Wednesday 30 December 2015

Re: [wanabidii] Kumsakama Kikwete hakumsaidii Magufuli

Comparison ya Nixon na Kennedy haina mashiko. Ni Kennedy aliyemaliza uhasama baina ya Marekani na Russia na kuilazimisha Russia kuondoa makombora yake
ya nuclear Cuba. Vivyo hivyo mlinganisho wa Obama na Bush. Toka mwanzo Obama alipinga vita ya Iraq na wakati anakampeni alisema atayarejesha majeshi ya Marekani kutoka Iraq. Kwa hiyo ni sahihi kulinganisha utawala wa Bush na Obama. Mmoja aliacha nchi imefilisika ikiwa vitani mwingine akaanza kujenga upya uchumi wa Marekani na leo amepunguza deficit ya Marekani. Kwa hiyo kuna merit kulinganisha utawala wa Obama na Bush kama ilivyo kulinganisha utendaji wa Magufuli na Kikwete.
em

2015-12-30 5:45 GMT-05:00 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
WAKATI John F. Kennedy akiwa Rais wa Marekani, sayari yetu ilikaribia kuingia katika Vita ya Tatu ya Dunia ambayo bila shaka ingetuangamiza sote kwa sababu uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia ulikuwa mkubwa. Ugomvi baina ya Marekani na Urusi ulikuwa katika kiwango cha juu.

Chini ya miongo miwili baadaye, Rais Richard Nixon alimkaribisha Rais wa Urusi, Leonid Brezhnev, katika Ikulu ya White House nchini Marekani. Nchi hizo mbili zilikuwa zimeamua kurekebisha uhusiano wao.

Lakini, hakuna Mmarekani aliyesema kwamba kwa uamuzi huo wa Nixon kuzungumza na Brezhnev, alikuwa amemuaibisha Kennedy. Wote walikuwa marais wa nchi moja lakini katika wakati tofauti walifanya maamuzi tofauti.

Ni sawa na stori ya George W. Bush na Barack Obama. Wote pia marais wa Marekani. Lakini, wakati Bush alianzisha vita ya Irak na Afghanistan, Obama amepunguza idadi ya askari waliokwenda kupigana. Kimsingi, kama angeulizwa maoni yake binafsi, inaonekana rais huyo wa sasa wa Marekani hana mpango na mambo ya vita.

Lakini, kwa uamuzi huo wa Obama, huwezi kusema kwamba amemgeuka Bush. Wakati Bush akipeleka askari Irak, Wamarekani walikuwa wameaminishwa kuwa nchi hiyo inahifadhi silaha za maangamizi. Wakati Obama anaingia madarakani, Wamarekani walikuwa wamefahamu kuwa walidanganywa.

Katika nyakati mbili tofauti, marais wawili tofauti wa nchi moja, wamefanya maamuzi tofauti.

Mifano hii haiishii Marekani pekee bali hata hapa kwetu ipo. Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa na uhusiano mbaya na mashirika ya IMF na Benki ya Dunia hususani katika siku zake za mwisho madarakani.
Alipoingia madarakani, Ali Hassan Mwinyi aliamua kufuata masharti yaliyowekwa na wakubwa hao. Wakati huo, hakuna aliyesema kwamba Mzee Mwinyi amemdhalilisha Nyerere. Hali ya uchumi ilikuwa mbaya na 'Mzee Ruksa' hakukubali kuona Watanzania wakipanga foleni kupata huduma muhimu.

Hata hivyo, urais wa Nyerere hauwezi kuonekana mbaya eti tu kwa sababu kwenye miaka ya 1980, hali ya uchumi wa Tanzania ilikuwa mbaya. Pamoja na hali hiyo ngumu ya uchumi, Mwalimu aliwafanya Watanzania kuwa kitu kimoja.
Ndiyo maana, kwa kauli ya busara kabisa, Mzee Mwinyi alipata kusema huko nyuma kwamba kila "zama na kitabu chake". Nyerere hakuwa mkamilifu kwa asilimia 100, Mwinyi na Benjamin Mkapa hivyo pia.

Bila shaka, Jakaya Mrisho Kikwete, naye si malaika na lazima alikuwa na mapungufu wakati wa miaka kumi ya utawala wake.

Awali ya yote kabisa, nakubali kwamba ili kusonga mbele, tunahitaji kufanya uchambuzi wa tulipotokea na tulipokosea. Ukosoaji wowote dhidi ya Kikwete unakubalika ingawa nitatofautiana na kinachoendelea sasa hapa kwetu.

Nina matatizo matatu na wakosoaji wa utawala wa Kikwete. La kwanza, wakosoaji wa Kikwete wanafanya hivyo kwa kumlinganisha na Magufuli. Hili nadhani ni kosa. Magufuli alikuwa na maono yake wakati akitaka urais. Anachofanya ni kile anachokiona ni sahihi.

Kama kila anachofanya kitatafsiriwa kuwa ni 'kijembe' au udhalilishaji dhidi ya mtangulizi wake, athari yake ni kuwa anaweza kuamua kuacha anachokifanya sasa. Lakini, kubwa zaidi, kunamfanya Magufuli aonekane kama Rais ambaye hakuwa na maono yake binafsi zaidi ya kubadili yale ya mtangulizi wake.

Yote hayo si sahihi. Tangu wakati wa kampeni, Magufuli alionyesha dalili ya kuwa hivi alivyo. Wakati CCM kikimpa Magufuli tiketi ya kuwania urais, kilijua kinampa mtu wa namna gani. Wapo wanasiasa wengine ndani ya CCM ambao kama wangepewa nafasi, wangefanana na Kikwete au Mkapa lakini inaonekana CCM ilitaka kwenda njia tofauti.
Njia ya John Magufuli.

Ndiyo maana, naamini si sahihi kutafsiri matendo ya Magufuli kuwa ni udhalilishaji dhidi ya Kikwete. Ni sawa na kusema Mwinyi alimdhalilisha Nyerere kwa kukubali masharti ya IMF au Mkapa alimdhalilisha Mwinyi kwa kuanza kubana wakwepa kodi.

Kila zama zina kitabu chake.
La pili ambalo wakosoaji wa Kikwete hawaliweki mezani kwenye ukosoaji wao ni tofauti ya watu hawa wawili kihaiba. Kikwete ana historia tofauti ya kisiasa na Magufuli.

Kikwete alitengenezwa kama mwanasiasa wakati alipopelekwa Zanzibar kuwa Katibu wa Chama. Zanzibar ya miaka ya 1970 ni ile ambayo hayati Rais Abeid Karume angeweza kwenda ofisini na kucheza bao na drafti na wananchi wake.
Zanzibar ya miaka ya 1970 ni ile ambayo ilikuwa inajaribu kutafuta mwafaka kati ya pande mbili za wahusika wa mapinduzi ya mwaka 1964. Hapa kuna kundi la ASP na wale waliokuwa kwenye Umma Party na Hizbu.

Mmoja wa walezi wakubwa wa kisiasa wa Kikwete wakati akiwa Zanzibar alikuwa ni Sheikh Thabit Kombo. Mojawapo ya ushauri wake ambao Kikwete amekuwa akiutaja mara kwa mara ni ule unaosema "Unapozungumza uweke na akiba ya maneno".

Hivyo, kwa maoni yangu, mtu anayemchambua Kikwete wa mwaka 2015, ni lazima aangalie pia alitengenezwaje. Alikuaje kuaje hadi akaja kuwa Rais?
Katika hali ya kawaida, si rahisi kwa mtu kuelewa kwanini Kikwete alikuwa na baraza la mawaziri la watu 60 kwenye Awamu yake ya Kwanza ya Urais. Lakini, aliingia madarakani wakati kukiwa na mpasuko uliosababishwa na kundi la mtandao lililomsaidia aingie madarakani.

Kwa malezi yake ya kisiasa, Kikwete fikra yake ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila kundi ndani ya chama linawakilishwa ndani ya serikali yake. Ni sawa na ilivyokuwa wakati wa serikali za mwanzo za Mwalimu Nyerere ambako alihakikisha baraza la mawaziri linakuwa na Waislamu, Wakristo, Wazee, Vijana, Wasomi,

Wasio Wasomi, Wazungu, Wahindi na walau kila kundi la kijamii.
Kwa sababu ya fikra hii "jumuishi" kwenye kutafuta mwafaka, Kikwete akaamua kuwa na baraza la mawaziri 60. Magufuli alikuta chama kimeungana dhidi ya mgombea wa upinzani. Hivyo yeye hakuwa na sababu ya kufanya "ujumuishi".

Hata hivyo, Magufuli ana historia tofauti. Yeye ametokea kwenye taaluma ya ualimu. Kazi kubwa ya mwalimu ni kuhakikisha anamsaidia mwanafunzi kufikiri hadi kufikia mwisho wa uwezo wake wa kiakili. Anaweza kufanya hivyo kwa kushauri, kuasa, ukali na mambo mengine.

Magufuli atafanya kila analoweza kuhakikisha Tanzania inafikia katika ukomo wa inapoweza kufikia. Ili kufika hapo, atatumia kila aina ya mbinu alizojifunza kama mwalimu na pia kama mwanasiasa kwenye miaka 20 iliyopita.

Kuna watu walikuwa wanajituma kwa asilimia 60 wakati wa Kikwete lakini sasa wanaweza kujituma kwa asilimia 80 hadi 90 kwa sababu wanajua Magufuli hatakubali. Ubaya wa siasa jumuishi ni kwamba wakati mwingine utendaji si kete muhimu.

Tuliona hata wakati wa Mwalimu Nyerere kwamba kuna watu walikuwa wanafanya madudu sehemu moja na kuhamishiwa kwingine. Kwenye serikali ya Abeid Karume, wapo watu waliokuwa hawajui hata neno moja la sheria lakini walihukumu watu kwenye mahakama zilizoundwa baada ya Mapinduzi.

Ndiyo maana, sioni busara ya kuwafananisha Magufuli na Kikwete.
Tofauti yangu ya tatu na wakosoaji wa Kikwete ni kwamba kwenye siku za karibuni imeanza kuonekana kuwa ukosoaji huo ni wa kibinafsi zaidi (personal) kuliko uhalisia.

Nimeona watu wanaolinganisha safari za Kikwete nje ya nchi baada ya kuondoka madarakani na zile zilizofanywa na Magufuli kwenye wakati huohuo. Kama tunataka ulinganifu, kwanini tusimlinganishe Magufuli na marais wa nchi jirani?

Hivi sasa, yanajengwa mazingira ionekane ni dhambi kwa Kikwete kusafiri. Hata katika safari ya kwenye Mkutano wa China na Afrika, ambao Kikwete alikuwa amealikwa na Serikali ya China na Tanzania haikuingia gharama, bado wakosoaji walimsakama.

Ukichunguza, utaona kwamba imekuwa kawaida kuwasakama marais wastaafu wa Tanzania mara wanapomaliza muda wao. Na kwa sababu msukumo unakuwa ni binafsi na si masuala ya msingi, taifa huwa linapoteza muda wa kujifanyia tathmini.
Kwa mfano, kwenye siku za mwisho za utawala wa Mzee Mwinyi, kila mali jijini Dar es Salaam ilianza kutajwa kama inamilikiwa na mke wa Rais, Sitti Mwinyi. Mzee Ruksa akajengewa picha kama kiongozi mbovu zaidi na mlea rushwa kuliko wote wengine.

Leo, imefahamika kuwa madai haya hayakuwa na ukweli.
Mkapa naye alisakamwa kwelikweli wakati anaondoka hususani kutokana na kitendo cha mkewe kufungua biashara wakati akiwa Ikulu. Cha ajabu, siku hizi Mkapa anaonekana kama mmoja wa marais wa Tanzania waliofanya vizuri wakati wao.

Ukichunguza ripoti za karibuni, utabaini kuwa walewale waliokuwa wakimsifia Kikwete na kumsakama Mkapa miaka kumi iliyopita, ndiyo walewale ambao sasa wanaongoza vita ya kumsakama Kikwete na kumsifia Magufuli. Kunani hapa?
Ninaamini pia kuwa wakati utakapofika, Watanzania wataanza kumjadili Kikwete kwa mazuri yake. Kwamba aliikuta Tanzania ikiwa moja na akaiacha ikiwa moja. Kwamba aliongeza ukusanyaji wa mapato. Kwamba alikuwa karibu na wananchi wake na aliwapenda pia.

Jambo ambalo halisemwi ni kwamba Oktoba mwaka huu, Tanzania iliweka rekodi mpya ya kukusanya kodi ya shilingi trilioni 1.1 na mwezi uliofuata, yaani Novemba, Mamlaka ya Mapato (TRA) walikusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.2.
Ili kumsaidia Magufuli, ni vema kueleza yalipo matatizo na namna ya kuyatatua. Namna ya kututoa hapa tulipo si kumsakama Kikwete. Tuliyoyafanya kwa Mwinyi na Mkapa, liwe fundisho kwetu.

Raia Mwema

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment