Monday, 1 April 2013

[wanabidii] Re: TANZANIANS AND FEAR TO SYSTEMATIC ANSWERS

Mnamo tarehe 7 Machi 2013, ikiwa ni takribani wiki mbili kabla ya kifo cha Mawalla, Manyerere aliandika maneno haya mtandaoni: "Tatu, Grumeti haipo Ngorongoro, bali ipo ndani ya Serengeti, wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Nabii wao wa kisheria ni Mawalla anayepatikana mjini Arusha. Hii ni mali ya kina Tudor Jones, Sir George Kahama na makaburu kadhaa. Kwa msaada zaidi kamwone Madanga Shaaban Madanga au yule veteran aliyeng'atuka Uhuru. Grumeti ni moja ya sehemu tamu kabisa za kwenda kupumzika. Kuna vyumba vya bei nafuu vya dola 1,800 za Marekani (siyo za Zimbabwe) kwa usiku mmoja! Wadau wengine watembelee huko wale maisha kama ulivyokula dada Leila"


From: Deo Kibambizi <kibambizi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, April 1, 2013 2:49 AM
Subject: [wanabidii] TANZANIANS AND FEAR TO SYSTEMATIC ANSWERS

Mara nyingi kwenye blog zetu,nimekuwa nikiona wana jamvi wakichangia sana sana kwa mambo ambayo majibu yake hayako wazi.Mfano mambo ya dini ambayo kila mtu anakuwa na jibu lake yamekuwa yakiongoza kwenye post.Na pia mambo ya majungu nikimaanisaha mambo ambayo kiukweli hamna wa kuthibitisha yamekuwa yakipata wachangiaji,na cha kusikitisha mchangiaji anajiita MSOMI.Ila kuna mambo mengine ambayo,japo yana kasoro ila yakipata mtu wa kuyaelezea vema(SYSTEMATIC) basi hakuna wa kuchangia kwa sababu watu wengi hasa ndugu waandishi hawana uelewa wa mambo fulani fulani.Ila we....LETA JUNGU UONE jinsi kila mmoja atakuwa mstari wa mbele kuachangia.Mfano;waziri wa ujenzi Dr.Magufiri anajiamini,na aliisha jua njia sahihi ya kutoa taarifa na pia kuwajibu na kuwaambia watu hasa waandishi wa habari...ni kutumia LOGIC ZA taaluma yake na hapo watu wana kaa kimya na kuendelea kumsifia kwa yale ayasemayo.Japo anafanya kazi vema,je hakuna hata wataalaamu wa kutegua LOGIC ZAKE kweli au hadi afe au atoke wizara moja aingie wizara nyingine?Ndugu zangu.Dr.Magufuri huwa ninampenda sana na kumuamini kwa mambo mengi anayofanya,na hii ni kwa sababu ninaona matokeo ya mambo ya misimamo yake na faida kwa Taifa.Ila kuna baadhi ya watu huwa tunaogopa kuokosoa mambo kwa kushindwa LOGIC SETTNG hasa waandishi na pia kuogopa kuwa responsible kwa wahusika pale tukipata nafasi ya kugundua maovu yao.
Suala la Marehemu Mawala limenifumbua macho na kuona udhaifu wa Manyerere.Manyerere aliogopa LOGIC za Mawala na akakaa kimya hadi siku ya kifo chake.Aliogopa LOGIC ZA LAW hadi TAIFA likaingia kwenye janga hili ambalo kila mwenye dhamana ya nchi,na hasa wale wanaolewa mambo ya kuendeleza uchumi wa nchi yetu.Manyerere alishindwa nini kutueleza haya kabla ya Mawalla kuaga dunia.Naweza kusema,Mawala wengine wapo wengi ambao Manyerere anawafahamu,ila anasubiria wafe ndiyo aonekane yeye ndiye nabiii wa yake yaliyopita na wala si wa yale yajao.

NAULIZA,Hasa kama Manyerere angejibu haya kama yumo humu,au rafiki amtumia ili tupate pa KUMSHKURU KWA HILI.Vinginevyo tufahamu kuwa hakuna anayeshukuriwa kwa UNAFIKI.
1.Je,kama Mawalla angeendelea kuishi kwa staili hii je,Manyerere angesema haya?
2.Je,Manyerere alifahamu hili mapema?Kwanini hakutariifu mamlaka zinazohusika?
3.Je,Manyerere kwa nini atokezee hadi baada ya kifo hiki?

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment