Sidhani kama wanafanya hivyo kwa sasa kujichora tumbo na uso! Labda tohara na ukeketaji.
Hiyo fashion ya kujichora miraba usoni na tumboni vijana imekwisha. Siku hizi ni kutunisha misuli au kuwa rasta. Hiyo imekwisha siku nyingi hata huko west African countries. Hata ya kutoboa masikio inakwisha/kupungua na ya kuchanja chale za pande mbili za uso kwa warufiji au chapa ya thumuni ya Wagogo usoni. Hii ya Kirufiji na Kigogo dawa za Measles (Rufiji) na za Trachoma (Ugogoni) zipo zinatolewa hospitali na Trachoma ina trained community drug distributers watoao dawa nyumba hadi nyumba kupunguza upofu utokanao na mainzi weusi wa klwenye kinyesi cha mifugo.
Hata huko unakosoma utaona wakitoa video darasani wanaonyesha ile ya 1860-1940s sio ile ya 2000 todate na siku hizi digitali. Hawataki kuonyesha Airport, Barabara za lami, maendeleo Beach Hotels ambapo baadae utaona wanafunzi au mkitembelea mahala watoto wanakuuliza ulifikaje kule, ulivaa wapi nguo ulikoipata. Wakiona watu wanakimbiza mifugo mgolole unapepea matako nje; au watoto uchi kijijini kinyumba cha nyasi mainzi uso mzima yanaingia mdomoni na kutoka na yamejaa machoni basi wanajua kila mtu na nchi nzima ni hivyo. Hata hao peace corps volunteers huwa hawaonyeshi picha zao wakiwa beach na mahotelini labda za mbuga za wanyama pori tu na huwadanganya sisi kuwa tunapanda miti kwa elevators/lift na simba ni pet majumbani. Volunteers walioishi kwetu huwa wanaonyesha wakiwa remote areas katk mazingira magumu sana, machafu waonekane waokovu. Niliona mimi. sio wote waelezao na kuonyeshao ukweli kuwa huku nako kuna cities na kuna vijiji poa/vizuri vyenye maendeleo pia. Na kuwa huwa nao wanaiba mpaka vikaka vyetu na wengine vibabu kuchukua visichana vidogo. Kazi ni kuzisema tu bila za huku kuwa primitive na kandamizaji. Mengi mabaya kuliko mema wao ndio wakombozi sio waharibifu. Soma somo la cultural anthropology huko uone utaonyeshwa nini kama hujapanda mori na wazimu humo vitu wanavyowekea mkazo.
--- On Sat, 27/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> Subject: Re: [wanabidii] Tudumishe mila To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Saturday, 27 April, 2013, 10:33
Kiwasila nilipoona hii Vedeo niliogopa sana maana inatisha, ila sasa kijana asipofanyiwa hivyo anaonekana sio mwanaume. Vitu kama hivi vinapaswa kukomeshwa. Alexander
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> To: wanabidii@googlegroups.com Sent: Saturday, April 27, 2013 3:20 AM Subject: Re: [wanabidii] Tudumishe mila Alexander una hatari. Sidhani kama ulimaanisha kweli kuwa tudumishe mila hizi. Hii video labda wamechukua kwenye film za zamani wakaiweka ktk video. sidhani kama wengi wanafanya haya kwa sasa kutokana na HIV infection kwani watoto huzaliwa nazo pia ni kutaka kujiua. Studies za TZ zimeonyesha akina mama na baba wazee ngariba na wakunga wa jadi wanaambukizwa ukimwi. Wengine-hasa akina mama akiulizwa-kama ana mume na mume ana wake wangapi anasema-mwanangu, nina mwaka wa 30 sasa sina baba na mambo hayo sina niliachwa au alikufa. Kuja kumuuliza shughuli zake-Ngariba, Mkunga!!! Ohooo-kukeketa kumempa HIV infection. Sasa hii tatooing inakuwaje? Mtaambukizana.
soma kitabu Cha 'Chale za Kimakonde' uone kwa nini walichanja-kutaka wachichukuliwe utumwa, wakaharibu ngozi asipendwe kuuzwa na kununuliwa. Kuchanja ikawa mila. wao wakageuzwa manokora. akitokea mwarabu-anakenua meno kumtishia na yapo kama msumeno na uso chale tupu.
Kutoboa masikio-Ecological. Bila ya matundu sikiono upepo huvuma kuingia ndani ya tundu la sikio-huwezi kusikia mnyama akilia na ng'ombe akitoa sauti ya hatari au ya kuzaa. Ukitoboa upepo unapita upande wa pili-inakuwa culture na kuweka mapambo for identity. Unachukuliwa utumwa toka Kivu congo kupelekwa Bagamoyo-ZNZ, tukizolewa tutajitambuaje? Tutapotezana! wanaamua kujiweka alama fulani ukimuona unajua huyu wa kwetu. Kuna vitabu vya anthropology vyenye picha za waafrika za 1800 jamani zina watu apo bila ya nguo lakini kitu muhimu kwao ni mapanki kichwani. yaani mapanki ya nguvu huwezi kuamini na vibwenzi akina baba na vijana hatari. Mapanki kama ya watu wa Ethiopia na makabila mengine Africa.
Fahamu kuwa hata FGM inafanywa kwa marembo tofauti Africa katika mila wanazokeketa. hata male circumcision kwa makabila ina marembo yake au muundo wake wa kufanisi. Hii nayo ipo vitabuni medical doctors wameiandikia na kuionyesha. Waisraeli ndio wanafanya kwa ustadi kabisa male circumcision yaani ni ritual ya hatari. pamoja na kuwa FGM inasemekana ni mila lakini uchunguzi unaonyesha vinginevyo hata kufikia kuukata na kuushona kuuziba ukifanyika kutatua matatizo maalum physical na medical sio cultural.
Kutoa meno ya chini-matatizo ya tetanus-ipo documented. Mtu akiupata ugonjwa huu na kuwa anabana meno kumpa uji na mitishamba inakuja kuwezekana kwa bamboo kama meno ya chini yametolewa.Kuyaondoa meno inakuwa preventive measure ili ukipata tetanus usaidike baadae inakuja kuwa-mila na matamshi ya maneno yanakuwa mazuri ukiondoa meno kuliko ukiwanayo hivyo mila inapata uwezo zaidi.
Kuna watu wa pwani na wengineo wakitoboa masikio na pua chini kuvaa majaribosi, kishaufu na kutoboa pua juu kuvaa kipini; baadhi bara kuvaa kigurudumu miguuni wengine kuvaa makorija ya vito vya dhamani na shanga. Kila kabila na mambo yake. lakini hii ya west african kujichora kali sana na utumwa uliwabeba sana kuwapeleka kulima mashamba bara la america huenda ilikuwa ni sehemu ya alama ya kujitambua baadhi yao kama si mila.
Makabila mengine-ni mwanaume anayejipamba sio mwanamke. anasuka nywele, ashakum anavaa shanga kila eneo (kila eneo na kwingineko kusikoonekana). wanawake hawajipambi hivyo wao ni wa kuangalia mwanaume mzuri aliyejipamba sana yupi nimpende. na kuna siku ya ngoma wanaume kucheza wanawake kuhama kundi hadi kundi la wachezao kujichagulia. ukiangalia kwa wanyama-ni ndege dume, wanyama dume wanaopendeza kuwa na manyoya, mkia wa kuchanua, rangi kali etc ili kuvutia mijike. tausi dume, Jogoo, simba dume ni mifano michache tu. Hivyo, usishangae kuona kwa wafugaji wanaume hujipamba sana na kuwa hodari wa kusuka mitindo ya nywele.
Lakini-pamoja na wengine kwa sasa kuchona masikio yaliyotobolewa zamani (baadhi); kutokuvaa ndonya au majaribosi-wapo vijana wanarudisha ya kale kwa kujichora mwilini kila sehemu au sehemu chache. wapo wanaotoboa masikio na wengine kuchonga meno na kuvaa kama Yonomamo wa Brazil porini au Wahindi wa zamani, kuwa rasta, kuweka manyewe yananing'inia. Huko ulaya ulipo kuna vituko vya watu wanaojiharibu miili kwa kila aina ya michoro na utomoaji mpaka wa vishaufu vya zamani vya pwani na umakondeni. Wengine wanatisha.
Kama unataka tudumishe mila ya kuchanja namna hii-imekula kwako utasambaza HIV na infections nyingine hata tetanus maana. Hizo vita za congo na sudan watu wanavyoambukizwa kwa kubakwa, leo tudumishe mila za kuweka tatoos si nchi zinazopigana zitabakia na watu hai 10% ya population ya sasa?
--- On Fri, 26/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> Subject: [wanabidii] Tudumishe mila To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Friday, 26 April, 2013, 21:56
Jamani angalieni hii vedeo ya kudumusha mila huko Benini Alexander
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
|
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
|
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment