Monday, 1 April 2013

[wanabidii] UVURUGWAJI WA MAKUSUDI ULOFANYWA NA MASHEHA KWA MCHAKATO WA KUYAPATA MABARAZA YA KATIBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UVURUGWAJI WA MAKUSUDI ULOFANYWA  NA  MASHEHA KWA MCHAKATO WA KUYAPATA MABARAZA YA KATIBA

Leo nchi imeingia katika mchakato muhimu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya kama sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 inavyoelekeza. Umuhimu wa kuwapata wajumbe hawa utakamilisha hatua ya tatu ya mchakato huo kabla ya hatua ya Bunge la katiba. Kwa uzito ulio mkubwa baada ya kukamilika hatua za kabla za utowaji wa maoni kwa njia mbali mbali hatua hii ni muhimu sana kwani inaweka msingi mkubwa wa kuupa uwakilishi wa wanachi kwenda kuipitia rasimu ya katiba iliyotokana na maoni yao.

Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kile kinachofanyika hivi sasa hapa Zanzibar cha kuuvuruga mchakato huu kwa makusudi na masheha ambao tume imewaachia  kufanya walitakalo kinyume na muongozo wa mchakato huu.

Kwamuhibu wa muongozo huo wa tume wajibu na majukumu ya sheha ni kama ifuatavyo:

  1. Kifungu cha 9.2.3.1. Kupokea majina ya wananchi wanaoomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
  2. Kifungu cha 9.2.3.2. Kubandika katika maeneo ya wazi / matangazo majina yote ya watu walioomba kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
  3. Kifungu cha 9.2.3.3. Kuitisha Mkutano wa Shehia utakaochagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano.

Pamoja na Chama cha wananchi CUF kutoa angalizo kwa Tume mapema sana juu ya hatari ya kushirikishwa masheha na kuwalalamikia viongozi hawa wa serikali za mitaa kwa maandishi lakini Tume haikuchukua hatua. Tayari kile ambacho CUF kiliitahadharisha Tume kuhusiana na mamlaka ya viongozi hawa wa serikali za mitaa kimeshachukua nafasi yake kwa viongozi hawa kuuingilia kati na kuuharibu mchakato huu. 

Baadhi ya matukio machache tu katika mengi ambayo yameshuhudiwa hivi asubuhi yakionyesha jinsi masheha hawa wakishirikiana na wajumbe wao na viongozi wa CCM wakifanya vitendo vya kuuvuruga mchakato huu ni hivi vifuatavyo:-

  1. Katika vituo vyote vya Unguja, sheha na wajumbe wake ndio walioendesha na kuratibu zoezi hilo huku wakichukua mamlaka kadhaa kinyume na muongozo wa Tume.
  2. Katika shehia ya Chumbuni, sheha aliandaa vipande maalum na kuwapa watu wake maalum kama ndio utambulisho wa kushiriki katika mchakato huu kinyume na muongozo wa Tume.
  3. Katika Shehia ya Migombani, sheha ameamua kughairisha mchakato kwa siku ya leo baada ya watu kufika kwa wingi katika kituo akidai amapokea amri ya kufanya hivyo kutoka juu.
  4. Katika shehia ya Meya, sheha amegawa karatasi za kupigia kura zisizokuwa za kituo hicho huku akiwatoa wagombea watatu (3) walioomba nafasi hizo na na ambao walikuwemo katika orodha ya wagombea tokea awali. 
  5. Katika shehia nyingi ikiwemo ya Nyerere, sheha amelazimisha kutumiwa kwa ZAN ID kama shahada ya kushiriki mchakato huo ikiwa ni kinyume na muongozo wa Tume.
  6. Katika shehia ya Kiembe samaki, sheha amechukua mamlaka ya kuteua katibu wa mkutano wa shehia kinyume na muongozo wa Tume.
  7. Katika shehia ya Dimani, sheha ametangaza kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba kwa madai ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura.
  8. Katika shehia ya Kihinani, sheha amewataka wagombea kuondoka katika kituo na yeye peke yake akichagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano wa shehia.
  9. Katika shehia ya Kibweni, sheha ndie aliyechagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano wa shehia. Halkadhalika watu wengi kutoka nje ya shehia hiyo wamekuwa wakiorodheshwa na kushiriki upigaji kura.
  10. Katika shehia ya Kwerekwe, sheha amelazimisha uchaguzi ufanyike ndani ya nyumba yake badala ya kituo kilichopangwa kwa ajili hiyo jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa Tume.
  11. Katika shehia ya Kwamtipura, sheha ametoa orodha ya watu wasio wakaazi wa shehia hiyo kushiriki katika uchaguzi huku akiwaacha wakaazi halali wa shehia hiyo.
  12. Katika shehia ya Mlandege, sheha ameteua Mwenyekiti na Katibu wa mkutano wa shehia kinyume na utaratibu, amewafuta wagombea anaodhani ni wa mrebgo kinyume na wake na kubakisha wagombea watatu (3) ambao ni wa mrengo wake. Pia sheha huyu amekua akiwakatalia wakaazi halali wasishiriki kuchaguliwa wala kuchagua kwa kisingizio si wakaazi huku akiruhusu watu wasio wakaazi kushiriki zoezi hili.
  13. Katika shehia za Kibweni na Kama masheha wakiwaruhusu askari wa KMKM kushiriki upigaji kura huku wakiwaacha wakaazi halali wa shehia hizo.

Kutokana na hali hii inavyoendelea ni uhalkika zoezi hili limekwisha kuharibiwa na huku ikizingatiwa Tume ina jukumu la kulinda na kusimamia haki za wananchi wote. Ili sheria ichukue nafasi yake na haki itendeke Tume lazima iliratibu upya suala hili na kuchukua mamlaka yake ili kuweza kuhakikisha zoezi linafanyika kwa taratibu zilizopo, kwa uwazi na kwa haki  bila ya wanachi kubaguliwa,  na  kuwapata  wajumbe   halali  kama  muongozo  wa  tume  ulivyoelekeza kushindwa  kuyasimamia haya hivi sasa ni  kuhakikisha  uchafuzi ambao  utaleta  dosari   kubwa katika  hatua   ya  kuwapata   wajumbe   wa  baraza   la  Wilaya   la  katiba .

HAKI SAWA KWA WOTE

………………………………

SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU, HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA

Headquaters P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania Tel 024 22 37446 Fax: 024 22 37445
Main Office: P.O Box 10979, Dare s salaam, Tanzania: Tel 022 861009 Fax: 022 861010


Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2PC9dQZNr

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment