Monday 28 December 2015

[wanabidii] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. IGP Mangu Alifumua Jeshi la Polisi.
Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wa mjengwablog.com.Ni habari kubwa na yenye kuigusa jamii na maslahi ya taifa kwa ujumla wake. Jeshi la polisi ni taasisi muhimu katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Ni jambo baya kwa raia kuanza kuonyesha kukosa imani na utendaji kazi wa baadhi ya askari katika jeshi hilo. Mathalan, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa raia juu ya matendo maovu ya baadhi ya polisi ikiwamo kubambikiwa kesi. Isitoshe, baadhi ya polisi wametuhumiwa kufanya vitendo vya kihalifu ikiwamo hili la hivi karibuni la mauaji ya wafanyabiashara. Itakumbukwa, huko nyuma, katika mazingira ya kutatanisha, kulitokea mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa kule Ulanga na polisi waliohusika katika kadhia ile walishaiaminisha jamii kuwa walikuwa ni majambazi, jambo ambalo halikuwa kweli. 
Katika hili, umma lazima uwe na imani isiyo na mashaka juu ya Jeshi lake la polisi. Kwamba raia anapokutana na polisi asiwe na chembe ya shaka kuwa anayekutana naye aweza kuwa mhalifu. Hatua ya IGP Mangu kulifumua jeshi hilo bila shaka imelenga kwenye kuleta mabadiliko ndani ya Polisi. Wakati tukisubiri kuona, mtandao wa Mjengwablog.com unaiona habari hii kuwa ni ya kuleta matumaini, na hivyo inaipa nafasi ya kwanza kwa uzito.

2. Polisi sita wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji
Hii ni habari inayopewa uzito wa pili, ingawa mhariri wa moja ya magazeti ameweka kichwa cha habari cha kuwatia hatiani kuwa wamefikishwa mahakamani kwa mauaji. Hili si sahihi, bali hadi sasa wanatuhumiwa kwa mauaji. Ni mahakama ndio yenye kazi ya kuthibitisha kama wameua au la. Hata hivyo, habari kwamba polisi wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara kwa mara nyingine inaleta mashaka kwa jamii juu ya baadhi ya askari waliomo katika jeshi hilo. Swali la kujiuliza hapa, ni mfumo gani unaotumika katika kusajili askari wetu kwenye jeshi la polisi? Isije ikawa si mfumo imara unaopelekea hata wenye rekodo za uhalifu kuingia kwenye jeshi hilo.

3. Watu wanane matatani kwa kupora mali ya misheni

Hii ni habari ya tatu kwa ukubwa kwa mujibu wa mtandao wamjengwablog.com. Imetokea huko Morogoro. Watuhumiwa wamekiri kuhusika na ujambazi huo uliofanyika kwenye eneo la kanisa kwa kuwavamia watumishi wa misheni wanaosemwa kuwa ni raia wa Uingereza. Moja ya vitu walivyoporwa ni bunduki. Jambo hilo pia ni la ajabu. Bunduki imefuata nini misheni?

Usikose kusoma pia, habari kubwa ya michezo kwa siku ya leo na katuni bora kwa siku ya leo. Ni kwenye http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment