Changamoto ya uzalishji umeme ni umwagiliji- muhongo
Na Ikungi
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema uzalishaji mdogo wa umeme wa maji nchini zaidi unatokana na shughuli za kilimo cha umwagiliaji na sio mabadiliko ya Tabia nchi.
Profesa Muhongo ameyasema hayo katika ziara ya siku nne (4) aliyoifanya kutembelea vyanzo vya umeme wa maji (HEP) vilivyopo katika mikoa mbalimbali nchini.
Jumla ya mitambo yetu yote (installed capacity) ina uwezo wa kuzalisha MW 561.24 za umeme. Lakini, uzalishaji wa jumla kwa sasa ni MW 110 tu ambayo ni takribani asilimia 20 ya uwezo wake? alisema Profesa Muhongo.
Aliongeza kuwa kuongezeka kwa kilimo cha umwagiliaji katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Morogoro ni sababu kubwa inayoathiri uzalishaji wa umeme wa maji nchini.
Umeme wa maji unaozalishwa katika mabwawa yetu yote ni asilimia 20 tu ya uwezo wa uzalishaji umeme wa mabwawa yetu? alisema mwanajiolojia mbobevu.
Toka jumapili hadi leo jumatano (16.12.2015) nimetembelea Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani,Mtera, Kihansi na Kidatu na kugundua kwamba tatizo sugu ni umwagiliaji na sio mabatiliko ya tabia nchi? alisisitiza.
Hivi karibuni Tanzania imeanza kutumia umeme unaotokana na uchakataji wa gesi ya Mtwara na hivyo kupunguza tatizo la upatikananji wa umeme nchini.
Mara tu baada ya kula kiapo, Waziri na Naibu wake wenye dhamana ya Nishati na Madini, walifuata nyayo za abos wao, Rais Dk. Magufuli na kuanza kushughulikia tatizo la nishati ya umeme ili kuleta uthabiti ndani ya muda mfupi.kwa hisani ya Jf
0 comments:
Post a Comment