Sunday, 30 June 2013

Re: [wanabidii] Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikanunua suti na viatu vilivyonibana!"



Waliona Ghadafi akiwa hai Africa haiyonyonyeka na kuwabembeleza kwani-akilipa madeni ya baadhi ya nchi za africa, akigharimia mikutano ya Au, alikiwa na jeuri ya fedha na kuzitumia kwa maendeleo ya wananchi na nchi yake. ukikaa na Mlibya Enzi hizo-huamini huduma wanazopewa bure, makazi ya majumba, ukioa na ukizaa. Bodu guard wake akina mama. pamoja na hata kama alijilimbikizia mali yeye binafsi au wanae-hela ilitumika kwa maendeleo ya nchi yake. Sasa imekula kwao. lakini damu ya Ghadafi daima itatembea kwa wale waliotoa uhai wake. wao wanaopiga mabomu na kuua afghanistan, Libya na kwingine kokote kule-hawapelekwi mahakama ya kimataifa ila Waafrika tu. Wanaowapa vikosi kazi vya wapinzani silaha wanafanya hivyo chini ya mwamburi wa demokrasia. haya sasa demokrasia Misri nayo inaanza maandamano upya raisi wao wa sasa aondoke maana akikaidi wayatakayo. Demokrasia ipo africa ukitendewa wewe uovu sio wewe ukitenda. Ilituumiza sana wakristu na waislamu kuona Muamar ghadagi akiuawa na tumeapiza-damu yake itajibu kwa walioshiriki kumuua.


From: heche suguta <hechesuguta29@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, 30 June 2013, 21:51
Subject: Re: [wanabidii] Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikanunua suti na viatu vilivyonibana!"

Hivo hivo Ghadafi alihenya sana na kujinyima na kutumia Raslimali za Libya kuijenga Libya kwa miaka mingi sana, huyu huyu Obama akaipiga Libya mizinga na mabomu na kuiharibu kabisa kabisa, kisha akamuua yule mzee kwa aibu!!! mimi na Waafrika wengi tunaona pia huyu hata angelifanya nini hatutakaa tumsahau kwa ubaya alioitendea Afrika...


From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, June 30, 2013 1:32 AM
Subject: [wanabidii] Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikanunua suti na viatu vilivyonibana!"

Obama Hafichi Kusimulia Alikotoka, Anasema; " Nilidunduliza nikaweza kununua suti na viatu vilivyonibana, ofisini walishangaa!"

Ndugu zangu,

Obama anasema; " Wakati tukiendelea na masomo yetu ya Sheria mimi na Michelle tulifanya kazi katika kampuni ya Uwakili ya Sidley na Austin jijini Chicago.

Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.

Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.

Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.

Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.

Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama ( Kutoka kijitabu cha Maisha Ya Barack Obama, alikotoka, aliko na anakokwenda, Maggid Mjengwa, 2008.)

Maggid,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment