Wewe kijana, utamuitaje mtu mhaini halafu kutwa unahamia kwake ndiko unakoweka biashara zako za mamilioni, unanunua ardhi unajenga na kulima, ndio unakokutegemea kibiashara. Mkikwaruzana nyumbani kwako kisiasa unapanda boat kulala huko na kurudi kwako kwa asili asubuhi mpkaka kunavyopoa ndio unakaa kikawaida. Baniani Mbaya lakini kiatu chake Dawa? hii sitaki nnataka itakwisha lini kati ya TZ bara na Visiwani? Uhaini upande mmoja tu-yaani mkosa daima ni mmoja sio pande zote. Halafu kuendelea kuhamia bara. Lakini pia- manaikanusha historia. Watu Kisiwani walizuka tu? walitokea wapi? hata kisiwa au visiwa vyenyewe vilitokana na volcanic actions na ipo siku vitarudi chini vilikotokea au kuzamishwa na Tsunami na rising sea level kutokana na CO2 itokanayo na uchafuzi wa mazingira. kwa hiyo ikitokea hivyo watajenga floating houses wakabie huko? tafuteni tu balaa!! Mnaona mifano ya mapigano yasiyoisha, mauaji, ubakaji, uporaji mali huko DRC, S. Sudan, Nigeria na matatito ya Udini, Mali, Central Rep of Africa haya anzeni. Wanaowadanganya wapo kuondoa stress zao huko walikotokea na kuja kupora mali zenu. Wajinga ndio waliwao!! Jiulize kwani Libya na Egypt wamepata nini. yaani hali ni bora kuliko alipokuwa Gadafi na Mubaraak? Oneni mbabe wa Syria anavyoimaliza nchi yake yeye na wapinzani wake wananchi wanahaha! Kiangalie kakijana cha nywele za Punk ka North Korea kalivyo kababe kanavyotaka kutetea nchi yake kipambane na S. Korea na wamarekani na Sera zao za ubabe pia. Bajeti yetu kubwa misaada toka nje-tumebweteka hapa na raslimali zipo. maneno, poroje uzalishaji mali finyu, visingizio kibao. Sasa mnataka kujimaliza kwa vita vya ukabila, ubaguzi wa kiasilia au udini? Kama tutaacha kubweteka, tutafanyakazi kwa bidii, hatotokuwa na muda wa malumbano na maandalizi ya kibaguzi na kupanga vita. tupo kuchakachua tu hata majengo kuchakachua na unajua litaanguka ukifanya hivyo. Unaona mwisho ilikuwa ghorofa 10. wewe mbia NHC na mwenzako unaona zinaongezeka 11 hadi 16 huulizi na kusimamisha ujenzi why? Aibu shirika la Taifa. Ndio hapo unasema 10 za ubia hiyo ya juu ya 11 ni yangu ya 12 ya fulani, 13-16 za waheshimiwa A-Z. Ndio hivyo yasemavyo maneno ya mtaani? kama ni uongo-why design ikiukwe? Kama mtu ni Mhaini humtaki-huuingii kwake kuvua samaki, kukata mikoko na kuisafirisha kupeleka uarabuni, kuoa na kuishi. Unakaa kwako ili usipate najis ya uhaini.Kwako unakufanya kuwe na maendeleo ya mfano kusiwe na chuki za ubaguzi ili mhaini akuonee wivu. Hamtomwagiana tindikali, kubaguana majumba ya kusali na kukwepa kuzikana sababu ya chuki. Watu huwa wakweli, wapenda haki, watoa zaka na kuchangia maendeleo. Bei hazipandi wakati wa sikukuu za dini wala mfungo wa sala. Lakini bongoland-ifike mfungo wa Ramadhani, sikukuu za Idd, Christmas, Pasaka-wanaosali sana, kufunga etc ndio wauzaji biashara za bei ya kuruka! Hunishangaza mtu unaona hiki ni kipindi ya utukufu wa Mungu mbona bei ndio zimepata sana? tunasali na nkufunga nini sasa na kutubu kitu gani wakati ndio tunavuna faida kubwa kwa kudhulumu? Sisi wabongo-waafrika tu nduma kuwili sana!! Hatutaendelea kwani tumekalia midomo tu utendaji mchache, visingizio kibao. Tutaacha haya yote kama kila mmoja wtu toka kaya hadi ngazi za juu atajiuliza-umeifanyia nini familia na nchi yako na kutimiza wajibu wako kwa kutumia nafasi yako na raslimali zilizopo hapo ulipo. Na bado-majengo yatatumbukia ardhini, malori ya mafuta kugonga majumba ya barabarani na kuua maelfu tusipozingatia sheria. Future unayoisema hapa ni ipi ambapo kila mmoja anauza samaki wa kukaanga kawaweka wazi wamejaa mainzi? boxi la waya au kioo analitumia tu kama kuna ukaguzi mkali ukiisha ukaguzi karudi kuwaweka katika sinia mainzi kibao. future ipi ambapo tunaangalia sifa tu sio matendo ya kisayansi. Wanajenga mabondeni toka mto unakopita Mbagala juu hadi mtoni, Tabata, Buguruni hadi Jangwani-twawaangalia tu kisha kuingia gharama ya matibabu mahospitali, uokoaji nao walivyotaahira, badala ya kuhama amepoteza familia na mali anasema-sihami nimezoea kuishi hapa. Future gani wakati unajua desturi za watu wako-badala ya kuchukua kampuni ikawajengea nyumba low cost ukawakabidhi-unawapa mabati na simenti lundo. Watauza baadhi kufanya sherehe kababmbe ya Arusi, mtoto kutoboa masikio etc badala ya kujenga. Utawakuta mahemani mpaka 2015. Future gani ambapo unaelewa tatizo la Mto Ng'ombe (mto Ubungo) ni wato kuufanya sewerage canal na eneo na utupaji takataka ngumu, taka maozo na taka maji. Kinachotakiwa mto unapopita mjini ni kuufanya kama Thames River wa UK mbona maijinia wamefika huko pamoja na Holland? Solution sio kuupanua!! Yaani kuwaongezea nafasi ya kuujaza takataka. Kuupanua kwa kuuchimba, kuzoa takataka kila baada na kabla ya mvua ni mbinu nzuri lakini inawapa nafasi ya kuongeza utupaji taka hizo na kuunganisha vyoo. Mikakati bora zaidi kuliko hii ifanyike kwa kutumia a multi-sectoral team ya wataalamu na kuwahusisha wananchi ili tabia ya uchafu ikomeshwe. Kuupanua si tija. Kuwajengea daraja la kuvuka kule jangwani bondeni ni kuwapa Ari ya kuendelea kukaa huko. Kuboresha miundombinu halafu wakauza eneo na kuhamia eneo hatarishi zaidi-Bomoa mara unapoona ujenzi unaanza. CIUPs project ziangalie hili. Zinaboresha kwa mkopo wa World bank, wanauza, wanahamia bondeni zaidi, wanazama, wanalalama serikali mbaya haitujali!! Hakuna future nzuri, hatujipendi, tu vipofu, viziwi, viwete tusio na hata wheel chair. zaidi ya vyote-Tu Vinyonga-hatuishi vigeugeu. Na sasa tuna malumbano ya nani achinje mifugo. Chinja kula mwenyewe. kama ni tatizo-kila dhehebu liwe na bucha lao lililoko karibu na mahekalu yao au maeneo yao ili yaishe. Hii nayo issue ya kuuana? twakuza vitu visivyo maana, why. Twachomeana majumba wakulima na wafugaji-hutaki kupunguza mifugo ufuge kisasa-kaa kwako kwenye asili yako ekari moja ukae na hao mifugo elfu 10. Umeoa wake 5 na una vyumba 2 na una watoto 30-utajiju wewe, uwape shida wengine why? Unaelewa ukomo wa nafasi ya chumba na nyumba, ukomo na uwezo wa ardhi-unataka jamii ikifanye nini unavyolimbikiza mifugo kuharibu mazingira yake? Hata upelekwe study tour ndani na nje ya nchi ukaone wenzako walivyobadilika-hutaki kubadilika. Ndio kwanza unavuna madini unajaza mifugo na familia kuwa kubwa katika karne hii ya climate change na UKIMWI. Pamoja na mlimbikizo huo wa mifugo-haupo tayari kuchangia uniform za mtoto na kiatu chacke na madeski-wanasoma kibanda cha nyasi, wamevaa kinyumbani, wamekaa chini. Serikali haitujali!! Ni sawa kule mjini wanakoelekeza vinyesi miferejini na kutupa taka nzito kisha mvua ikija yale yote watupayo wenyewe yanawarudia ndani ya vyumba na nyumba zao wao, kuyakoga na kuyanywa wanapozama-Serikali itupanulie mifereji ili taka hizi zisitudhuru!! Excuse me Chipalazya!! --- On Mon, 1/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment