Kwa janga hili jamani kama kweli kumbe mapendekezo ya Tume ya Lowasa hayakutekelezwa nadhani labda Mh. Mtoto wa Mkulima atapata upenyo awe shujaa kwa kujiuzuru... Nakumbuka Waziri Mkuu wa Japan alijiuzuru kutokana na mtetemeko wa ardhi kuadhiri kinu cha mtambo wa nuklia. Kujiuzuru ni ushujaa jamani husani mtu akijituma kujiuzuru!! Ila kule kufeli kwa mitiani ya kidato cha Nne nako kulikuwa sawa na kudondokewa jengo pia jamani!!! Maana wanasiasa wetu walio anzisha sekondari za kata 2006 walikuwa na uthubutu kama wa jamaa huyu wa mTaa wa Ghandhi kujenga orofa 16 kwa ramani ya nyumba ya orofa 9 labda tena kwa nondo za orofa moja!!!! Au siyo?!!! Ladba serikali nzima ya CCM iliyoanzisha sekondari za kata nayo ifanya kitendo cha ushujaa ijiuzuru kwa kuanguka jengo ilo la elimu duni? Nadhani hakuna atayejiudhuru maana vyeo si dhamana tena kama enzi za Mzee Ruksa bali ni nafasi ya kupata marupurupu....Mungu ataendelea kutusaidia!!!
Mwl. Lwaitama
Date: Tue, 2 Apr 2013 03:34:03 +0100
From: khildegarda@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: wanabidii@googlegroups.com
Inakera, kwa sababu sheria zipo na vinaonekana. Tukazane basi hao wenye fedha wasaidie GVT kununua vifaa vya uokoaji. Wanapochangia chama cha siasa millioni 500 wanaweza pia kuchangia ununuaji wa helikopta ya zima moto angalau moja kila ya baada ya miaka 5 pamoja na vyombo vya uokoaji baharini na nchi kavu (migodi, kuanguka majengo). Na bado yataanguka mengi, kuwaka moto na kutumbukia ardhini. Tusubiri tu tutaona. Si kila mwenye ghoroda anapasua ardhi kwa kuchimba kisima kiregu na kupampu maji, kutengeneza nyufa ardhini na vacuum, kupasua mawe chini ambayo hulegea? ujenzi wetu si uchakachuaji hata visima? Moto utawaka kwani maghorofa na nyumba za makazi, vigenge, petrol station, garages na welding places vimebadana bila mpangilio? Ramani ya 1979 ya mipango miji haizingatiwi kabla hiyo ya 2013 haijatoka. Tulikwenda vema huko nyuma za ni Economic liberalism ambapo unafanya utakavyo. Wenzetu hawakwenda pekupeku hivi na uchumi huru walizingatia sheria za ujenzi, utupatji taka, usalama barabarani na uwekezaji. Hizi sera za uchakachuaji na rushwa; kuogopana kutokana na kutishiana na kuuana au kung'oana kucha ndio zinafanya vitu viende hovyo. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alisema-Uhuru Bila ya Kuzingatia Sheria ni sawa na Wenzawazimu-Kichaa. Watanzania tukubali kubalidika na kuongozwa na sheria kwa sababu ni kwa manufaa yetu. Ona sasa hasara iliyopatikana, mpita njia kaangukiwa na jumba sio tu mfanyakazi. Na majumba mengi yanaendelezwa juu yakiwa huku yanatumika eneo la zamani chini kuna wafanyakazi. Ikiwa yataanguka-ni hasara kiasi gani? Urefu kwenda juu unaruhusiwa bila ya nchi kuwa na vifaa vya uokoaji. Moto ukiwaka itakuwaje? Ghorofa zipande juu kulingana na uwepo wa zana za uokoaji ama sivyo ziishie kama mpango wa zamani ulivyokuwa ukionyesha-mfano magomeni mwisho ghorofa mbili, kariakoo nne posta huko ndio zaidi kidogo. Na zamani ikitegemewa ghorofa ni za Institutions sio nyumba binafsi. Tuzingatie sheria ili kuokoa matumizi mabaya ya fedha za umma na zetu. RC wa DSM ni mtu mwelewa sana na mwenye msimamo. Akazanie Dar isiwe kichaka cha uchafu na ujenzi holela na kiongozi wa maafa pamoja na mafuriko ya kujitakia kutokana na tabia za uchafu na ujenzi mabondeni. --- On Mon, 1/4/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
|
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment