Umeielezea vizuri sana Japhet.
Tatizo pekee la Fastjet ni kusimamia kile wanachokisemka na walichokiandika kama ndio muongozo wao. Unajua waswahili tumezoea kuwa kila kitu lazima kiwe na room ya ku-compromise, utakuta mtu yuko benki chini ya alama ya usitumie simu yeye anapiga simu. Ukimuuliza anakwambia mwanangu mgonjwa au nina tatizo hili na lile.
Kupitia hili la Fastjet tujifunze kuwa sio kila mahali au kila kampuni ina uswahili wa ku-compromise kwenye kanuni zao. Kwenye hili mimi sina cha kuwalaumu Fastjet........................
2013/4/28 Japhet Makongo <japhetmakongo@yahoo.com>
Mh! Nawasikia wa-TZ,Kwangu wote hawa-precision au fastje ni matatizo tupu-hawana ubinadamu. Precision kazidiwa mzigo, na kama punda hasemi ila mwenyewe ugundue tu. Fasrtjet anajua nachokifanya na kama baadhi ya wenye punda hajali hata kama anajua mzigo huo unakuumiza.
Precision anatkiwa kujua kuwa anamiza watu kwa kutotoa mawasiliano na kuwa muungwana katika ahadi yake ya kutoa huduma. Lakin ia fasjet, kama nimpata mtoa hoja yeye hajali kama unaumia...kanuni alizoweka n ngumu sana kutekelezeka katika mazingira ya tz. kuchelewa folen, ukiwa na dharura bas ticket imeenda. ukibadili safari unalipa kma ticket mara mbili, nk. Mimi nilikuwa na safari nikakwama kutoka bagamoyo kwa ajli a foleni tegeta..nikapiga simu wakasema hawawezi kubadlisha hadi nifike mwenywe ofisini na kulipa nyongeza ya badiliko.... tshs 40,000! Sikuwahi kufika kwa muda na tiketi ikaendaHoja yangu inarudi kwa serikali kama msimamizi wa huduma kuu za wananchi...tuwaombe waanglie wajibu wao wa kutetea wanynge......Makongo----------------------------------------------------------------Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
From: Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: Mussa Mziya <mkmziya@yahoo.com>
Sent: Saturday, April 27, 2013 10:46 PM
Subject: Re: [wanabidii] FASTJET – KASUKU MWENYE KUCHA ZA SIMBA?
Kuna siku na Mimi niliapa Kwamba sintosafiri na Pecision tena kwa jinsi walivyotutesa kwa kutuacha Mwanza kuanzia saa mbili usiku hadi saa Sita, kila baada ya MUDA wanasema tutaondoka baada ya muda mfupi.Serikali haiwezi na nadhani hawana nia kuboresha usafiri wa anga hapa kwetu. Angalia masaibu yanayoipata ATC hewani, labda tupange kuwapeleka mahakamani hawa wanaotusumbua.Nawasilisha
On Saturday, April 27, 2013, Mussa Mziya wrote:--
Ndugu zangu;Kwa mara ya kwanza wakati shirika la ndege binafsi la fastjet linaanza kazi hapa nchini, lilionekana kama ni mkombozi kwa wananchi wanyonge, wasio na uwezo mkubwa kusafiri na ndege! Kadri siku zinavyosogea shirika hili ndivyo linavyokunjua makucha yake na kuonyesha kwamba ni chui aliye ndani ya ngozi ya kondoo. FastJet imekuwa ikiwaimbisha wananchi wanyonge na nauli yake ya 32,000 tu! Ilhali ni wananchi wachache sana wanaopata nafasi katika daraja hili la chini.Mbali na nauli zake zinazobadilika kama kinyonga wa jangwani, lakini sera zake (policy) zimejilenga kujineemesha zaidi na kuwadhulumu wananchi wanyonge. Mfano usiposafiri hata kwa dharura gani, huwezi kurejeshewa fedha zako. Pia huwezi kubadilisha tarehe ya kusafiri hata kama una dharura ya namna gani, bila kulipa fedha nyingi, wakati mwingine hata kukaribia bei ya tikiti mpya, inginevyo itabidi tiketi hiyo ipotee na uje ukate nyingine. Moja ya sera zake unapotaka kubadili muda wa safari inasema '' Fare difference may be substantial'' (tofauti ya nauli inaweza kuwa kubwa) bila kuonyesha kiasi cha ukubwa wenyewe mpaka pale watakapokuwa wamebadili, wakati ambapo ni lazima ulipe kwani tayari watakuwa wameshaiuza kwako.Labda nieleze kisa kilichonipata jana na leo:Jana: Kuna ndugu yangu aliyekuwa asafiri kwa ndege FN 0161 kutoka Dar kuja Mwanza leo asubuhi (ambayo ndiyo ilifutwa) lakini kwa bahati alibadilisha muda na kusafiri jioni kutokana na dharura iliyompata. Ilibidi alipie kiasi cha Shs. 56,000 (ziada ya bei aliyonunulia tikiti ya Shs. 155,000/= one-way) kubadili tu huo muda wa safari. Lakini dharura ile iliendelea na ikabidi niombe tena kumbadilishia safari iwe kasho asubuhi. Hapo kwa mujibu wa utaratibu wao, system ika charge malipo ya 40,000/= kama adhabu (penalty) ya kubadili safari na malipo ya ziada ya Shs. 104,000/= kwa 'kosa' hilohilo la kubadili safari kwa dharura. Sasa ukijumlisha malipo tuliyolipa kwa safari ya one-way ni 155,000 + 56,000 + 40,000 + 104,000 = 355,000!!! Kwa safari moja tu (one-way Dar/Mwz) Sawa taratibu ni taratibu, lakini taratibu za hawa ndugu zetu ni za dhulma kubwa. Kumbe yule kasuku mzuri tunayemwona, ana kucha za Simba!.Leo: Nilikuwa nisafiri na ndege hiyo ya fastJet flight No. FN 0162 kutoka Mwanza kwenda Dar-es-Salaam saa 2:50 asubuhi. Ndege hiyo ilifutwa (cancelled) kwa sababu tuliyoelezwa kuwa ni ya kiufundi. Tukaambiwa tutasafirishwa kwa ndege yao ya jioni saa 11. Lakini cha ajabu, tofauti na utaratibu unaotumika na mashirika mengi ya ndege ''serious'' duniani hakukuwa na msaada wowote (consideration) kwa wasafiri ukizingatia wasafiri hawa wametumia fedha kukodi taxi kuwaleta uwanja wa ndege. Tulifika airport kwa gharama zetu, tukaondoka kwa gharama zetu na kurudi tena jioni kwa gharama zetu. Sasa ilipokuwa ni dharura kwa upande wangu mimi mteja, wakanichaji fedha nyingi (355,000) eti kwa usumbufu walioupata kubadili safari. Sasa iweje na wao wanapokuwa na dharura za kuharibikiwa na ndege hawatujali hata kwa nauli ya taksi? Achilia mbali suala la wasafiri kupelekwa hotelini na kurudishwa wakati wa safari!Nadhani wakati umefika sasa kwa Serikali kupitia mamlaka husika (nadhani ni mamlaka ya safari za anga) kuchukua hatua za makusudi kuangalia na kuridhia taratibu (policies) za mashirika haya ya ndege ili ziwe fair na zisiwadhulumu wananchi kiasi hiki. Nadhani hii itakuwa ni safari yangu ya kwanza na ya mwisho kusafiri na Kasuku huyu mwenye kucha za Simba (FastJet) na nawapongeza PRECISION AIR kwa utaratibu wao mzuri wa 'KIUTU' wa kuwajali wateja wao.Mussa
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Ezekiel J. Massanja
Director of Finance and Administration
Legal and Human Rights Centre
P.O. BOX 75254
Dar es Salaam
Tel: +255 22 2773038, 2773048
Fax: +255 22 2773037
Cel: +255 754 283593
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Wasalaam,
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
" Low aim, not failure, is a crime"
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment