Wednesday 4 February 2015

RE: [wanabidii] RAISI MTALAJIWA 2015 NI EDWARD LOWASSA

Tukizingatia ukweli kabisa... tukisema Lowassa Fisadi kwa kigezo cha Richmond tunamuonea. Waziri mkuu hana uwezo wa kuunda mradi hewa kama ule rais asiwe coordinator.....ntamshangaa sana Lowassa akikubali kufa kwa hili la ufisadi wakati anajua hauhisiki.

'Ambokege Benard M' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mambo mengine ni kero kwa kweli,
Hivi tunamtaka Rais mwenye sura nzuri au tunayedhani kuwa ataibadilisha nchi hii iliyo jaa rasilimali lukuki kwa ajili ya kuuimarisha uchumu wa nchi na wananchi wake. Sio vema sana kufika mahali kumnadi mtu kwa kutoa matusi kwa watu wengine.
Hapa hatuangalii sura Bali Uwezo wa mtu. Tukiangalia sura hata Lowasa mwenyewe hafai maana ndani ya chama Kuna wenye sura nzuri kuliko yeye.
Swala la mtu kuumwa ni nyeti sana, labda utufafanulie anacho umwa, na je nani ndani ya chama chako aliye mzima?
Tusilete hoja za kijinga hapa. Mwaka 2005 mambo yalikuwaje na leo nchi iko na hali gani!
Kama tukisema kila mtu aseme anachotaka katika jukwaa hili naamini ama wadhibiti wa mawasiliano nchini watufunga hili jukwaa. Tuwe makini lakini zaidi nikiamini wengi wa watumiaji wa mtandao huu ni watu walioenda shule ni vema tukawa na staha katika matumizi ya lugha na hasa ni vema kujiepusha na matusi hasa kwa wale ambao wameonyesha nia lakini hatuwapendi.

Yangu ni hayo, tuchunge ndimi zetu kupitia maandishi yetu maana kike ukiandikacho ndicho kitokacho mdomoni kwako kupitia ukurasa huu.

Nawasilisha!


ABM

From: 'Hezron Kaaya' via Wanabidii
Sent: ‎2/‎4/‎2015 9:56
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RAISI MTALAJIWA 2015 NI EDWARD LOWASSA

Emma chunga sana ulimi wako.kauli uliyoitumia kwa hao viongozi sio nzuri.Toa hoja acha matusi unamchafulia hata huyo unayemtaka.


On Monday, January 26, 2015 9:01 PM, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:


Tukiendelea kufumbia macho ufisadi na kuwatukuza wanaotufisidi tutaishia kutawaliwa na akina Sauli.
em

2015-01-26 12:00 GMT-05:00 'frank patrick materu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Mungu hana demokrasia. Yeye ana theokrasia. (Theocracy). Wana wa Israel walitaka mfalme, wakaangalia sura wakapewa Sauli na akachukua mali zao na yale yaliyo mazuri kwao, akachukua rushwa na kuwatia katika kazi zake mwenyewe na kuwafanya watumwa wake. "Wakalia siku ile kwa sababu ya mfalme waliojichagulia, Bwana asiwajibu…."[1 Sam 8:10-23]
Mungu huwapa watu kiongozi sawasawa na mioyo yao. Je, mioyo ya Watanzania ikoje mbele za Mungu?
       Kukumbuka kuwa ni Mungu aliye Hai na Yeye peke yake ambaye naweza kubadilisha jinsi mambo yalivyo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment