Baba wa Taifa alisema "Pokea na kula hela zake lakini ikifika wakati wa Kura usimpigie au kumchagua!!"
Ataona kupigiwa makofi na watu kujaa halafu kura NIL lakini walimpamba na kura hawakumpa. Ni fundisho kwa vizee vinavyong'ang'ania madaraka. Abaki Monduli akiwafundisha nduguze kwa lugha ya kwao wafuge kisasa, waache kuhamahama na kuharibu amani na uchumi wa wenzao. Toka Monduli, simanjiro, Loliondo, ngorongoro na maelfu ya mifugo to Morogoro, Kilosa-Kilombero, Mgeta Juu milimani
kukausha mto Ruvu, hadi kisarawe-Rufiji, Kilwa-Lindi au Iringa-Mbararli, Mbeya-Sumbawaka kote huko kulishia mashamba, kupiga watu, kuua na kuharibu vyanzo vya maji eti wanaonewa hawana ardhi kwao. Huko simanjiro na ndani ya mbuga hifadhi ya ngorongoro-wanalima kwa plough na trekta. Hela za Tanzanite mererani na vijiji vyao wanachimba madini-wanalimbikiza mifugo. Wanakaribisha wenzao wa Kenya wanajazana NCAA na Loliondo na maeneo mengine. ardhi yao inakuwa kame mifugo imezidi na wanalima wanyamapori wanakosa chakula nao waliwekwa nao kwa vile hawalimi sasa wanalima hawanunui mahindi tena. Hata mkulima hawezi kuachwa analima misitu hifadhi anafukuzwa na kuadhibiwa. Wao wataua watashinda kesi si wanahela za kuhonga? Ranchi za ufugaji kisasa zipo kibao na misaada ya wazungu kuwasaidia kujikimu kibao ila kubadirika utata. Hata ardhi ilikopimwa makwao hawazingatii. Kila mtu akae kwao na atumie ardhi sustainably hakuna kuhamahama kwa kilimo wala mifugo. Wabunge
wasioonyesha mfano bora katika kusaidia kuboresha maisha wa watuwao majina yao yasipitishwe na vyama vyao. Huwezi ukaendelea kumchagua Diwani na Mbunge ambaye atakuwa anaandamana tu daima kupinga serikali ila sio yeye kuamka kuingia mtaani aishipo na kwenda jimboni kuhamasisha watu wake na kuongoza mabadiliko. Mbunge na diwani wanaona kinyesi kinatiririshwa na wakazi mtaani kwake na kutupa taka ngumu ndani ya mitaro tena mipya ya halmashauri-naye anaruka kinyesi haongei na wanaotiririsha; mbunge anahudhuria ndoa ya msichana mtoto wa kiaka 12 kwa libaba la miaka 68 naye anakuwa ngeni rasmi!? Anaona raia wanaziba njia na kuweka usalama mdogo moto ukiwaka-anapita anawasalimia kwa kuwachekea na kuwapungia mkono. Unahangaika na Urais, uwaziri wakati pale ulipo hatuoni tofauti kimaendeleo kwa raia wako-Hufai!!
--------------------------------------------
On Tue, 10/2/15, 'godfred mbanyi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, 10 February, 2015, 14:hagua12
Declare interest first! Upo kundi gani??? Membe, Makamba
Jnr, Pinda, au???
--------------------------------------------
On Tue, 2/10/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
wrote:
Subject: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge
wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, February 10, 2015, 1:10 PM
Lowassa
anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni
aliyonayoNa
Mwandishi MaalumMAGAZETI
kadhaa yatolewayo kila siku nchini, Jumatatu Februari 9,
2015, yaliongozwa na habari kuu kuhusu
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba 'anang'ara
katika mbio za urais'.Katika habari hiyo, magazeti hayo
yote yalinukuu kauli za wabunge saba wa CCM wanazodaiwa
kuwa
walizitoa katika hafla iliyotajwa kuwa "ya aina yake"
ya
chakula cha jioni, Jumamosi iliyopita.Lakini katika hali
isiyokuwa ya
kawaida, hafla hiyo kamwe haikutaja ilikofanyika zaidi ya
kuelezwa tu kuwa "nyumbani kwa kigogo mmoja wa CCM",
Kilimani mjini Dodoma.Kwa
nini kigogo huyo alifichwa utadhani hafla hiyo ilikuwa
haramu au kwamba iliambatana na vitendo vya
kihalifu?Wabunge waliotajwa na kunukuliwa
wakizungumza ni Deogratius Ntukamazina (Ngara), Diana
Chilolo (Viti Maalum – Singida), Stephen Ngonyani au
'Profesa Maji Marefu' (Korogwe Vijijini) na Mary
Chatanda ambaye pia wa Viti Maalum (Tanga) na Katibu wa
CCM
wa Mkoa wa Singida.Wengine ni
Kapteni John Komba (Mbinga Magharibi), Mussa Azzan Zungu
(Ilala) na Yahya Kassim Issa ambaye ni mbunge wa Chwaka,
Zanzibar.Wote walinukuliwa
wakimwelezea Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani
kwamba "ni kiongozi bora, kiongozi makini, chaguo la
Watanzania" na kadhalika.Ntukamazina kwa mfano alisema:
"Kule kwangu Ngara wananiuliza yule waziri mkuu
aliyeleta
hizi shule za kata yuko wapi? Mimi nawajibu atarudi na
kila
mtu mitaani anataja jina lako, kwa hiyo sauti ya wengi ni
sauti ya Mungu".Wasiwasi
kuhusu habari hiyo
Kila gazeti, licha ya habari hiyo kuandikiwa ukumbini na
isiyokuwa ya uchunguzi, yote hayakutaja jina la mwandishi
kwa kusema ni "Mwandishi Wetu, Dodoma", halafu zote
zinafanana kwa kila kitu katika mambo yafuatayo:
(i) Kutotaja jina la kigogo wa CCM aliyeandaa hafla hiyo
kuwa ni nani;(ii) Idadi ya
wabunge waliohudhuria hafla hiyo imetajwa na kila gazeti
kuwa 150 utadhani kila mwandishi aliwahesabu au
walihesabiwa
mlangoni, kisha hesabu yao ikatangazwa hadharani;(iii)
Wabunge waliotajwa kwenye
magazeti hayo kuwa waliongea ni walewale; na(iv) Wabunge
hao pia wametajwa kwa
mtiririko uleule, nukuu zilezile, namna ileile huku kila
kitu kikiwa kinafanana kama barua iliyopigwa photocopy na
kusambazwa huko kote;Katika
hali hiyo, yapo mambo kadhaa ya kutilia wasiwasi kwa
wasomaji makini ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:
(i) Kuna kila mwelekeo wa kuwa hafla hiyo iliandaliwa kwa
agizo au kwa gharama za Lowassa mwenyewe;(ii) Kuna kila
mwelekeo wa kuwa
hafla hiyo iliandaliwa maalum kwa ajili ya kampeni za
urais
za Lowassa, lakini ukakosekana umakini wa kutosha ili
kufanikisha siri iliyolenga kuwadanganya Watanzania;(iii)
Wabunge waliozungumza
inaelekea kwamba waliandaliwa maalum, halafu inawezekana
kuwa maneno waliyozungumza walipewa au walielekezwa na
Lowassa mwenyewe ama na washauri wake; na(iv) Habari hiyo
imeandikwa na
mwandishi mmoja, kisha ikasambazwa katika magazeti hayo
yote
kwa gharama za mwanasiasa na mbunge huyo ikiwa ni sehemu
ya
kampeni zake za urais.Ili
kuthibitisha vinginevyo, magazeti hayo inabidi yajibu
maswali makubwa yafuatayo kwa wasomaji wake ambao ni
pamoja
na mimi kwamba ilikuwaje habari hiyo ifanane kwa zaidi ya
asilimia 75 kuhusu:(i)
Mpangilio wa wabunge walivyozungumza katika hafla
hiyo?(ii) Ilikuwaje idadi ya
wabunge waliozungumza na kunukuliwa na magazeti hayo yote
iwe ileile?(iii) Ilikuwaje
mtiririko wa habari hiyo ufanane kiasi hicho kwa magazeti
yote na kuonekana kuwa imeandikwa na mwandishi mmoja kama
kweli ni tofauti?(iv) Kama
habari hiyo iliandikwa na waandishi tofauti, wapi
walikokutana, kisha wakakubaliana kuwa nukuu zao zote ziwe
ni zilezile?(v) Wapi
waandishi hao walikokutana na kukubaliana kuwa vilevile
mtiririko wa nukuu zote hizo ufanane kama mayai?Mfano
ninaomaanisha ni kama pale
Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina aliponukuliwa na
magazeti hayo yote akisema:"…Oktoba tutakuwa na
uchaguzi
mkuu wa kumchagua kiongozi atakayesukuma mbele nchi
yetu."Sote tunafahamu chama
chetu bado hakijatangaza utaratibu, lakini sisi wabunge
marafiki zako tunakuomba muda ukifika uchukue fomu kwa
sababu unatosha".Nukuu hiyo
ya neno kwa neno ipo katika kila gazeti, halafu imeandikwa
kwa staili ileile na kwa aya zinazofanana utadhani
ilipigwa
'photocopy' na kusambazwa huko kote.Mbali na hapo,
habari hiyo pia
inafanana kwa kila kitu katika magazeti hayo yote ambapo,
pale palipoandikwa bila ya kunukuu neno kwa neno inakuwa
hivyo kwa kila gazeti, na pia kila paliponukuliwa (quoted)
napo panakuwa vilevile utadhani pamefanyiwa
'scanning'.Aidha,
magazeti hayo yote yamemwandika Chilolo kwa aya moja yenye
maneno 22 tu kama ifuatavyo:"Kwa upande wake, Mbunge wa
Viti
Maalum, Diana Chilolo (CCM) aliunga mkono kauli ya
Ntukamazina kwa kusema Lowassa ni chaguo la
wengi".Wasomaji wote makini walioisoma
habari hiyo ndani ya magazeti hayo au baadhi yake hakuna
mashaka kwamba waligundua kuwa ilitengenezwa maalum kwa
ajili ya kumbeba Lowassa katika harakati zake za
urais.Pamoja na ukweli kuwa
kila mwanasiasa anayetafuta madaraka ya uongozi wa umma
huwa
na njia zake mwenyewe za kutafuta ushindi, lakini mbinu
hiyo
ya Lowassa haiwezi kuwadanganya walengwa ambao hasa ni
viongozi waandamizi wa CCM.Wabunge aliowatumia kutaka
kufanikisha mkakati wake huo wa kuitisha CCM ili iogope
kuwa
isipomteua kugombea urais itaondoshwa madarakani na
wapinzani, kwamba asipoteuliwa yeye ili kusimama katika
kinyang'anyiro hicho basi chama hicho kitashindwa kuna
wengine wamekubali kutumika kiasi hicho kwa sababu
inaelezwa
kwamba ana pesa nyingi.Ukimwondoa mtu kama Ntukamazina
ambaye ameshasema kuwa hagombei tena ubunge mwaka huu,
Chatanda anajipanga kutaka kugombea ubunge wa jimbo la
Korogwe Mjini huku Komba au 'Maji Marefu' nao
wakikabiliwa na hali ngumu majimboni kwao.Ili waweze kupata
ushindi kwanza
kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, wabunge hao inabidi
kila mmoja awe na kiwango kikubwa kabisa cha pesa za
kampeni, fedha ambazo hakuna hata mmoja aliyenazo.Wote
wanategemea kiinua mgongo
ambacho kila mmoja atalipwa na serikali baada ya muda wao
wa
sasa kumalizika kiasi cha miezi mine ijayo, lakini
wanafahamu kwamba hazitoshi kuwapa ushindi
wanaoutafuta.Kwa mfano, Komba
amekuwa akitishiwa hadi kufilisiwa na benki anakodaiwa
mamia
ya mamilioni ya fedha alizokopa pamoja na riba, deni
linalotishia hadi kukamatwa kwa mali zake kwa sababu
ameshindwa kulipa.Wote
walijitolea mhanga kumsifia hadharani mbele yake mwenyewe
siyo kwa sababu eti wanamuunga mkono kwelikweli, bali
walifanya hivyo kwa sababu wanayataka mamilioni ya pesa
zake.Wanataka kumdanganya kwa
sababu wanataka fedha hizo ili nao pia wakahangaikie
ubunge
kwa muhula mwingine kwenye majimbo yao. Walikuwa hawamsifu
eti kwa sababu anatakiwa kiasi hicho kuwa Rais wa Serikali
ya Awamu ya Tano.Wote
wananyemelea mamilioni ya fedha anazodaiwa kufadhiliwa au
kwa yeye mwenyewe kujikusanyia kwa namna moja ama
nyingine.NI MTAZAMO WANGU
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment