Monday, 1 April 2013

[wanabidii] Religion and paying tithe 10%


Hon MP. Iringa Town,
 
Thanks for your article concerning the difference between religious and spiritual people, as well as paying God 10%.
In fact God is not a religion. God is a Spirit. Religious people are not righteous. Spiritual people are righteous.
It was the religious people that killed the Living Savior. Jesus told them 'you belong to your father, the devil'.
Religious people need deliverance from the the religious demons and the fear of men.
We are excited about having a section of our website dedicated to Swahili.
We sure appreciate this opportunity and do pray that Swahili speakers will benefit from this outreach.
First four articles are now up. One concerning a religion.
We put a link on the front page of our site. You cant miss it.
Will you please check it and give me some feedback?
Praise God that we can work together on this.
Concerning the tithe or paying God 10%  Jesus came to pay  on the cross that debt which no man could fully pay.
No scripture in the New Testament, where we are supposed to pay 10% to God. Go to the book of Acts. Here is 100%
Jesus offered Himself 100%. Let me ground in to detail in Swahili.

FUNGU LA KUMI YESU ALITULIPIA KAMILI
Yesu alikuja kulilipa lile deni ambalo hakuna mwanadamu awezaye kulilipa kamili.
 
"Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa Imani yenu. Kwa maana, amin nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu". Mat.17:20
 
Swali: Nimekuwa nikifikiria kuwa Yesu alikuwa anasema kama tungeweza kuwa na hata imani ndogo, ingekua mpaka ikawa kubwa ya kutosha kuhamisha milima. Nadhani mbegu ya haradali ilikuwa ndiyo mbegu ndogo kuliko zote katika Palestina lakini inapopandwa inakuwa mti mkubwa kuliko yote.
 
Jibu: Ndiyo; yote hayo ni kweli. Hata hivyo kuna kitu cha msingi zaidi katika kanuni za kudumu za Baba.
 
Swali: Je, kupanda mbegu ndicho Yesu anachosema Kutoa na kuvuna mavuno kutoka kwenye mbegu ndicho anachokiita kupokea?
 
Jibu: Ndivyo kabisa.
 
Swali: Halafu mbegu ya utoaji ndiyo mbegu ya imani na mbegu inatakiwa ipandwe kabla hatujauambia mlima wetu wa mahitaji kuondoka. Mbegu ya imani huja kwanza, ndipo  hapo utakapoongea na mlima wako wa hitaji. Sasa nimetambua kwamba KUTOA ni mbegu ya imani yenyewe na ningeweza kuelekeza mbegu kuhamisha mlima maalumu wa hitaji.
 
Jibu: Soma kwa makini hotuba ya mlimani, na hasa undani wake na utaona kwamba KUTOA ndiyo kiini cha yote ambayo Yesu aliwafundisha watu. "Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa;  kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa –sukwa hata kumwajika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopewa". Lk.6:38
 
Swali: Kutoa ni KUPANDA KWA AJILI YA MUUJIZA WAKO ambapo Mungu chimbuko lako atakuzidishia katika nyongeza ambayo itakuwa kubwa na yenye nguvu zaidi kuliko milima yetu ya mahitaji na matatizo?
 
Jibu: Kutoa ni kitu ambacho unakifanya na kukifanya kwanza. Hotuba ya mlimani imelenga katika kitu unachokifanya kwanza. Samehe kwanza, tafuta kwanza ufalme wa Mungu, uwe na njaa na kiu ya haki kwanza, toa kwanza..."Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo". Lk.6:31
 
Swali: Nimegundua katika Agano la Kale kwa kawaida kutoa kimsingi kulitokana na kupokea kwanza ndipo utoe. Kwa ule uhalisia sheria ya zaka ilitokana na kupokea kitu na kutoa sehemu ya kumi kumrudishia Mungu. ilikuwa ni deni unalodaiwa na Mungu.Unalipa zaka zako. Hii ndiyo maana ya Malaki 3.
 
"Je,mwanadamu atamwibia Mungu? lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mnasema, tumekuibia kwa namna gain?. Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la". Mal. 3:8-10
 
Jibu: Hii ni sawa kabisa......Yesu alikuja kulilipa lile deni ambalo hakuna mwanadamu awezaye kulilipa kamili. Pale msalabani alilipa lote kwa kila mtu. Yeye ndiye mbegu ya Daudi Baba aliyoahidi kuwa Masihi, Kristo. Tangu ayatoe maisha yake pale msalabani na kumlipia kila mtu deni lake, alirejesha utoaji katika kusudi lake la mwamzo.
 
Swali: Je kusudi lake lilikuwa lipi hilo?
 
Jibu: Hapo mwanzo  ilikuwa kwanza kipindi cha mbegu ikifuatiwa na mavuno "Muda nchi idumupo ,majira ya kupanda na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma". Mwa.8:22. Kwa asili hii haijabadilika. Katika kipindi cha manabii, kanuni hii ilitumika mara nyingi kwa mfano kile Eliya alichokifanya na yule mwanamke  mwenye njaa na mjane wa Sarepta ......"Eliya akamwambia usiogope enenda ukafanye kama ulivyosema lakini unifanyie KWANZA mkate mdogo uniletee, kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao, kwa kuwa Bwana Mungu wa Israeli asema hivi, lile pipa la unga halitapunguka wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoileta mvua juu ya nchi". 1Fal.17:10-14.
 
Wakati Israeli ilipokuwa Taifa, wana wa Israel ilibidi kufundishwa mali ya Mungu kwao. Kwa mfano mtoto wa kwanza wa kiume alikuwa mali ya Mungu, siku ya saba ilikuwa ya Mungu, mwaka wa saba ulikuwa hakuna kupanda wala kuvuna. Mwaka wa hamsini ulikuwa mwaka wa jubilee, watumwa wote waliwekwa huru, ardhi yote iliyonunuliwa inarejeshwa kwa wenyewe, madeni yote yanafutwa..... "Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi,  ni sabato kwa Bwana, usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu....na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote waiketio;  itakuwa ni jubilee kwenu ninyi; kila mtu atairudi milki yake mwenyewe nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. Law.25:3, 10.
 
 
Yote haya pamoja na fungu la kumi ilikuwa kumlipa Mungu lakini hakuna aliyeweza kumlipa Mungu kamili. Israel walimwibia Mungu fungu la kumi, uzao wa kwanza na vitu vingine vilivyowakilisha mali ya Mungu kwao. Ikawa deni zaidi ya uwezo wao wa kustahimili hivyo Mungu akaamua kumtuma Mwanae wa pekee kuja kulipa gharama yote ya kumkomboa mwanadamu na kumrejesha. Tangu kifo na ufufuko wa Yesu, utoaji sio kitu unalipa, kwa maana Yesu alisha lipa deni. Utoaji katika Agano jipya ni mbegu unapanda.
 
Swali: Kama Wakristo, wafuasi wa Bwana Yesu kutoa, kwangu  sio tena deni ninalodaiwa lakini ni mbegu ninapanda?
 
Jibu: Ndiyo,Yesu aliikamilisha ile sheria ya zamani ya zaka kwa kutoa maisha yake msalabani. Msalaba ndio mbegu ya maisha yake. Mbegu aliyoitoa ilikuwa mbegu ya imani ambayo Baba aliizidisha kwa kumfufua Yeye katika wafu na kumwongeza zaidi ya alivyokuwa mwanadamu. Je, unaliona hili?
 
Swali: Ndiyo, ndiyo, inaondoa ile hofu ya kutakiwa kulipa deni  katika kile kitendo cha ulazima kwa sababu mara nyingi nimelipa kwa sababu nililazimishwa katika ile hali ya kutakiwa kufanya hivyo kwa kuwa ni kitu ninachodaiwa. Kwa hiyo hapakuwa na furaha katika utoaji wangu. Ikikuwa zaidi kama kitu cha kulazimishwa. Naogopa nimewahi kutoa kitu ambacho hakikuwa kabisa kutoka moyoni mwangu. Utoaji wangu mzuri ulikuwa ule wa kutoa kwa moyo wa furaha.
 
Jibu: "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu hupenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu" 2Kor.9:7.    Kumbuka Agano Jipya linasema Mungu hupenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Kumbuka vilevile Yesu alisema ni heri kutoa kuliko kupokea. "Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea".  Mdo.20:35
 
"Tena ndugu zetu, twawaarifu habari za neema ya Mungu,waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe, walitoa vitu vyao" 2Kor.8:1-3.
 
Swali: Ninaona kwamba wakati ninapotoa, ninaonyesha sura halisi niliyonayo kwamba mbegu itazidishwa.
 
Jibu: Ndiyo. Hiki ni sahihi. Imani ndiyo ikufanyayo wewe upande mbegu. Vinginevyo usingelipanda mbegu kabisa. Inahitaji imani kupanda mbegu, na inahitaji imani kuamini kwamba mbegu iliyopandwa itaota na kuleta mavuno.
 
 
Swali: Ndipo sio kile kitu ninachokipokea kilichozidishwa, bali ni kile ninachopanda au kutoa?
Jibu: Ndiyo, unapokuwa na mlima wa hitaji, panda kwa ajili ya muujiza wako. Kama utaweza kuwa na ujasiri wa kupanda mbegu, ambapo ni kutoa kitu fulani cha kwako, ndipo hiyo mbegu itamea kwa njia ya udongo wa maisha yako (udongo ni uhusiano wako binafsi na Yesu Kristo) na utaleta matunda yake au mazao. Ile mbegu itakupa wewe nguvu ya kuongea na mlima wowote wa mahitaji yako na kuuamuru kuondolewa kikamilifu, na hakuna kitu  kisichowezekana kwenu.
Swali: Unasema kwamba ile mbegu ya imani kweli itaniondolea milima yangu?
 
Jibu: Kabisa kabisa, wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Yesu alilisema hili    wazi katika Mt.17:20.
 
Swali: Unasema wala halitakuwako neno lisilowezekana kwangu?
 
Jibu: Ndiyo, wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu kama mtaipanda mbegu kwanza. Huu ni mpango wa Mungu kwenu kama watoto wake na wanafunzi wake kwamba wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
 
Swali: Yesu alinilipia deni langu lote kwa njia ya mbegu yake pale msalabani.Wala siko tena chini ya kifungo cha kutoa kutokana na kulazimishwa au kulipa deni ninalodaiwa na Mungu, kitu ambacho ni njia ya zamani ya utoaji zaka. Mara zote nimekuwa nikifundishwa kwamba wakati ninapotoa, sitakiwi kutarajia kurudishiwa kitu. Hapa,Yesu anasema kupanda mbegu na kutarajia mavuno kwamba kama nikitoa nitapokea.
 
Jibu: Hutakiwi kutarajia kutoka kwao au kutoka kwa wale ambao unawapa. Utoaji wako unatakiwa uwe  ni kwa Mungu na matarajio yako yanatakiwa yawe  kwa Mungu.
 
Swali: Halafu sihusiki na matokeo ya wale ninaowasaidia kwa kupanda mbegu yangu. Natakiwa kutoa hata kama zitajarudi kwangu au hapana?.
 
Jibu: Hilo ni sahihi. Sababu ni kwamba wao sio chanzo lako. Wale uwapao, wanaweza kukupa na wewe au wasikupe. Ndiyo sababu Yesu anakutaka wewe utoe ili kwamba akaweze kufanya kazi yake. Anachotaka ni mbegu yako utoaji wako kwanza ili kwamba ukaweze kuongea na mlima wako wa hitaji. Ina maana baada ya kupanda kwako, anza kutarajia muujiza na uendelee kutarajia mpaka utakapokuja.
 
Swali: Lakini kwenye kutarajia muujiza kutoka kwa mbegu ya imani niipandayo, natakiwa kutarajia tu kutoka kwa Mungu chanzo changu?
 
Jibu: Ndiyo. Mungu ndiye pekee asiyebadilika na chimbuko lote  la kutegemea "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".Flp.4:19.
 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. 2Kor.8:9. Yesu alikuwa maskini lakini si kwa ajili yake bali kwa ajili yenu. Katika siku hizo, hakuwa na hata mahali pa kulaza kichwa chake. Lakini baada ya kifo chake na kufufuliwa, Yesu sio maskini tena. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Mt.28:18. Utajiri wote mbinguni na duniani ni mali ya Yesu Kristo.Yeye hana mipaka katika utajiri wake na uwezo wake wa kukupatia kila unachokihitaji. Ndiyo maana Biblia inasema "Ni Mungu ambaye atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu,  ndani ya Kristo Yesu".
 
