Nachangia kirefi kama Kawa
Huyo Mheshimiwa Afanye Utafiti ili afahamu kuwa watu wa Pwani kwa makabila ni Matrilineal. Wanarithi kwa Mama wavulana na wasichana. Hii inakwenda mpaka Lindi na Mtwara. tatizo ni pale mwanaume toka kabila lingine anapomuoa na kutaka ardhi iandikishwe kwa jina lake na mwanamke akakubali. Kisha mwanaume anaiuza. Mwanamke ukimpiga au kumuonea anaondoka kurudi kwao na ukafanye kazi ya kikao ili arudi tena kwako na kulipa faini utakazopewa. Kipigo tu kitamrudisha kwao. Hela yake akiuza embe, nazi, mazao au kupika chapati, kuuza maandani etc NI ZAKE sio za mume hata. Akitaka atachangia matumizi ya familia ila ni zake ananunua atakacho mume kazi yake kulisha familia, kwenda sokoni-dukani kuleta mahitaji. Wakienda shamba wote au mama atakwenda na vijana wake kazi ya mume kuandaa shamba yeye kupalilia, kupanda na kuvuna. Kubeba mizigo ya mazao-baba. Customary land titles muhimu kwa akina mama coastal areas lakini hata umuoe umkute na ardhi kubwa ni ya Mke si ya Mume. Hata mimi nimenunua ardhi Dar Salasala ya Mama Mzee Mzaramo na Mumewe Mzarano. Familia hiyo wanawake wamemiliki ardhi kama kitongoji kizima. Kwa sasa wamama hao wazee wameuza wamemaliza kubakiza kidogo wanapoishi na baadhi wameshafariki. Wajukuu walipopewa ardhi-wameiuza yote na sasa familia zimahamia mashimo ya kuvunja mawe na kokoto! Muhimu kusoma na kujua historia ya kabila na property ownership, matatizo ya sasa ili uwasaidie vizuri zaidi. Wafundishe Sheria ya Ardhi na kuunda kamati zake zipewe mafunzo. Viongozi wa Vijiji (sio ukoo) ndio mara nyingi huwapora ardhi na kuigawa/kuiuza kiwizi wakifahamu hao wamama Wazee hawajui kusoma na kuandika, hawajui mfumo wa sheria wanawaonea tu. Hata kule ambako NGO za Jinsia zimefundisha Sheria ya Ardhi na Haki ya Mwanamke, kujenga uwezo kamati zilizoundwa kwa kuzingatia sheria ya ardhi, kuanzisha oparalegals na majarida ya ardhi vijiji -bado kuna utata mkubwa wa sustainability na magomvi ya ardhi, mapigano kati ya wakulima na wafugaji wajao na kuvamia ardhi yapo. Morogoro vijiji vilipata mafunzo kutoka LHRC lakini inaongoza kwa mapigano. Magomvi yapo Hai ambako Land Laaw na kamati ziliunda na NGO za jinsia na zikifanya vizuri. Sustainable land use ndio ya kuzingatia hasa na ni hitaji kubwa ili kupunguza uharibifu ardhi, njaa na umasikini.
Mume anapouza ardhikinyemela anajua ardhi si yake na anataka kumkata makali mwanamke miliki ardhi. Hivyo, kutoa hati miliki kimila au statutory itasaidia na hati ipigwe muhuri-Haihamishiki bila ya Kibali cha Waziri husika ambaye atapiga muhuri unaotambulika ihamishwe umiliki. Hii itazuia uuzaji hovyo wa ardhi kwa wanaume wa ndoa, urafiki na ndugu matapeli me au ke. Vibaka wapo ndani ya familia pia. Anamdanganya bibi auze kisha anasepa na hela na kumpa kidogo. Kwa assa serikali inachukua ardhi ya kimila na kumpa owner 60%. Inawapa ruhusa mabwana ardhi kuuza 40% na kujaza matumbo wanajipa umiliki na kula hela. Mpe 100% si ana wajukuu, watoto atagawia? atapata mwekezaji na atakuwa mbia atapata hela ya kula. GVT estate lands zipunguzwe ndio raia wengine wapate ardhi. Kupima viwanja miji midogo kisha unampa owner viwanja high density badala ya shamba lake atakosa pa kulima na kujilisha na hana ajira. Matokeo yake umalaya utakuwa vitoto vidogo kuuzwa ili bibi apate kula na vijukuu. Kwa ninimtanzania haelewi hili? unakuta mtu ana ekari zake 5 Bunju, ana minazi, miembe, shamba la mananasi anauza na kabonde analima nyanya na bamia anauza. Serikali inapima viwanja na kumwacha na plot moja mabonde yanapimwa plots na kugawiwa. Utaona Bagamoyo eneo la Bonde la Mto Ruvu ambalo Raia wazawa wakilima mpunga na mazao ya bustani toka ulimwengu uundwe awwe huko hata Ukoloni na post Independece-Leo hii wasomi wengi, wetlands sheria inataka zilindwe lakini pita uone minara na kungo, fence na majengo ndani ya Wetland area! Ni hivyo ukifika Morogoro Mjini Wetlands zimepimwa plots za nyumba na viwanda, godowns na maji ya mto yanapita nje ya jengo kayawekea mfereji. Watoe mashamba ya katani ambayo yapo dry area wajenge nyumba wawache wazawa na wetland zao wawapimie waendelee kulima kujiajiri ila wakataze utengenezaji tofari za kuchoma bondeni kando ta mito! Nani haelewi haya. Vyama vya Jinsia (NGO) ikazanie hili pia kwani muathirika ni mwanamke, mama mzee, msichana anayeuza nyanya, bamia zitokazo bondeni hapa na kujipatia chakula. Wakulima wengi ni wanawake na wanaume wazee na wasichana.
Kingine cha kusimamia na kutetea ni serikali kupiga marufuku kuhamahama kwa kilimo na ufugaji nje ya ardhi yako unayomiliki. Ndio inajulikana kuwa watu walitumia ardhi kulingana na ecology (ecological niches). Analima Kibaha anashamba pia mlandizi analima mazao tofauti. Anashamba la midizi na Kahawa juu milimani Pare na analima bondeni Upareni huko ana mashamba ya mpunga kilimo cha umwagiliaji, nyanya, bamia, kabichi na mazao mengine ya bustani na ana mifugo. ana ndugu juu na bondeni au wake zake vitongoji-vijiji mbali mbali ambako wana ardhi ya mashamba na kuna mifugo. Wape hati zao na watumie ardhi kiendelevu/sustainably. Ikiwa marufuku kuhamahama uharibifu wa ardhi public land, protected area kwa kilimo na mifugo utaisha. Ukikutwa na mifugo ndani ya ardhi si yako aidha private au group land-adhabu kali pamoja na kukufirisi mazao au mifugo ugharimie uharibifu uliofanya. Hii ya Kutoa Hati single/group na marufuku kuhamahama itaondoa mapigano ya wakulima na wafugaji. Watu wanatiwa vilema, kuuawa, kubakwa pia ktk kulipizana kisasi. Ni upumbavu tunaoulinda kutetea mtu ahame na mifugo kutoka Mwanza, Manyara aende Kisarawe, Kilwa,Lindi, Tunduru au Sumbawanga. Tuache SIASA tuangalie Sera na Sheria na kutekeleza mikakati yake. Tuache kuwaiga wazungu wanaoona eti wafugaji wanaonewa. Hebu tembea nenda vijiji vya Loliondo, NCAA, Babati, Monduli, Manyara uone wanavyolima kwa trekta na plau na hawalishii mifugo mashambani. Wanachuma madini -dhahabu, Tanzanite, kununua mifugo na kuongeza wake. Wanajenga kambi na lodges za utalii ndani ya malisho ya mifugo na pia wildlife conservation areas ambako wameruhusiwa kuishi sio kulima. Lodges na magari ya utalii yanaongezeka na wanalima na mifugo iliyojazwa kugawiwa wafugaji kupeleka kwingine. Mashamba yanalishiwa mifugo hata ndani ya townships na municipalities. Hakukuwa na mifugo Bunju, Ruvu kilimo cha umwagiliaji Makurunge Bagamoyo au Mhenda Kilosa, Zombo, Ulaya ambako kuna wetlands za kilimi kikumbwa cha mpunga na mahindi-leo hii mifugo imejaa na watu kuishi kwa waziwasi. Mauaji mpaka ya watoto, ifuguze isile mahindi upigwe, ubakwe au uuawe, nyumba yako ichomwe. Viongozi kula hela kimagendo kutoa ardhi kwao na mpaka kwa wageni wahamiaji bila kushirikisha umma wa kijiji kama miongozo inavyoelekeza. Bado hao wahamiajikutoka Burundi na kwingineko. Hili la kuhamahama linakoma na maendeleo kuwepo, ardhikutumika sustainably kama sustainable crop farming and livestock keeping itakuwa ni sheria. Ukimkuta analipa milimani bila ya makinga maji (matuta for soil conservation) abapte kibano. Pia idadi ya mifugo-kama ng'ombe mmoja anahitaji ekari 5 yeye anao katika eka 5 ng'ombe elfu 10-kibano! Ulaya wamewezaje sisi tushindwe na ardhi kubwa na kilimo na ufugaji haitumiki? Kwa nini wazurure watakavyo na kusababisha mapigano? Unatoaje Kibali cha kutaka mito kuuza mkaa Kisarawe na Muhusika hana Shamba la Miti? Wasukuma wamejaa Kisarawe wanakata miti mpaka ya miembe na mikorosho mkaa unauonaukija Mbagala na maeneo mengine ya Dar. Anampa mkaa mama mzee na kumlimia shamba yeye anakata miti migumu ambayo ni mengi sana Coastal areas kwa vile minazi inatoa kuni za kupikia pia mikoroshoi na miembe-waannchi hawakati hovyo miti. Leseni za magogo, mkaa, mbao ndio chanzo kikuu SERIKALI kuhalalisha deforestation and environmental degradation. Wanahamia mpaka misitu ya hifadhi kulima kwa visingizio na mifugo kujaa na miti kukatwa. Zuia kuhamahama, toa hati miliki ardhi, hamia na lima, lisha mifugo pale ambapo una hati miliki tu! Nje ya hapo-Kisago-HAPA KAZI TU!! Tunahitaji kushikishwa adabu sasa kuzingatia sheria kwa nguvu. Elimu zinatolewa hatusikii. Toa support kwaextension staff kwani wabongo wanatabia ya VISASI na mauaji sheria inapotekelezwa!
Kama Kawa
--------------------------------------------
On Wed, 8/2/17, Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] DC Kisarawe ataka wanawake washirikishwe ardhi ya familia inapouzwa
To: "Ahmad Michuzi" <amichuzi@gmail.com>, "Adam Mzee" <thamani80@gmail.com>, "Geofrey Adroph" <pamojapure@gmail.com>, "assenga oscar" <assengaoscar@gmail.com>, "william malecela" <willymalec@gmail.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Deogratius Rweyunga" <drweyunga@gmail.com>, "Richard Mwaikenda" <rmwaikenda@yahoo.com>, "uwazi@hotmail.com" <uwazi@hotmail.com>, "Haki Ngowi" <Haki.yako@gmail.com>, "Henry Mdimu" <mdimuz@gmail.com>, "Luke Joe" <djlukejoe@gmail.com>, "Josephat Lukaza" <josephat.lukaza@gmail.com>, "Jestina George" <jestinageorge@gmail.com>, "johnbukuku@gmail.com" <johnbukuku@gmail.com>, "Krantz Mwantepele" <krantzcharles@gmail.com>, "Krantz Mwantepele" <kmwantepele@gmail.com>, "Muhidin Sufiani" <sufianimafotoblog@gmail.com>, "Othman Michuzi" <othmanmichuzi@gmail.com>, "Blog za mikoani" <blogzamikoa@live.com>, "info@dewjiblog.com" <info@dewjiblog.com>, "Bashir Nkoromo" <nkoromo@gmail.com>, "BINAGI MEDIA GROUP" <binagimediagroup@gmail.com>, "Lindi Yetu Blog" <lindiyetu@gmail.com>
Date: Wednesday, 8 February, 2017, 12:40
DC
Kisarawe ataka wanawake washirikishwe ardhi ya familia
inapouzwa
[caption
id="attachment_77424" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77424" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8532.jpg"
alt="" width="800"
height="446" /> Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,
Happyness Seneda (kushoto) akizungumza alipokuwa akifunga
semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa
Serikali za mitaa juu ya utafiti raghibishi ngazi ya Wilaya
ya Kisarawe uliobaini uwepo wa migogoro mingi ya ardhi.
Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela
Mwampamba akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi. Semina hiyo
iliandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption]
[caption
id="attachment_77427" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77427" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8563.jpg"
alt="" width="800"
height="552" /> Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,
Happyness Seneda (kushoto) akizungumza na washiriki katika
semina hiyo iliyofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Kulia ni Katibu Tawala wa
Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba. Semina hiyo iliandaliwa
na TGNP Mtandao.[/caption]
[caption
id="attachment_77428" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77428" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8578.jpg"
alt="" width="800"
height="427" /> Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza na
washiriki katika semina hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda pamoja na Katibu Tawala
wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela
Mwampamba.[/caption]
[caption
id="attachment_77426" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77426" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8538.jpg"
alt="" width="800"
height="486" /> Baadhi ya washiriki wa semina
kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali
za mitaa kutoka Wilayani Kisarawe wakijadili changamoto za
migogoro ya ardhi na nmna ya kuikabili. Semina hiyo
iliandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption]
[caption
id="attachment_77430" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77430" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8589.jpg"
alt="" width="800"
height="589" /> Mwakilishi wa wananchi Kijiji
cha Vilabwa, Kuruthum Mbwana (katikati) akizungumzia
wanawake wanavyominywa katika umiliki wa ardhi katika eneo
lao.[/caption]
[caption
id="attachment_77431" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77431" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8600.jpg"
alt="" width="800"
height="539" /> Picha ya pamoja ya washiriki wa
semina hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda,
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),
Bi. Lilian Liundi.[/caption]
<strong>MKUU</strong> wa
Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda amewataka watendaji na
viongozi wa vijiji vya wilaya hiyo kuakikisha wanatoa
vipaumbele kwa wanawake katika umiliki wa ardhi na pia
familia kuwashirikisha wanawake kutoa uamuzi pale wanapotaka
kuuza ardhi mali ya familia. Bi. Seneda alitoa kauli hiyo
alipokuwa akifunga semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji
na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kisarawe
iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kujadilia
matokeo ya utafiti raghibishi uliobaini uwepo wa migogoro
mingi ya ardhi.Kiongozi huyo amesema wanawake wengi
wamekuwa wakiachwa nyuma katika suala zima la umiliki ardhi
na wakati mwingine hata familia zimekuwa zikiuza ardhi
kinyemela pasipo washirikisha wanawake jambo ambalo si la
kiungwana."...Wakati mwingine unakuta
mume anaamua kuuza ardhi hata bila kumshirikisha mkewe hili
lazima viongozi mlisimamie, unapoletewa maamuzi ya familia
kutaka kuuza ardhi waulizeni wanaume je wamewashirikisha
wake zao katika uamuzi wa kuuza ardhi hiyo?," alisema
Bi. Seneda akizungumza katika warsha
hiyo.Alitoa
tahadhari kuwa endapo ataletea taarifa ya mwanamke katika
wilaya yake kudhuumiwa ardhi na kiongozi au mtendaji wa
kijiji kukaa kimya atahakikisha anaanza kumuwajibisha
kiongozi kwa kufumbia macho dhuluma hiyo. Hata hivyo
alisisitiza kuwa wanawake wana haki ya kumiliki ardhi kama
ilivyo kwa wanaume hivyo viongozi wanapaswa kulisimamia
suala hilo vizuri ili kundi hilo lisinyanyasike katika
umiliki.
Aliwataka viongozi wa vijiji
kuhakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi ngazi za
juu kutatua migogoro ya ardhi ili kupunguza kero za wananchi
na migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo hayo.
Alisema uongozi wake kwa kushirikiana na vyombo vingine
wataendelea kufanya oparesheni za mara kwa mara kuhakikisha
wanawaondoa wafugaji ambao wamekuwa wakivamia baadhi ya
vijiji vya wilaya hiyo na kulisha mifugo yao jambo ambalo
limekuwa likileta migogoro na uharibifu wa mazao ya
wakulima.
[caption
id="attachment_77429" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77429" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8585.jpg"
alt="" width="800"
height="482" /> Bi. Bahati Magendo (wa kwanza
kulia) mwakilishi wa wananchi Kijiji cha Vilabwa
akizungumzia migogoro ya ardhi katika
vijiji.[/caption]
Kwa
upande wake, Bi. Bahati Magendo mwakilishi wa wananchi
Kijiji cha Vilabwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi na
watendaji wa vijiji kuwapokea wafugaji kinyemela pasipo
husisha wananchi jambo ambalo limekuwa likiendeleza migogoro
baina yao na wafugaji. Alisema viongozi wamekuwa
hawawashirikishi wananchi suala la kupokea wafugaji vijijini
jambo ambalo limekuwa chanzo kikubwa cha migogoro.
"..Viongozi wanatudharau wananchi hasa sie akinamama
wamekuwa hawatushirikishi katika maamuzi...utakuta mfugaji
anakuja kijijini anazungumza na kiongozi kimya kimya baadaye
anahamia sisi hatuambiwi chochote," alisema
Magendo.
[caption
id="attachment_77425" align="alignnone"
width="800"]<img class="size-full
wp-image-77425" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/02/IMG_8537.jpg"
alt="" width="800"
height="399" /> Baadhi ya washiriki wa semina
kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali
za mitaa kutoka Wilayani Kisarawe wakijadili changamoto za
migogoro ya ardhi na nmna ya kuikabili. Semina hiyo
iliandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption]
KAWAIDA:-
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (kushoto)
akizungumza alipokuwa akifunga semina kwa baadhi ya
madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa juu ya
utafiti raghibishi ngazi ya Wilaya ya Kisarawe uliobaini
uwepo wa migogoro mingi ya ardhi. Kushoto kwake ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba akifuatiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),
Bi. Lilian Liundi. Semina hiyo iliandaliwa na TGNP
Mtandao.
Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (kushoto) akizungumza
na washiriki katika semina hiyo iliyofanyika Katika Ukumbi
wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Kulia ni
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba. Semina
hiyo iliandaliwa na TGNP Mtandao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian
Liundi akizungumza na washiriki katika semina hiyo. Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda
pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela
Mwampamba.
Baadhi
ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na
wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilayani Kisarawe
wakijadili changamoto za migogoro ya ardhi na nmna ya
kuikabili. Semina hiyo iliandaliwa na TGNP
Mtandao.
Mwakilishi
wa wananchi Kijiji cha Vilabwa, Kuruthum Mbwana (katikati)
akizungumzia wanawake wanavyominywa katika umiliki wa ardhi
katika eneo lao.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa semina hiyo na Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe, Happyness Seneda, Katibu Tawala wa Wilaya ya
Kisarawe, Mtela Mwampamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian
Liundi.MKUU wa
Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda amewataka watendaji na
viongozi wa vijiji vya wilaya hiyo kuakikisha wanatoa
vipaumbele kwa wanawake katika umiliki wa ardhi na pia
familia kuwashirikisha wanawake kutoa uamuzi pale wanapotaka
kuuza ardhi mali ya familia. Bi. Seneda alitoa kauli hiyo
alipokuwa akifunga semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji
na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kisarawe
iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kujadilia
matokeo ya utafiti raghibishi uliobaini uwepo wa migogoro
mingi ya ardhi.
Kiongozi huyo amesema wanawake wengi wamekuwa wakiachwa
nyuma katika suala zima la umiliki ardhi na wakati mwingine
hata familia zimekuwa zikiuza ardhi kinyemela pasipo
washirikisha wanawake jambo ambalo si la kiungwana.
"...Wakati mwingine unakuta mume anaamua kuuza ardhi
hata bila kumshirikisha mkewe hili lazima viongozi
mlisimamie, unapoletewa maamuzi ya familia kutaka kuuza
ardhi waulizeni wanaume je wamewashirikisha wake zao katika
uamuzi wa kuuza ardhi hiyo?," alisema Bi. Seneda
akizungumza katika warsha hiyo.
Alitoa tahadhari kuwa endapo ataletea taarifa ya mwanamke
katika wilaya yake kudhuumiwa ardhi na kiongozi au mtendaji
wa kijiji kukaa kimya atahakikisha anaanza kumuwajibisha
kiongozi kwa kufumbia macho dhuluma hiyo. Hata hivyo
alisisitiza kuwa wanawake wana haki ya kumiliki ardhi kama
ilivyo kwa wanaume hivyo viongozi wanapaswa kulisimamia
suala hilo vizuri ili kundi hilo lisinyanyasike katika
umiliki.Aliwataka
viongozi wa vijiji kuhakikisha wanashirikiana na wananchi na
viongozi ngazi za juu kutatua migogoro ya ardhi ili
kupunguza kero za wananchi na migogoro kati ya wakulima na
wafugaji katika maeneo hayo. Alisema uongozi wake kwa
kushirikiana na vyombo vingine wataendelea kufanya
oparesheni za mara kwa mara kuhakikisha wanawaondoa wafugaji
ambao wamekuwa wakivamia baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo na
kulisha mifugo yao jambo ambalo limekuwa likileta migogoro
na uharibifu wa mazao ya wakulima.
Bi.
Bahati Magendo (wa kwanza kulia) mwakilishi wa wananchi
Kijiji cha Vilabwa akizungumzia migogoro ya ardhi katika
vijiji.Kwa
upande wake, Bi. Bahati Magendo mwakilishi wa wananchi
Kijiji cha Vilabwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi na
watendaji wa vijiji kuwapokea wafugaji kinyemela pasipo
husisha wananchi jambo ambalo limekuwa likiendeleza migogoro
baina yao na wafugaji. Alisema viongozi wamekuwa
hawawashirikishi wananchi suala la kupokea wafugaji vijijini
jambo ambalo limekuwa chanzo kikubwa cha migogoro.
"..Viongozi wanatudharau wananchi hasa sie akinamama
wamekuwa hawatushirikishi katika maamuzi...utakuta mfugaji
anakuja kijijini anazungumza na kiongozi kimya kimya baadaye
anahamia sisi hatuambiwi chochote," alisema
Magendo.
Baadhi
ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na
wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilayani Kisarawe
wakijadili changamoto za migogoro ya ardhi na nmna ya
kuikabili. Semina hiyo iliandaliwa na TGNP
Mtandao.
--
___________________________________________________________________________________Joachim
Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na
Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:-
mushi@thehabari.com/
jomushi79@yahoo.com/
info@thehabari.com
Mobile:- 0717
030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment