Wednesday 30 December 2015

[wanabidii] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. Magufuli ateua Makatibu Wakuu

Hii ni habari inayochukua nafasi ya kwanza kwa mujibu wa mtandao wamjengwablog.com. Inahusu Serikali na utawala wa nchi. Baada ya kukamilisha zoezi la kuteua mawaziri wake, hatua hii ya pili ya kuteua Makatibu Wakuu nayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kutokana na umuhimu wake inapozungumziwa ufanisi katika utendaji wa shughuli za Serikali. 
Kimsingi, kwa kiasi kikubwa Makatibu Wakuu ndio Serikali yenyewe. Nchi inaweza kwenda bila Mawaziri, lakini, ni vigumu kwa nchi kwenda bila Makatibu Wakuu. 
Tumeona, Rais Magufuli amefanya uteuzi uliosheheni wachapa kazi. Na katika maeneo yenye kuhusiana na kupambana na uhalifu ikiwamo ujangili, Rais ameteua Makatibu Wakuu wenye weledi pia kwenye masuala ya kijeshi.

Ni safu ya Makatibu Wakuu yenye kuonyesha dhamira ya kusonga mbele kiuchumi. Angalizo ni kwa kutorudi kwenye mazoea ya baadhi ya wanasiasa kuingilia majukumu ya Makatibu Wakuu katika utendaji wa kazi zao. Wakati yawezekana Waziri au Naibu Waziri wake wakawa ni wenye majimbo, Katibu Mkuu hana jimbo. Jimbo lake ni Tanzania. Anapaswa kuelekeza rasilimali za nchi kwa kuangalia maslahi ya nchi na si ya mwanasiasa na jimbo lake la uchaguzi.

Hatua iliyobaki muhimu ni uteuzi wa Wakurugenzi wa Idara mbalimbali ikiwamo taasisi na mashirika ya umma. Katika wakati tulio nao, ingelikuwa vema tukayapa mgongo mazoea ya uteuzi, badala yake Serikali kuajiri Wakurugenzi kwa kutangaza nafasi za kazi. Na Katibu Mkuu wa Wizara hapa angepaswa kuwa mshiriki mkuu katika zoezi la kuchambua waombaji wenye sifa stahiki katika kujaza nafasi za Wakurugenzi na ambao kimsingi, ndio watakaomsaidia Katibu Mkuu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

2. Kashfa yazikumba MCC, Symbion

Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili kwa ukubwa. Wakati MCC inaweka masharti magumu kwa nchi masikini kama Tanzania katika kutoa misaada yake ya maendeleo, imeripotiwa, hata MCC na symbion nao wamo katika kashfa ya ndani katika utendaji wa kazi zao. Soma zaidi taarifa hii kwenyehttp://mjengwablog.com

3. Serikali lawamani kuchelewesha pembejeo
Imeripotiwa kutoka Nachingwea, kuwa wakati msimu wa kilimo umeshawadia, wakulima bado hawajapatiwa ruzuku ya pembejeo za kilimo ikiwamo mbolea. Tafsiri ya habari hii ni kuwa, kama hali hii ya Nachingwea iko mahali pengine nchini, basi, tusije tukashangaa itakapokuja habari kuwa wananchi Nachingwea na kwingineko wamekumbwa na njaa. Ni wakati wa Waziri Mwigulu Nchemba kufanya ziara ya ' kushtukiza' kwa wenye wajibu wa kuwafikishia wakulima pembejeo.

Usikose pia kuangalia katuni bora ya leo na mbili nyingine na habari bora ya michezo kwa siku ya leo. Ni kwa kutembelea; http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment