lutunwa et al hawana hoja wana aurgue with no solutions.....nisawa na wanung"nunikaji flani hv......sasa unasem huyu hafai unaambiwa mtaje anaefaa huna....basi tulia tu usitoe hja dhaifu.......achana nao kaka Kaaaya sisi tusonnge mbele
From: 'Hezron Kaaya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, February 10, 2015 6:13 AM
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
Uchambuzi wako haukubaliki hata kidogo kwa vile inaonyesha una jina jingine moyoni mwako unalolipenda kwa hiyo tukio hilo linakukera .Hivi karibuni tu tutaona matukio ya aina hiyo mengi sasa nayo utasemaje.Ni vema tuache watu wajizatiti wanavyoweza lakini waamuzi ni wananchi wenyewe.
On Tuesday, February 10, 2015 3:39 PM, Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com> wrote:
Lesian,
Haina haja kuwataja hapa jukwaani, ila what you need to know ni kwamba wapo watanzania wengi wasafi ambao wanaweza kuongoza nchi na ultmately tukawaona ni wakombozi. sio hiyo mijizi. Reject ya Nyerere.
2015-02-10 15:08 GMT+03:00 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
--mzeeemhigo mlete mnaedhan kuingia ikulu badala ya lowasa tujue give us altenative president to be ambaye ni msafi msiwe mnaongea utopianism jamani.........mleteni, mtajeni mwenye sifa zenu, clean and smart ambaye watanzania watamkubalia kuongoza nchi kwa kura nyingi au lipumba, sema kama unamtaka dk slaaa, ama kaka yetu Mbatia....semeni
From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, February 10, 2015 2:57 PM
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
Huu ndio ubovu wa kutumia mitandao kuusaka urais. Mtandao huu sasa uunakosa watu makini kama waliokuwemo ndani ya mtandao wa 2005.
Mambo kama haya yalikuwepo 2005 lakini umakini wa waliotumiwa sasa haupo.
najua sasa kuwa huenda taifa hili lisipokuwa makini tutampata mhuni kuingia ikulu.
Mungu apishe mbali
--------------------------------------------
On Tue, 2/10/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Lowassa anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni aliyonayo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, February 10, 2015, 1:10 PM
Lowassa
anadanganywa na wabunge wanaonyemelea mamilioni
aliyonayoNa
Mwandishi MaalumMAGAZETI
kadhaa yatolewayo kila siku nchini, Jumatatu Februari 9,
2015, yaliongozwa na habari kuu kuhusu
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwamba 'anang'ara
katika mbio za urais'.Katika habari hiyo, magazeti hayo
yote yalinukuu kauli za wabunge saba wa CCM wanazodaiwa kuwa
walizitoa katika hafla iliyotajwa kuwa "ya aina yake" ya
chakula cha jioni, Jumamosi iliyopita.Lakini katika hali isiyokuwa ya
kawaida, hafla hiyo kamwe haikutaja ilikofanyika zaidi ya
kuelezwa tu kuwa "nyumbani kwa kigogo mmoja wa CCM",
Kilimani mjini Dodoma.Kwa
nini kigogo huyo alifichwa utadhani hafla hiyo ilikuwa
haramu au kwamba iliambatana na vitendo vya kihalifu?Wabunge waliotajwa na kunukuliwa
wakizungumza ni Deogratius Ntukamazina (Ngara), Diana
Chilolo (Viti Maalum – Singida), Stephen Ngonyani au
'Profesa Maji Marefu' (Korogwe Vijijini) na Mary
Chatanda ambaye pia wa Viti Maalum (Tanga) na Katibu wa CCM
wa Mkoa wa Singida.Wengine ni
Kapteni John Komba (Mbinga Magharibi), Mussa Azzan Zungu
(Ilala) na Yahya Kassim Issa ambaye ni mbunge wa Chwaka,
Zanzibar.Wote walinukuliwa
wakimwelezea Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani
kwamba "ni kiongozi bora, kiongozi makini, chaguo la
Watanzania" na kadhalika.Ntukamazina kwa mfano alisema:
"Kule kwangu Ngara wananiuliza yule waziri mkuu aliyeleta
hizi shule za kata yuko wapi? Mimi nawajibu atarudi na kila
mtu mitaani anataja jina lako, kwa hiyo sauti ya wengi ni
sauti ya Mungu".Wasiwasi
kuhusu habari hiyo
Kila gazeti, licha ya habari hiyo kuandikiwa ukumbini na
isiyokuwa ya uchunguzi, yote hayakutaja jina la mwandishi
kwa kusema ni "Mwandishi Wetu, Dodoma", halafu zote
zinafanana kwa kila kitu katika mambo yafuatayo:
(i) Kutotaja jina la kigogo wa CCM aliyeandaa hafla hiyo
kuwa ni nani;(ii) Idadi ya
wabunge waliohudhuria hafla hiyo imetajwa na kila gazeti
kuwa 150 utadhani kila mwandishi aliwahesabu au walihesabiwa
mlangoni, kisha hesabu yao ikatangazwa hadharani;(iii) Wabunge waliotajwa kwenye
magazeti hayo kuwa waliongea ni walewale; na(iv) Wabunge hao pia wametajwa kwa
mtiririko uleule, nukuu zilezile, namna ileile huku kila
kitu kikiwa kinafanana kama barua iliyopigwa photocopy na
kusambazwa huko kote;Katika
hali hiyo, yapo mambo kadhaa ya kutilia wasiwasi kwa
wasomaji makini ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:
(i) Kuna kila mwelekeo wa kuwa hafla hiyo iliandaliwa kwa
agizo au kwa gharama za Lowassa mwenyewe;(ii) Kuna kila mwelekeo wa kuwa
hafla hiyo iliandaliwa maalum kwa ajili ya kampeni za urais
za Lowassa, lakini ukakosekana umakini wa kutosha ili
kufanikisha siri iliyolenga kuwadanganya Watanzania;(iii) Wabunge waliozungumza
inaelekea kwamba waliandaliwa maalum, halafu inawezekana
kuwa maneno waliyozungumza walipewa au walielekezwa na
Lowassa mwenyewe ama na washauri wake; na(iv) Habari hiyo imeandikwa na
mwandishi mmoja, kisha ikasambazwa katika magazeti hayo yote
kwa gharama za mwanasiasa na mbunge huyo ikiwa ni sehemu ya
kampeni zake za urais.Ili
kuthibitisha vinginevyo, magazeti hayo inabidi yajibu
maswali makubwa yafuatayo kwa wasomaji wake ambao ni pamoja
na mimi kwamba ilikuwaje habari hiyo ifanane kwa zaidi ya
asilimia 75 kuhusu:(i)
Mpangilio wa wabunge walivyozungumza katika hafla
hiyo?(ii) Ilikuwaje idadi ya
wabunge waliozungumza na kunukuliwa na magazeti hayo yote
iwe ileile?(iii) Ilikuwaje
mtiririko wa habari hiyo ufanane kiasi hicho kwa magazeti
yote na kuonekana kuwa imeandikwa na mwandishi mmoja kama
kweli ni tofauti?(iv) Kama
habari hiyo iliandikwa na waandishi tofauti, wapi
walikokutana, kisha wakakubaliana kuwa nukuu zao zote ziwe
ni zilezile?(v) Wapi
waandishi hao walikokutana na kukubaliana kuwa vilevile
mtiririko wa nukuu zote hizo ufanane kama mayai?Mfano ninaomaanisha ni kama pale
Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina aliponukuliwa na
magazeti hayo yote akisema:"…Oktoba tutakuwa na uchaguzi
mkuu wa kumchagua kiongozi atakayesukuma mbele nchi
yetu."Sote tunafahamu chama
chetu bado hakijatangaza utaratibu, lakini sisi wabunge
marafiki zako tunakuomba muda ukifika uchukue fomu kwa
sababu unatosha".Nukuu hiyo
ya neno kwa neno ipo katika kila gazeti, halafu imeandikwa
kwa staili ileile na kwa aya zinazofanana utadhani ilipigwa
'photocopy' na kusambazwa huko kote.Mbali na hapo, habari hiyo pia
inafanana kwa kila kitu katika magazeti hayo yote ambapo,
pale palipoandikwa bila ya kunukuu neno kwa neno inakuwa
hivyo kwa kila gazeti, na pia kila paliponukuliwa (quoted)
napo panakuwa vilevile utadhani pamefanyiwa
'scanning'.Aidha,
magazeti hayo yote yamemwandika Chilolo kwa aya moja yenye
maneno 22 tu kama ifuatavyo:"Kwa upande wake, Mbunge wa Viti
Maalum, Diana Chilolo (CCM) aliunga mkono kauli ya
Ntukamazina kwa kusema Lowassa ni chaguo la wengi".Wasomaji wote makini walioisoma
habari hiyo ndani ya magazeti hayo au baadhi yake hakuna
mashaka kwamba waligundua kuwa ilitengenezwa maalum kwa
ajili ya kumbeba Lowassa katika harakati zake za
urais.Pamoja na ukweli kuwa
kila mwanasiasa anayetafuta madaraka ya uongozi wa umma huwa
na njia zake mwenyewe za kutafuta ushindi, lakini mbinu hiyo
ya Lowassa haiwezi kuwadanganya walengwa ambao hasa ni
viongozi waandamizi wa CCM.Wabunge aliowatumia kutaka
kufanikisha mkakati wake huo wa kuitisha CCM ili iogope kuwa
isipomteua kugombea urais itaondoshwa madarakani na
wapinzani, kwamba asipoteuliwa yeye ili kusimama katika
kinyang'anyiro hicho basi chama hicho kitashindwa kuna
wengine wamekubali kutumika kiasi hicho kwa sababu inaelezwa
kwamba ana pesa nyingi.Ukimwondoa mtu kama Ntukamazina
ambaye ameshasema kuwa hagombei tena ubunge mwaka huu,
Chatanda anajipanga kutaka kugombea ubunge wa jimbo la
Korogwe Mjini huku Komba au 'Maji Marefu' nao
wakikabiliwa na hali ngumu majimboni kwao.Ili waweze kupata ushindi kwanza
kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, wabunge hao inabidi
kila mmoja awe na kiwango kikubwa kabisa cha pesa za
kampeni, fedha ambazo hakuna hata mmoja aliyenazo.Wote wanategemea kiinua mgongo
ambacho kila mmoja atalipwa na serikali baada ya muda wao wa
sasa kumalizika kiasi cha miezi mine ijayo, lakini
wanafahamu kwamba hazitoshi kuwapa ushindi
wanaoutafuta.Kwa mfano, Komba
amekuwa akitishiwa hadi kufilisiwa na benki anakodaiwa mamia
ya mamilioni ya fedha alizokopa pamoja na riba, deni
linalotishia hadi kukamatwa kwa mali zake kwa sababu
ameshindwa kulipa.Wote
walijitolea mhanga kumsifia hadharani mbele yake mwenyewe
siyo kwa sababu eti wanamuunga mkono kwelikweli, bali
walifanya hivyo kwa sababu wanayataka mamilioni ya pesa
zake.Wanataka kumdanganya kwa
sababu wanataka fedha hizo ili nao pia wakahangaikie ubunge
kwa muhula mwingine kwenye majimbo yao. Walikuwa hawamsifu
eti kwa sababu anatakiwa kiasi hicho kuwa Rais wa Serikali
ya Awamu ya Tano.Wote
wananyemelea mamilioni ya fedha anazodaiwa kufadhiliwa au
kwa yeye mwenyewe kujikusanyia kwa namna moja ama
nyingine.NI MTAZAMO WANGU
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:
Post a Comment