Swali: Ni nini cha kufanya mimi baada ya kupanda mbegu yangu?
 
Jibu: Tarajia muujiza wako. Unapotoa, kupanda mbegu yako ya imani kwa Mungu utarajie kuivuna, utachuma mavuno. Kwa vile mavuno hayawezi kuelezwa kibinadamu ni muujiza, inabidi uutafute na uutarajie. Kama huutarajii, wakati muujiza unapokuja utakupita.Unaweza kuanza kulaumu kwanini Mungu hanibariki mimi lakini muujiza wako unakuja na wewe hautambui.
 
Swali: Ni kwanini kwamba wakati mwingine unakuja haraka, lakini wakati mwingine inaelekea kuchukua muda mrefu sana?
 
Jibu: Kwa sababu nyakati na majira ziko kwa Baba peke yake. Anafahamu wakati muafaka na njia nzuri zaidi ya kukutumia miujiza yako. Tena ndiyo maana anasema kama ukiweza kuwa na imani kama mbegu.....Biblia inasema "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani,....lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza". Ebr.10:38,11:6
 
Swali: Nakumbuka Paulo Mtakatifu aliandika katika Wagalatia 6:9 kwamba kuna "wakati wake" kwa mbegu iliyopandwa.Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia moyo.
 
Jibu: Mtakatifu Paulo alieleza kwamba Agano Jipya limejengwa juu ya mbegu ya imani." Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna".Gal.6:7. Mbegu nzuri au mbegu mbaya zote zitaleta mavuno yake. Mbegu nzuri zitaleta mambo mazuri katika maisha yako na mbegu mbaya zitaleta mambo mabaya katika maisha yako. Halafu Paulo aliongeza, na tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia moyo. Kama ukipanda mbegu nzuri, Mungu atapanga muda wake na njia yake kwa ajili yako wewe kuvuna. Huo ndio utakuwa ni wakati wako.Hivyo usikate tamaa kutegemea muujiza. Msubiri Mungu.Wakati wako muafaka utafika.Kumbuka kwamba anawajali na atawapa kila mnachokihitaji.
 
                        
"Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;  kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi" Rum.12:10-13  Kumfuata Kristo kama askari wake inagharimu maamuzi yasiyo ya kichoyo.Inahitaji uangalifu mkubwa wa maisha yetu ya kibinafsi. "Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumisjhi wenu kwa ajili ya Yesu", 2Kor.4:5. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuutafuta mwili,bali tumikianeni kwa upendo.Gal.5:13
 
"....bali tulikuwa wapole kati kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.." 1The.2:7-8. Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake vile vile kama mnavyofanya. IThe.5:11


   
IN TRUTH AND LOVE are all these various instructional resources brought forth. The love of God for the lost, the love of God for those who are His—in that Spirit of love—for education and edification we offer to humanity as a FREE GIFT these Prophetic Words, articles, videos, testimonies and more. May you be set free, blessed, increased in the knowledge of the truth. May the love of God be with you in truth. (John 3:16-21.)

DOWNLOAD.   
www.aggressivechristianity.net 

READ BOTH WORDS HERE.

LISTEN TO BOTH WORDS HERE.
(Note: Slower connections will take longer to load and play files. Files can take up to 60 Seconds to begin streaming.)

Let us know your thoughts. Order Our FREE Publications, CDs, DVDs, and tapes.
Contact us!

  CONTACT INFORMATION
Tired of your dead church routine? Phony religion got you down? Sick of religious racketeers, perfumed preachers, beligerant beggars? Why not do something real for the Kingdom of God during your lifetime?! We would love to hear from you! Get AGGRESSIVE and REVOLUTIONARY for Jesus and your life will never be the same.
To request literature or more information about our community please E-mail us:
livingword@aggressivechristianity.net
To contact the Generals personally please use this E-mail:
Generals-az@aggressivechristianity.net





Looking forward to hearing from you,
Major Frank Materu,
ACMTC - TANZANIA





Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 








0 comments:

Post a Comment