Sunday 27 December 2015

[wanabidii] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. CCM Zanzibar yajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa marudio

Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza kwa ukubwa kwa siku ya leo kwa mujibu wa mtandao wa mjengwablog.com. Inatoa tafsiri, kuwa katika mtanziko wa kisiasa uliopo visiwani CCM, na katika meza ya majadiliano ya pande mbili, CCM Zanzibar wameweka mezani ' karata ya kurudia uchaguzi'. Kwamba CCM wako tayari kurudia uchaguzi. Hivyo, tafsiri ya jambo hilo inaonyesha pia, kuwa upande wa pili kwa maana ya CUF, wao wamerusha mezani ' karata ya katu usirejewe'. 
Kwa mazingira yalivyokuwa kabla ya matokeo kufutwa, ikiwamo ulalamishi na madai ya kuvunjwa kwa taratibu, uzoefu unaonyesha, kuwa, kama pande zote mbili zina hakika ya ushindi, basi, kuna mahali wakitanguliza busara, itabidi ziwaandae wapiga kura wao kwenda kwenye roundi ya pili katika mazingira yatakayozihakikishia pande zote mbili, kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki. Hakuna namna nyingine ya kumaliza kadhia hii bila kufanya uchaguzi mwengine utakaoridhiwa, sio tu na pande mbili, bali jumuiya ya kimataifa.

2. Waganga wa Tiba za Jadi waigomea Serikali. Hii ni habari inayopewa nafasi ya pili kwenye mtandao wa Mjengwablog.com. Nafasi ya waganga wa tiba asilia ni kubwa katika jamii yenye wengi wenye kukumbwa na maradhi. Lakini, waganga wa tiba asilia watambue pia, kuwa Serikali ina jukumu na wajibu wa kuhakikisha jamii inapata tiba zenye uhakika. Kumejitokeza baadhi ya waganga wa tiba asilia wasio waadilifu. Ni wajibu wa Serikali kuratibu shughuli za tiba asilia.

3. Magufuli awatesa Mawaziri wake
Habari hii inapewa nafasi ya tatu. Ni kwa namna gani Rais anawatesa mawaziri wake? Ni swali ambalo msomaji angependa kupata majibu yake. Neno kutesa lina tafsiri ya mtu kumuumiza mwingine kimwili na kisaikolojia. Hatudhani kama Rais Magufuli anawatesa mawaziri wake. Kuhimiza watendaji wake kufanya kazi ni jukumu lake kama Rais. Na kama ni kwa mawaziri wenyewe kuamua kutoenda likizo ya krismasi na kufanya kazi yawezekana wamejikuta wana viporo vya kazi ambavyo katika mipangilio yao ya kazi hawakuwa na budi, bali kuvimaliza Lakini, kama waziri atathibitika kutokwenda likizo ya krismasi kwa kuonyesha tu yuko ofisini, kwamba anajali zaidi kufanya kazi kuliko kupumzika na familia yake kusheherekea krismasi na mwaka mpya, basi, hilo ni tatizo la muhusika.

Usikose pia kusoma habari bora ya michezo kwa siku ya leo, na katuni bora pia kwa mujibu wa mtandao wa mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment