweli rais amethubutu kuifumua mikataba.= Mafisadi, wala rushwa, na waharibifu wa mali za umma vimedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.= Biashara na matumizi ya madawa ya kulevya vimeshughulikiwa kwa kiwango cha hali ya juu na si muda mrefu kuna watu watakuja kujifunza Tanzania ilifanyaje katika vita hii.= Nidhamu imerejea. Nani angetegemea watu kama Singasinga wa IPTL angelala rupango? Nani angefikiri Manji angelala lockup? Wafanyakazi serikalini na ofisi za umma kwa ujumla sasa ukifika unahudumiwa kwa nidhamu sana. Kuna wanaosema watu hawako huru. Nani alitarajia watu waliokuwa wanaingia ofisini na kutoka, waache tabia hiyo kwa uhuru? Ni halali walazimishwe kufika kazini na kuifanya kwa ufanisi. Kama wanalazimika sawa. Si wanalazimika kwa mujibu wa mikataba tu? Lakini nidhamu imerudi.Kazi hii kubwa iliyofanywa na rais Magufuli imefanikiwa na kuonwa ndani na nje. Viongozi badala ya kusubiri rais aende kwao kuomba sasa wanakuja wenyewe na kuahidi misaada. Tumeshuhudia majuzi waziri mkuu wa India anaamua kujiunga na rais magufuli alipotembelea kibaha huku akiwa kwao. Akakatisha shughuli zake na kuhutubia mkutano wa magufuli kwa njia ya mtandao. Lini uliisikia hiyo. Tena anafanya hivyo kueleza shkrani zake na kuahidi kuisaidia Tanzania kuondokana na tatizo la maji..Kwa wale waliokuwa wanafaidika wanaona hakuna mtu mbaya kama Magufuli. Wako tayari kufanya lolote na hii ilitarajiwa. Wako tayari kutumia mbinu yoyote ili kumyumbisha au kuyumbisha umma wa Tanzania. Wako tayari kugharimia kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kuangalia kati yetu kuna nani wanaoweza kulipwa wakafanya wanaloweza kufanya. Nitaeleza huko mbele lakini siamini kama Tundu Lisu, kwa mfano; hayuko kwenye Pay roll ya mtuWakati hilo kundi hilo likiyaona anayoyafanya Magufuli kuna kundi la pili lililokataa si kuona tu anayofanya Magufuli bali haliko tayari kusikia ulimwengu unamsemaje. Kama watu wasio na akili wakati wengine wanamsifu wao wanakazana kuwaelimisha wengine kuwa Magufuli hafanyi chochote. Kuna mambo mengine kama unaona kitu Fulani na walio wengi wanaona kingine lazima utafute mkakati wa kuwaelimisha unachoona na namna bora ni kunyamaza kwanza. Hivi watu waliokandamizwa na hayo yote niliyoyataja wawezaje kusimama mbele za watu ukasema tunateseka kwa kukosa kibali cha kuandamana? Una akili kweli? Watu walikandamiza na rushwa na ufisadi, mzigo wa serikali kubwa, makusanyo makubwa ya kodi isiyoonekana inafanya nini. Sasa hayo yameondoka. Unasema hatuna kibali cha kuandamana. Kuandamana kudai nini? Mambo ya kufanya watu waandamane yameondolewa. Kwanza hata bila kupiga marufuku kuandamana utaandamana kupinga nini? Badala ya kwenda shambani kulima ili upitishe mazao kwenye barabara nzuri unataka utumie barabara nzuri kuandamana tena bila kudai chochote? Hii nayo inakutwa Tanzania tu.Angalau wengine wamejirudi. Wanasema Magufuli anafanya vizuri lakini ======. Angalau hao unaweza kupata cha kujadiliana naoLakini tunaye mwenzetu Tundu Lisu. Sehemu ninayomfahamu ni mwanaharakati. Kwa kidogo nikijuacho anapenda kutetea haki. Hana historia ya kuhusika na Rushwa. Niliwahi kuambiwa kuwa kama angekuwa mtoa rushwa angeishakuwa mbunge zamani. Kwa sababu hiyo nilitokea kumpenda. Wakati CHADEMA Ikiwa na kiongozi (Dr. Slaa) kulikuwa na udhibiti. Mambo ya kipuuzi tunayoyaona sasa angekuwepo tusingeyaona. Wabunge wake walitamka mambo yaliyohaririwa kwa mantiki. Sasa hayupo ndipo tunashuhudia madhara yake.Tundu lisu, mbunge wa Singida anatamka mambo mpaka UNAULIZA kama huyu alilelewa na bibi yake au alilelewa msituni tu na nyani kwa hiyo utamaduni wa binadamu anajifunza kadri anavyowazoea binadamu. Ni kweli anamchukia Dr Magufuli. Huenda ana sababu. Huwezi kujua aliahidiwa nini kama chama chake kingeshinda. Anaweza kuumia kuliko wengine. Kuna matamshi anayatamka juu ya Magufuli ukiyapima unaona yako nje ya mlolongo wa siasa. Sipendi kutamka maneno yoyote anayoyasema ili kila anayetaka atafute. Lakini matamshi yake unaweza kujiuliza taaluma yake ina maadili ya kazi? Yeye ni Rais wa TLS. Hivi humo TLS ndivyo wanavyojibizana wakitofautiana? Au hawatofautiani? Watu wengi waliitahadhalisha TLS kuhusu Lisu kuchaguliwa kuwa rais wa taasisi hiyo. Kwa ushabiki sijui niuiteje wakamchagua. Bila shaka walidhani wanamkomesha aliyewatahadhalisha. Sasa tunajiuliza TLS ina Codes of Conduct? Zinaruhusu hayo tunayoyaona Lisu akifanya? Sasa nina uhakika kuwa TLS iko njia panda: Kuendelea kukubaliana na Lisu, heshima yake ikashuka machoni pa jamii au kuamua kujitenga na Lisu. Kama Codes of Conduct zinaruhusu hayo basi ndiyo hivyo. TLS inafutika. Inajifuta.Mwenendo huu wa Lisu usipodhibitiwa basi taifa litaingia pabaya. Mimi ninadhani hatutafika huko. Kama Serikali itashindwa, wapo wazalendo wa nchi hii watamdhibiti Tundu.Subiri kidogo.Elisa Muhingo0767 187 507--Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment