Wednesday 4 February 2015

[wanabidii] Re: RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE

Kama aliyesema hivyo ni malaika basi yuko sahihi; ila kama ni binadamu kama mimi hiyo kauli haina mashiko. Yeye ana uhakika, mauno gani ya kumfanya aweze kujua hatima ya hii nchi kwa miezi kadhaa ijayo. Kiukweli, binadamu hayuko sahihi kwa 100/% kuweza kujua yeye mwenyewe baada ya dakika kadhaa nini kinaweza mtokea.
Hali halisi ni kwamba nchi hii ilikwisha yumba tangu rais wa awamu ya pili katika muhula wa pili wa uongozi wake na hali imeendelea kuwa mbaya zaidi hadi huyu wa awamu ya nne anaongea hivyo akijua hana cha kupoteza kwa upande wake. Na kwa vipindi vyote hivyo CCM imekuwa ikiongoza dola hadi hivi sasa na hakuna cha kujivunia na mbaya zaidi kufanya bajeti ya nchi yetu kuwa tegemezi tuuu hadi hivi sasa mtu anasimama bungeni kutoa mchanganuo wa bajeti ya nchi; ....%pato la ndani, na ....% nchi wahisani. Swali la kujiuliza, hivyo hao wahisani ni ndugu zetu? Hii ni aibu kwa nchi yenye utajiri kama Tanzania ambayo ningetegemea yenyewe ndiyo ingekuwa kinara wa kuwasaidia wengine. Chini ya uongozi wa CCM nchi bado ni ombaomba ile ombaomba na kukopa hovyo hovyo.
Kwa hili la bajeti tegemezi, wizi na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa; sheria zinazo wakandamiza walio dhaifu na kuwaacha walio imara bado tu nchi haijayumba na mtu kuja kutuambia itayumba! Nafikiri huyu hana nia nzuri na watanzania.

On Monday, February 2, 2015 at 10:39:13 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:

RAIS AJAYE ASIPOTOKA CCM, NCHI ITAYUMBA - KIKWETE
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete amewaagiza viongozi wa chama hicho kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Dkt Kikwete ametoa agizo hilo katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo zimefanyika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho.

Akimnukuu mwalimu Nyerere, amesema kuwa Rais wa Tanzania anaweza kutoka chama chochote lakini Rais bora ni lazima atoke CCM hivyo amewataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanafanya mikutano na kuwatembelea wananchi ili kujua matatizo yao kama anavyofanya Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdulrahman Kinana.

Aidha ameonya kuwa wana CCM wanatakiwa kutambua kuwa endapo CCM haitashinda, nchi itayumba na huenda CCM isibaki kama ilivyo, kwa hiyo ni jukumu lao kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani kwa kila jitihada.

Amewataka wawe makini wakati wa kuteua wagombea hususani katika nafasi ya urais ili wapate mgombea mwenye uwezo wa kuendelea kujenga umoja ndani ya chama na taifa kwa ujumla, na pia mwenye uwezo wa kuongoza Tanzania na watanzania wakamkubali.

"Msifanye makosa katika kupata mgombea, chagueni mgombea atakayekubalika na mwenye uwezo, hata kama yupo lakini hajajitokeza, siyo vibaya kumshawishi kama mimi nilivyoshawishiwa…" amesema Kikwete.

Amewataka viongozi wa chama hicho kuwashawishi wanachama wote kujiandikisha katika daftari la kupiga Kura kwa mfumo wa BVR ili waweze kushiriki uchaguzi huo wakiwa na vitambulisho vipya.

Amesema "Kwa mahesabu yaliyopo CCM ina wananchama zaidi ya Milion 6, tukiwaongeza na hao kama milioni 2 hivi, itakuwa million 8, tayari tutakuwa na mtaji wa Kura million 8 za kuanzia, na hao million 8 kila mmoja ana mpenzi, akimshawishi mpenzi wake kuipigia CCM tutakuwa na kura million 16, ambapo tutaweza kumshinda mtu yoyote……"

Ameongeza kuwa "CCM ni chama cha kuongoza dola, siyo chama cha michezo wala muziki, mambo ya muziki Kapten Komba anatosha, yupo na Diamond pia, wanatosha hao, lakini sisi tuhakikishe CCM inaendelea kuogoza dola"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment